Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 34162 articles
Browse latest View live

Zenj Empire Islamic Festival


Wateja wa Zantel na Tigo Sasa Kufurahia Huduma Salama na Yauhakika ya Kutumiana Fedha kwenye Mitandao yao kwa 100%.

$
0
0
Watendaji wa Kampuni za Simu za Zantel na Tigo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace kuitambulisha huduma ya kutuma fedha kupitia mitandao hiyo bila ya gharama kubwa hutumika kwa gharaza za kawaida za makampuni hayo, kutoka kulia Mkurugenzi wa Huduma za Fedha Zantel Mr.Hashim Mukudi, Mkurugenzi Biashara Zantel Mr Mohammed Khamis Mussa Baucha, Mkuu Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr.Andrew Hodgson na Meneja Chapa Mr. William Mpinga.
Mkurugenzi Biashara Zantel Mr Mohammed Khamis Mussa (Baucha) akizungumza na waandishi wa habari uzinduzi wa huduma za utumiaji wa huduma ya Fedha kwa mitandao ya Zantel na Tigo kwa wateja wa makampuni hayo kuweza kutuma fedha kwa mteja wa Tigo kwenda kwa Zantel kwa kiwango cha gharama cha kawaida kama unavyotuma fedha kwenda kwa Zantel kwa Zatel na kwa Tigo hali kadhalika, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar. 
 Mkuu Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr.Andrew Hodgson, akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar, kuwajulisha wateja wa Togo wanaweza kutuma fedha kwenda Zantel bila ya gharama kubwa makato yake kama unavyotuma fedha kwenda Tigo kwa Tigo. 
Mkurugenzi wa Huduma za Fedha Zantel Mr.Hashim Mukudi, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo kwa waandishi wa habari kuhusiana na huduma hiyo ya ushirikiano na kampuni ya Tigo kuweza kutumia viwango sawa wakati wa kutumiana fedha mteja wa Zantel kwenda Tigo.
Meneja Chapa Mr. William Mpinga, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kuhusiana na huduma hiyo kwa wateja wa Tigo kuweza kutuma fedha kwenda Zantel.

Waandishi wakifuatilia uzinduzi huo wa Zantel na Tigo kutowa huduma bora kwa wateja wake kupitia huduma ya fedha kwa wa Tigo na Zantel bila ya gharama kubwa. 

Maofisa wa Kampuni ya Simu ya Zantel wakiwa katika ukumbi wa Grand Palace Malindi wakifuatilia uzinduzi huo wa Zantel na Tigo kutowa huduma ya Fedha kwa Wateja wa mitandao hiyo miwili bila ya kutozwa gharaba kubwa. 
Mkurugenzi Huduma ya Fedha Zantel kulia Mr.Hashim Mukudi, wakipongezana na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr Andrew Hodgson, baada ya hafla ya kuitambulisha huduma hiyo kwa Wananchi wa Zanzibar kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar leo.kwa kutuma fedha kupitia mitandao ya Zantel na Tigo kwa kutumia gharama za kawaida za kampuni hizo.
Mkurugenzi Huduma ya Fedha Zantel kulia Mr.Hashim Mukudi, wakipongezana na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha Tigo Mr Andrew Hodgson, baada ya hafla ya kuitambulisha huduma ya kutuma fedha kupitia mitandao ya Zantel na Tigo kwa kutumia gharama ya kawaida ya kampuni hizo inayokatwa kwa kutuma fedha kwenda Zantel na Zantel, kulia Mkurugenzi wa Miradi wa Zantel Bi Shihuna Kassim na Mkurugenzi Biashara Zantel Mr. Mohammed Khamiss Mussa na kushoto Meneja Chapa wa Togo Mr William Mpinga, wakifurahia udugu huu baada ya kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
Viongozi wa Kamuni za Simu za Zantel na Tigo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuutambulisha uhusiano wao kwa Wateja wao kupata huduma ya kutumiana Fedha kupitia mitandao hiyo. utambulisho huo umefanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.

Tigo and ZANTEL customers to enjoy 100% secure and reliable Mobile Money services across their networks

$
0
0
                          


PRESS RELEASE


Tigo and ZANTEL customers to enjoy 100% secure and reliable Mobile Money services across their networks


Zanzibar, 17th December 2014. Tigo and ZANTEL have officially launched the mobile money interoperability service in Tanzania that will open up a number of mobile money transactions between the customers’ of the two telecom operators. In addition to transactions within their own network, EzyPesa and TigoPesa customers are now able to send and receive cash direct to and from customer friends and family on their partner networks across the country.


This places Tigo and ZANTEL among the pioneers of this service in the world, a progressive initiative announced by EzyPesa, TigoPesa and Airtel Money early this year.


How it works


Zantel Customers:

Tigo Customers:

1.      Dial *150*02#

1.      Dial *150*01#

2.      Choose : Option 1 (Send Money)

2.      Choose : Option 1 (Send Money)

3.      Choose : Option 2 (Send to TigoPesa)

3.      Choose : Option 5 (Send to EzyPesa)

3.1.   Enter TigoPesa Number

3.1.   Enter TigoPesa Number

3.2.   Enter Amount

3.2.   Enter Amount

3.3.   Enter Password

3.3.   Enter Password

3.4.   Wait for the confirmation SMS

3.4.   Wait for the confirmation SMS


There is no surcharge for sending money across networks and charges are priced the same as sending within their home network.  Customers receiving money from another network can cashout from their own networks agents and no longer have to find agents from the other network.


Tigo’s Head of Mobile Financial Services, Andrew Hodgson, said, “We are delighted to expand our customers transacting capacity through our partnership with Zantel. By expanding our customer’s mobile money ecosystem, particularly in Zanzibar where there is still a lot of potential for mobile financial services growth.  


Similar to other telecommunication services like voice calls and text messages there are often huge opportunities to improve the customers experience by cooperating rather than only competing with industry partners massively expanding the digital financial inclusion in Tanzania.



Through our partnerships with other industry players we are able to expand our customer’s digital world by leveraging existing technology to effectively combine our mutual customer base, thereby exponentially expand the transactional ecosystem potential. In this way we are able offer additional convenience in terms transaction versatility, speed, safety and security to both our own, and our partner’s customer base.


Indeed today’s partnership will bring our two companies closer together but it more importantly will bring our customers even closer, by providing access to electronic and digitized financial service that they were never previously able to access,”  Hodgson added.


Zantel’s Commercial Director, Mohamed Mussa, commented that Zantel continues to fulfil its promise of bringing ease to its customers by enabling them with financial mobility through their partnership with Tigopesa.


By doing this we have increased the mobile money spectre for our customers, this new transaction type enables customers interact with bigger addressable market for sending and receiving money. 

We have increased scope in financial participation for our two sets our customers by combining our core business strongholds and tapping on one of the most important financial transaction corridors between Zanzibar and Mainland, concluded Mr. Mussa.


Zantel is at the fore front to ensure the rate of financial inclusion and financial participation in Zanzibar is improves. We have ensured our Agent network and the support agency mechanism are in place to serve the customers.


About Zantel

Zantel currently serves a growing subscriber base and consistently demonstrates its core values of affordable, consistent and seamless services. Zantel believes that apart from offering a solid platform of technological innovation, sustainable investment is the bedrock of stellar growth and economic stability.We offers International Gateway services, Fixed, Mobile , data services through its CDMA, GSM , 3G networks and mobile Finance services popularly known as ‘Ezypesa”. 


Zantel is part of Etisalat Group which has been recognized as “Best Operator” 10 times since 2006 and “Best Wholesale Provider” 4 times in the last three years servicing 145 million customers in 15 countries. Etisalat continues to reach out to new customers and markets.


For further information about Zantel visit; www.zantel.co.tz 

Arnold Madale – Senior Manager, Media and Brand

Mobile: 0779 222 344



About Tigo:


Tigo Tanzania is the leading innovative telecommunication company in the country, distinguished as a fully-fledged digital lifestyle brand. Offering a diverse product portfolio in voice, SMS, high-speed internet and mobile financial services, Tigo has pioneered innovations such as Facebook in Kiswahili, Tigo Pesa App for Android & iOS users, and East Africa’s first cross-border mobile money transfer with currency conversion. 


The Tigo 3G network guarantees the best services to its subscriber’s in all regions across the country.  Between 2013 and 2014 alone the company launched over 500 new network sites and plans to double its investment by 2017 in terms of coverage and additional capacity networks for deeper penetration in rural areas. With over seven (7) million registered subscribers to their network, Tigo directly and indirectly employs over 100,000 Tanzanians including an extended network of customer service representatives, mobile money merchants, sales agents and distributors.


Tigo is the biggest commercial brand of Millicom, an international company developing the digital lifestyle in 44 countries with commercial operations in Africa and Latin America and corporate offices in Europe and the USA. With the certain knowledge that only constant innovation will keep them on top, Millicom keeps creating greater shareholder value; applying their concept of “demand more” is how they do business and retain their position as digital lifestyle leaders in some of the most unique and challenging markets.


“SMILE, YOU’RE WITH TIGO”


For further information about Tigo visit:  www.tigo.co.tz  Or contact:

John Wanyancha – Corporate Communications Manager

Mobile: 0658 123 089


Wateja wa Tigo na ZANTEL sasa kufurahia huduma salama na uhakika ya kutumiana fedha kwenye Mitandao yao kwa 100%

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Wateja wa Tigo na ZANTEL sasa kufurahia huduma salama na uhakika ya kutumiana fedha kwenye Mitandao yao kwa 100%

  
Zanzibar - 17 Desemba, 2014. Kampuni za simu za mkononi za Tigo na ZANTEL zamezindua rasmi huduma za kutumiana pesa miongoni mwa wateja wake Tanzania.  Mbali na huduma hiyo ya kutumiana pesa miongoni mwa wateja wa mitandao hiyo, wateja wa EzyPesa na TigoPesa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kwa marafiki na ndugu walio katika mitandao hiyo popote pale nchini.


Kutekelezwa kwa mpango huo kunazifanya Tigo na ZANTEL kuwa viongozi wa huduma kama hiyo Duniani.  Haya ni matokeo ya makubaliano yaliyotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu na EzyPesa, TigoPesa na Airtel Money.  


Jinsi Huduma hiyo inavyofanya kazi:


Wateja wa Zantel:

Wateja wa Tigo:

1.      Piga *150*02#

1.      Piga *150*01#

2.      Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)

2.      Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)

3.      Chagua: Chaguo la 2 (Tuma TigoPesa)

3.      Chagua: Chaguo la 5 (Tuma EzyPesa)

3.1.   Ingiza Namba ya TigoPesa

3.1.   Ingiza Namba ya TigoPesa

3.2.   Ingiza Kiwango

3.2.   Ingiza Kiwango

3.3.   Ingiza Neno la Siri

3.3.   Ingiza Neno la Siri

3.4.   Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno

3.4.   Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno


Hakuna gharama za ziada mteja anapotuma pesa kwa mtandao mwingine isipokuwa gharama zinakuwa sawa na zile anapotuma kwenye mtandao wake.  Wateja wanaopokea pesa kutoka mtandao mwingine wanaweza kutoa pesa kwa wakala wa mtandao wao na hapatakuwa tena na ulazima wa mteja kutafuta wakala wa mtandao wa mtu aliyemtumia pesa.


Akizungumza kutoka Zanzibar, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Andrew Hodgson alisema: “Tunafuraha kupanua wigo kwa wateja wetu kwa ubia na Zantel.  Hatua hii ni muhimu hasa kwa Zanzibar ambapo fursa ya kukua kwa huduma za fedha kwa mitandao ya simu bado ni kubwa.”


Anasema kama ilivyo kwa huduma nyingine za simu kama milio ya sauti na ujumbe mfupi wa maneno, kuna fursa kubwa ya kuimarisha huduma kwa wateja kwa kushirikiana badala ya kushindana baina ya wadau katika sekta ya mawasiliano kwa kupanua huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao Tanzania.

Anafafanua zaidi kuwa kwa kufanya kazi na wadau wengine, kunawawezesha kupanua wigo wa wateja na hivyo kwa pamoja kutoa huduma ambazo ni bora zaidi, salama, na za haraka kwa wateja wa pande zote.

“Ubia ambao tumeingia leo sio tu utaleta karibu kampuni zetu, bali muhimu zaidi ni ukaribu wa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za fedha za kielektroniki bora zaidi ambazo hawakuweza kuzipata hapo awali,” alisema Hodgson. 

Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed Mussa, anasema Zantel inaendelea kutimiza ahadi ya kuwarahisishia huduma za fedha wateja wake kwa kufanya kazi pamoja na Tigopesa.


“Kwa kufanya hivi tunapanua wigo kwa wateja wetu, huduma hii inawawezesha zaidi wateja kutuma na kupokea fedha kwa urahisi zaidi,” anasema.


Anafafanua zaidi kuwa kwa huduma hii itasaidia kuimarisha huduma za fedha kati ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania Bara.


“Zantel iko katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa ushiriki wa wananchi wa Zanzibar katika sekta muhimu ya fedha unaimarika na kukua.  Tumehakikisha kuwa mtandao wa mawakala wetu na watoa huduma wengine wako tayari kuwahudumia wateja wetu,” anasema Bw. Mussa.

 

About Zantel

Zantel currently serves a growing subscriber base and consistently demonstrates its core values of affordable, consistent and seamless services. Zantel believes that apart from offering a solid platform of technological innovation, sustainable investment is the bedrock of stellar growth and economic stability.We offers International Gateway services, Fixed, Mobile , data services through its CDMA, GSM , 3G networks and mobile Finance services popularly known as ‘Ezypesa”. 

Zantel is part of Etisalat Group which has been recognized as “Best Operator” 10 times since 2006 and “Best Wholesale Provider” 4 times in the last three years servicing 145 million customers in 15 countries. Etisalat continues to reach out to new customers and markets.

For further information about Zantel visit; www.zantel.co.tz

Arnold Madale – Senior Manager, Media and Brand

Mobile: 0779 222 344






About Tigo:


Tigo Tanzania is the leading innovative telecommunication company in the country, distinguished as a fully-fledged digital lifestyle brand. Offering a diverse product portfolio in voice, SMS, high-speed internet and mobile financial services, Tigo has pioneered innovations such as Facebook in Kiswahili, Tigo Pesa App for Android & iOS users, and East Africa’s first cross-border mobile money transfer with currency conversion. 


The Tigo 3G network guarantees the best services to its subscriber’s in all regions across the country.  Between 2013 and 2014 alone the company launched over 500 new network sites and plans to double its investment by 2017 in terms of coverage and additional capacity networks for deeper penetration in rural areas. With over seven (7) million registered subscribers to their network, Tigo directly and indirectly employs over 100,000 Tanzanians including an extended network of customer service representatives, mobile money merchants, sales agents and distributors.


Tigo is the biggest commercial brand of Millicom, an international company developing the digital lifestyle in 44 countries with commercial operations in Africa and Latin America and corporate offices in Europe and the USA. With the certain knowledge that only constant innovation will keep them on top, Millicom keeps creating greater shareholder value; applying their concept of “demand more” is how they do business and retain their position as digital lifestyle leaders in some of the most unique and challenging markets.


“SMILE, YOU’RE WITH TIGO”


For further information about Tigo visit:  www.tigo.co.tz  Or contact:

John Wanyancha – Corporate Communications Manager

Mobile: 0658 123 089






Magazetini Bongo Tz

Wadau wa utalii Ufaransa wachangia gari tano

$
0
0
Na Joseph Ngilisho, Arusha
Wadau wa sekta ya utalii nchini Ufaransa, wameisaidia Tanzania magari matano aina ya Toyota Land Cruiser yenye thamani ya shilingi 599,338,330, yatakayotumika kupambana na ujangili katika maeneo mbalimbali yenye uhifadhi wa wanyama pori nchini.


Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu na mwakilishi wa wadau hao hapa nchini,Mohsin Shem,ambaye alieleza kuwa msaada huo umetokana na michango ya taasisi mbalimbali za kusaidia na kupambana na ujangili nchini humo.


Alisema gari hizo zitasaidia kupunguza changamoto inayotokana na ujangili,unaosababisha sekta ya utalii kushuka,kupoteza watalii wa ndani na nje pamoja na kutoweka kwa wanyama ambao ni kivutio kikubwa cha utalii nchini.


“Kwa umoja uliooneshwa na taasisi za utalii,wameahidi kuendelea kutoa misaada mingine mingi ikiwemo vitendea kazi vya kupambana na ujangili,lengo ni kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya uharamia wa wanyama nchini,” alisema.



Waziri Nyalandu aliwashukuru wadau hao na kusema suala la ujangili nchini bado ni kubwa, hivyo alitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza kupiga vita vitendo vya ujangili ili kutokomeza kabisa.


Hata hivyo,alisema serikali ipo mbioni kunununua helkopta mbili zitakazotumika kuongeza nguvu kwa kufanya doria maeneo mbalimbali ya uhifadhi,huku helkopta iliyoanguka hivi karibuni ikiwa mbioni kulipwa na bima.



Aidha alisema serikali inakabiliwa na uhaba wa marubani,ambapo aliitaka jamii kujitokeza kusomea urushaji wa ndege ili kupunguza changamoto hiyo,hata hivyo alizishukuru kampuni mbalimbali za uwindaji zaidi ya 50 zilizojitokeza kumsomesha rubani wa kike,Anna Lorayo (32) atakayesaidia kurusha ndege kwa ajili ya doria ya kupambana na ujangili.

Miti shamba yachangia watoto kuzaliwa wafu Kivunge

$
0
0
Na Fatma Kassim
Imebainika wazazi wengi wanaofika hospitali ya Kivunge kujifungua wanapata watoto wafu kutokana na matumizi ya kupindukia ya dawa za miti shamba.


Matumizi ya dawa hizo pia wakati mwengine husababisha kuzaliwa watoto wakiwa na afya dhaifu na kupata magonjwa ya kudumu.


Matatizo mengine ni kuongezeka kasi ya uchungu kwa mjamzito na kusababisha mtoto kufia tumboni, kuzaliwa akiwa amechunika ngozi, wakati mwengine husababisha kuchanika fuko la uzazi na baadae mama hushuka kizazi.


Asha Haidar  mwenye umri wa miaka 32 mkaazi wa  Pitanazako wilaya ya kaskazini ‘A’ mkoa wa kaskazini Unguja, alifikishwa hospitali ya Kivunge Disemba 6 na anasema lipotoka nyumbani  tayari alikuwa amepewa dawa na mama yake kwa lengo la kukazisha uchungu ili akifika hospitali ajifungue mara moja.


“Na dawa za miti shamba nimeanza kutumia tangu ujauzito wangu una miezi minne na nimetumia dawa hizi kwa lengo la kuondoa maumivu nnayoyapata tumboni pamoja na mtoto wangu awe na afya njema na wakati nimeanza uchungu nikiwa nyumbani nimepewa dawa na uchungu ulikuwa na kasi,” alisema.



Aidha alisema aliugua kwa siku nzima bila kujifungua na siku ya pili kwa jitihada za madaktari alijifungua mtoto akiwa tayari ameshafariki tumboni.


Mama wa Asha, Mwatima Ali, alisema ni utamaduni wao kutumia dawa za asili kwa sababu zinaimarisha afya ya mjamzito na wakati wa kujifungua hujifungua mara moja.


Dk. Khamis Hamad Ali, alisema jamii katika mkoa huo imekuwa na hamasa ya matumizi ya dawa za miti shamba kwa wajawazito tangu mimba ikiwa changa, tatizo linalosababisha kujifungua watoto wakiwa wameshafariki.


“Jamii imekuwa na utamaduni wa matumizi ya dawa za miti shamba ambapo matumizi yake kwa kiasi kikubwa yanakiathiri kiumbe kikiwa tumboni na hatimaye kujifungua wakiwa wameshakufa,” alisema.


Katika kubabiliana na tatizo hilo, alibainisha kuwa wamekuwa wakiwaelimisha wajawazito athari za matumizi ya dawa hizo kwa afya za watoto tangu wanapohudhuria kliniki athari za matumizi ya dawa hizo.


Alisema wamekuwa wakiwaelimisha wakunga wa jadi hasa kwenye mikutano ya afya za vijijini ambapo hutumia fursa hiyo kuwaeleza athari za matumizi ya   dawa hizo pamoja na umuhimu wa mjazito kuzalia hospitalini na wasiwazalishwe na wakunga wa jadi.


Alisema tangu Disemba 1 hadi 10 jumla ya watoto watatu wamezaliwa wakiwa wafu kutokana na matumizi ya dawa za miti shamba.


  

Elimu kwanza ndio mbiu ya Ujumbe wa Makunduchi Wakiwa Ziarani Nchini Sweden

$
0
0

Manispaa ya Sundsvall, Sweden yapeperusha bendera ya Zanzibar kuonyesha heshima yao kwa ujumbe wa wadi za Makunduchi wakati ndugu Magnus Braxenholm akitoa maelezo kuhusu muundo wa Manispaa ya
Sundsvall pamoja na kazi zake za kila siku. Maelezo hayo yalitolewa kabla ndugu Hafifth bin Ameir (senior citizen of Makunduchi) hajahutubia Baraza la Manispaa (Sundsvall Municipal Assembly) lenye wajumbe zaidi ya 100.


Mtaalamu wa elimu kutoka Manispaa ya Sundsvall ndugu Roy Resare akitoa maelezo kwa ujumbe wa Wadi za Makunduchi (hawapo kwenye picha) kuhusu mikakati ya Manispaa kuwa na Skuli bora nchini Sweden na duniani kote ifikapo mwaka 2021
Ujumbe wa wadi za Makuduchi na bendera ya Zanzibar katika picha ya pamoja na wenyeji wao ndanibya Jengo la baraza la Manispaa (Sundsvall Municipal Assembly). Kutoka kushoto mwalimu mkuu wa skuli ya Makunduchi, Kinore; ndugu Sweden; diwani Zawadi Hamdu; ndugu Mohd Simba; ndugu Mohamed Muombwa na ndugu Hafifth bin Ameir (senior citizen of Makunduchi)
Ujumbe wa wadi za Makunduchi wapata heshima ya kuhudhuria na kuhutubia ndani ya kikao cha Baraza la Manispaa ya Sundsvall (Sunesvall Municipal Assembly) Kwenye picha ndugu Hafifh bin Ameir (senior citizen of Makunduchi) akihutubia kwenye baraza lenye wajumbe zaidi ya 100. Katika hutuba yake ameelezea umuhimu wa mashirikiano kati ya Makunduchi na Manispaa ya Sundsvall. Huu ulikuwa ni mkakati wa wadi za Makunduchi kuwashawishi wajumbe wa Baraza kupitisha kwa kishindo mashirikiano ya sekta ya elimu.
Miongoni mwa mikakati ya wadi za Makunduchi ni kuitangaza Zanzibar kiutalii pamoja na biashara ya wanawake wa Makunduchi. Diwani Zawadi Hamdu akimkabidhi zawadi ya kipochi cha ukili bi. Christin ambaye ni mratibu wa mashirikiano.
"Ahaaa unapendeza bi Christin!"Hayo ndiyo maneno aliyonena diwani Zawadi baada ya kumaliza upambaji

Ujumbe wa Katuni Huooooooooooo.....

Wananchi Wakifuatilia Habari za leo Magazetini Zenj.

$
0
0
Wananchi wakifuatilia vichwa vya habari vilivyoripoti habari ya kujiuzuu kwa Mwanasheria Mkuu ikiwa magazeti yote yamepamba habari hiyo, Wakiwa katika moja ya kituo cha kuuzia magazeti darajani Zenj.

Maalim Seif Ziarani Nchi Uturuki

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa jumuiya za watembezaji watalii nchini Uturuki.
Baadhi ya viongozi wa jumuiya za watembezaji watalii nchini Uturuki, wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (hayupo pichani) walipokutana naye kwa mazungumzo mjini Istanbul nchini Uturuki. (Picha na Salmin Said, Istanbul).

Tatizo la Wamachinga na Ombaomba maeneo yasioruhusiwa Dar Kutafutiwa Dawa.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akifuangua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.


Na.Aron Msigwa –MAELEZO.
Jiji la Dar es salaam linaangalia upya utaratibu wa kuwaondoa ombaomba na wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga) katika maeneo yasiyoruhusiwa katika jiji la Dar es salaam kufuatia sheria na hatuazinazochukuliwa ikiwemo kuwarudisha ombaomba hao katika mikoa wanayotoka kutokuzaa matunda na kuwa endelevu kufuatia wengi wao kurudi katika maeneo ya awali kila wanapoondolewa.
 
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki wakati akifuangua kikao cha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) kilichofanyika leo jijini Dar es salaam kujadili masuala mbalimbali ya mendeleo katika jiji la Dar es salaam.
 
Amesema kuwa kuendelea  kuwepo kwa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi ni moja ya changamoto inayolikabili jiji la Dar es salaam kutokana na biashara wanazozifanya kuchangia kuzuia maeneo ya barabara ya waenda kwa miguu, kusababisha uchafuzi wa mazingira,kusabisha msongamano wa magari kwa baadhi yao kuweka bidhaa barabarani.
 
Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara walio na biashara rasmi ambao hulipa kodi za Serikali wamekuwa wakilamikia hali  ya ukwepaji wa kodi inayofanywa na wafanyabiashara hao.
 
Bw. Sadiki amesema mpango wa mkoa wa sasa ni kuendelea kuwatumia wafanyabiashara hao kama  fursa ya mtaji wa rasilimali watu ambayo itatumika kama chanzo cha mapato katika kuleta maendeleo ya mkoa.
 
Amesema watendaji na viongozi wa halmashauri za mkoa wa Dar es salaam wanalojukumu la kuweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na kuwatumia katika shughuli za uzalishaji kwa utaratibu mzuri utakaowekwa ili waendelee kunufaika na shughuli wanazofanya.
 
Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii zikiwemo za Maji, Elimu na Afya katika jiji la Dar es salaam  amesema kuwa Serikali inaendelea kuzijengea uwezo shule kwa kuongeza majengo ya madarasa, maabara na kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaofaulu elimu ya msingi wanapata fursa ya kuendelea na masomo ya Sekondari.
 
Kuhusu huduma za afya amesema kuwa mkoa unaendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la ghorofa nane, eneo la Magomeni katika manispaa ya Ilala litakalotumika kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto na kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 500.
 
“  Sasa tuko kwenye maandalizi ya ujenzi wa jengo maalum la kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika jiji la Dar es salaam litakalogharimu zaidi ya shilingi bilioni ishirini na moja, tayari benki ya Tanzania Investment Bank imeshakubali kutoa mkopo kwa ajili ya jengo hilo” Amesisitiza.
 
Aidha, katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa ufafanuzi kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima  Desemba 14 mwaka huu na kueleza kuwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam ambayo uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vurugu, uchaguzi huo utarudiwa ndani ya siku saba.
 
Ameeleza kuwa katika mkoa wa Dar es salaam uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika kwenye mitaa 561 lakini kutokana na changamoto mbalimbali ulifanyika kwenye mitaa 491 na kuahirishwa kwenye kata 70.
 
Amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa linaimarisha ulinzi na usalama wakati wa marudio ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika ndani ya siku 7 katika mitaa yote ambayo uchaguzi uliahirishwa .

Zanzibar cloves harvest in pictures

$
0
0

The archipelago of Zanzibar in Tanzania, sometimes known as the Spice Islands, was once 
the world's largest producer of cloves. It is still an important industry for farmers on
 the island of Pemba as the BBC's Ruth Nesoba found out during the harvesting of 
the flower buds which when dried are used as a spice in cooking, to flavour drinks 
like mulled wine and in medicine.
Worker harvesting cloves
The months of September, October and November are the crucial time of year for clove 
farmers on Pemba. It is the period of the short seasonal rains when the cloves are 
harvested by hand. Bunches on lower branches can be pulled off or shaken free.
Worker harvesting cloves
Harvesting is strenuous work. The bunches of cloves can be tucked away in dense
 foliage where they are difficult to get at.
Worker harvesting cloves up a tree
Clove trees can grow up to 15m (49ft) high. Farmers are often skilled climbers, scaling 
the trees to pull bunches off higher branches. Many people on the island depend on 
cloves for their livelihood. That has been the case since the trees were introduced from 
Indonesia around the turn of the 19th Century.
Workers involved in clove harvest
Here at Konde village, as in much of Pemba, every family member is expected to help. 
Men, women and even young children get up early to help pick the cloves. Scaling the 
trees is generally left to the men, while women and children gather the cloves that fall to
the ground.

Farmer laying out cloves for drying
The picked flower buds and leaves are carried in a gunny sack from the farmers' land to 
the villages. The crop is then sorted to separate the leaves from the buds. Both are left
 to dry in the sun. The dried leaves are crushed and can be used in perfumes and 
fragrances.
 They are also used in an oil which can have sanitary applications and is sometimes 
used in dentistry.
Drying cloves
The buds are dried on mats in the sun. At this time of year one often sees mats covered 
with drying cloves lying by the roadsides. The cloves are left out for about three days. 
As they dry, they release a sweet, heady aroma, which wafts throughout the island.
Carrying cloves to treatment centre
The cloves are then carried to the collection centre. There are three government-run 
collection centres in Pemba. Farmers from Konde take their crop to Chake Chake.
Sifting at clove treatment centre
Here the cloves are sifted by hand to remove dirt and other unwanted particles. 
It is a thorough procedure intended to ensure that the final product is of high quality.
Laying sifted cloves on mats
The sifted cloves are then laid out where they can be checked for quality and tested.
Weighing cloves
The final crop of dried cloves is then weighed. Each farmer is paid immediately. 
For every 90kg (198lb) sack a farmer receives $720 (£460). A 1kg bag fetches $8.
Officials checking cloves
The heaviness, dryness and smell of the cloves are checked. Indonesia is the biggest 
grower, importer and consumer of cloves, producing between 60,000 and 80,000 tonnes 
a year. But Zanzibar cloves from Pemba are in great demand, says Suleiman Jongo
the deputy director of Zanzibar State Trade Centre.
Bagging cloves at collection centre
"The cloves have a very strong aroma and the majority of the flower buds are large and 
intact, making them among the best in the world," Mr Jongo says.
Putting cloves in sacks at collection centre
The cloves are put in sacks and taken to the warehouse awaiting transportation to 
the packaging centre from which they will either be sold locally or exported for use in 
cooking, medicines, cosmetics, or clove cigarettes which are popular in Indonesia.
Source : BBC

Ofisi ya ZFA Taifa Ikiwa na kofuli

$
0
0
Ofisi ya Chama cha Mpira Zanzibar ZFA ikiwa na kofuli baada ya kuamriwa na Mahakama viongozi wake kusimamishwa na kuamriwa kuchanguliwa Uongozi wa muda, baada ya mmoja wa Kiongozi Makamu wa Rais ZFA Zanzibar Alhaj Haji Ameir Haji, kufungua kesi mahakamani.

Viongozi waliozuiliwa ni Rais wa ZFA Taifa Ndg Ravia Idarous,Makamu wa Rais ZFA Pemba Ndg, Ali Mohammed na Katibu Mkuu wa  ZFA Ndg.Kassim Haji.
Pia Mahakama imeagiza kuzuiya kwa muda akaunti mbili za ZFA, zilioko PBZ na KBC.
Pia wamezuiliwa kujiingiza kuingia katika masuala yoyote yanayohusu ZFA, hadi hapo zuio lililofunguliwa na walalamikaji litakaposikilizwa pande mbili pamoja.na kutoshiriki katika utayarishaji na matumizi ya Katiba mpya ya Chama hicho.
Mahakama imemuagiza Mrajisi wa Vyama vya michezo kuunda Kamati ya Muda.itakayosimamia masuala ya ZFA.

Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi wakiwa na Wenyeji wo.

$
0
0
Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi, Wazee wa Wanafunzi wa Sundsvall Gynasium. Wanafunzi wa skuli hi Ai wanategemea kuja kutembelea Makunduchi na wenyeji wao watakuwa Skuli ya Kusini ambayo ndio Skuli rafiki ya Sundsvall 


Waziri Haroun kwa Kushirikiana na (ILO) Wazindua Kitabu cha Sheria za Kazi katika lugha nyepesi ni Toleo Maalum kwa Ajili ya Wafanyabiashara Ndogondogo na za Kati.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman na Mkurugenzi wa (ILO) kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma wakizindua kitabu cha sheria za Kazi katika lugha nyepesi, katika Hoteli ya Double Tree Shangani Mjini Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman akizungumza na wageni waalikwa katika sherehe za Uzinduzi wa kitabu cha sheria za Kazi katika lugha nyepesi katika Hoteli ya Double Tree Shangani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya walikwa waliohudhuria katika Uzinduzi wa kitabu cha sheria za Kazi katika lugha nyepesi Hoteli ya Double Tree Shangani.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Maalim Seif Akiendelea na ziara yake Nchi Uturuki

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni mashuhuri baada ya kufika kwenye jumba la makumbusho la Melvana nchini Uturuki.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akipata maelezo ndani ya jumba hilo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akitembelea sehemu ya jumba hilo la makumbusho.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akitembelea hospitali ya rufaa ya Acibaden mjini Istanbul nchini Uturuki akiwa katika ziara yake kutembelea Nchini hiyo (Picha na Salmin Said, Istanbul).

Uwanja wa Gombani Ukiwa katika Ujenzi wa Njia ya Kukimbilial

$
0
0
Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Pemba Ndg Ali Nassor, akitowa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Habari, Mifugona Utalii Mhe.Mbarouk Juma Mlinde akiwa na Kamati yake wakitembelea uwanja wa Gombani Pemba,uwanja wa gombani ukiwa katika matayarisho ya kuwekwa Tatan .
Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Mifugo,Habari na Utalii wakimsikiliza Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Ndg Ali Nossor hayuko pichani wakati walipofika kuangalia maendeleo ya Uwanja wa Gombani Pemba 
 Mhe Mohammed Raza akiuliza swali baada ya kupata maelezo ya Uwanja wa Michezo wa Gombani Pemba, wakati wa ziara yao kisiwani Pemba. 
Waheshimiwa Wawakilishi wakimsikiliza Mhandisi wa ujenzi huo wa uwekaji wa Tatan katika uwanja wa Gombani akitowa maelezo ya ujenzi huo kwa Kamati hiyo ilipofika kuangalia maendeleo ya uwanja huo.

UZINDUZI WA UMEME DONGONGWE KATI UNGUJA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini  Unguja katika sherehe za Uzinduzi wa Umeme Kijijini hapo leo (kushoto) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdalla Ali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini  Unguja katika sherehe za Uzinduzi wa Umeme Kijijini hapo leo.
Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi baada ya kuzindua rasmi nishati ya Umeme katika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja leo, [Picha na Ikulu.]

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

  Zanzibar                                                                                                           18.12.2014

---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezindua umeme katika kijiji cha Dongongwe, Mkoa wa Kusini Unguja na kusema kuwa Serikali kuwapelekea huduma bora za kijamii, kiuchumi na maendeleo wananchi wake ni wajibu wake na kusisitiza kuwa hayo ndio malengo ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.


Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya kuzindua umeme katika kijiji cha Dongoongwe, kiliopo wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa na serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali wa Jimbo la Uzini na vitongoji vyake.


Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa kufikish huduma za umeme ambazo amezizindua leo, huduma za maji ambazo tayari zimeshafika kijiji hapo pamoja na barabara ni wajibu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kama Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ilivyoeleza.


Akinukuu Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika Ibara ya 10, Dk. Shein alisema kuwa Ibara hiyo imeeleza wazi kuwa  “Kwa madumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika nchi itakuwa ni wajibu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ...kutoa huduma za kutosha kwa ajili ya kuendeleza watu...”.


Aidha, Dk. Shein alisema kuwa maendeleo ni mchakato kwani ni jambo ambalo halikamiliki siku moja na badala yake huenda hatua kwa hatua hivyo Serikali itaendelea kuzipeleka huduma nyengine zilizobaki kijijini humo ikiwemo barabara na kuwaahidi wanakijiji hao kutengenezewa barabara yao hatua kwa hatua.


Dk. Shein alisema kuwa maendeleo hayachagui mtu wala eneo analotoka hivyo Serikali anayoiongoza itahakikisha inawapelekea maendeleo wananchi wote kwani hilo ndio jukumu la Serikali na pia ni malengo ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.



Alisema kuwa jitihada za kupeleka umeme vijijini ni kubwa sana kwa upande wa Unguja na Pemba na kusisitiza kuwa ingwa Zanzibar ni nchi ya mwanzo katika Afrika Mashariki kwua na umeme katika mwaka 1875 lakini sio watu wote waliobahatika kuupata.


Akitoa historia ya huduma hiyo hapa Zanzibar Dk. Shein alisema kuwa matumizi rasmi ya umeme kwa kisiwa cha Unguja yalianza mwaka 1908 na kwa kisiwa cha Pemba ni mwaka 1959 na kusema kuwa wananchi walio wengi walianza kupata huduma za umeme mara baada ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.


Dk. Shein alisema kuwa Mapinduzi ya Januari 12,1964 ndio yalioleta maendeleo ikiwemo kusambaza huduma za umeme kwa wananchi.


Aliongeza kuwa watawala wote walioitawala Zanzibar wakiwemo Wareno na Sultan kutoka Oman ambaye ametala zaidi ya miaka 100 hawakupeleka umeme katika kijiji hicho cha Dongoongwe lakini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Chama cha Mapinduzi kimepeleka huduma hiyo na nyenginezo.


Alisema kuwa hatua kubwa za maendeleo hapa Zanzibar zimefanywa kutokana na Sera za ASP na sasa ni CCM chama ambacho kimekuwa kikitekeleza Sera na Ilani yake. Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na shukurani kwa shirika la umeme Zanzibar ZECO, Wizara husika pamoja na wananchi wa kijiji hicho na viongozi wao.


Katika sherehe hizo za uzinduzi Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi wa Dongoongwe kuitumia huduma hiyo ya umeme kama inavyotakiwa kwa lengo la kuwapatia maendeleo pamoja na huduma zao nyenginezo za kijamii.


Dk. Shein katika Sherehe hizo za uzinduzi wa umeme kijijini hapo, alitoa vyeti maalum kwa viongozi wa Kamati za Umeme katika Jimbo hilo la Uzini huku sherehe hizo zikipambwa kwa tenzi na ngoma ya maubwa ambayo ilitoa burudani safi.


Nae Waziri wa Maji, Ujznei, Nishati na Ardhi Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban alisema kuwa  hayo yote ni Matunda ya Mapinduzi kwani bado yanaendelea na kusisitiza kuwa umeme si anasa ni kitu muhimu hivyo ni lazima kitumike hasa katika dunia ya leo ya sayansi na teknolojia.


Mapema Mkurugenzi wa Shirika la umeme Zanzibar ZECO Bwana Hassan.. alisema kuwa Sera ya Serikali ya Mapindyuzi ya Zanzibar ni kuhakikisha kuwa inawasogezea huduma za kijamii wananchi wake popote walipo na kazi hiyo ni endelevu hadi  Serikali ihakikishe wananchi wote wanafikiwa na huduma zote muhimu ikiwemo umeme.


Alisema kuwa gharama zilizotumika katika kupelekea umeme kijijini hapo ni shilingi milioni 100,480,500.00 ambapo kati ya fedha hizo Shirika limechangia jumla ya shilingi milioni 85,480,500.00 na Mbunge wa Jimbo hilo amechangia shuilingi milioni 15,000,000.00.


Alieleza kuwa kazi ziliyofanywa ni pamoja na ujenzi wa njia kubwa ya umeme ya mkondo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 2.7, uwekani wa vitop viwili vya transfoma zenye uwezo wa 100KVA kwa Ghana na 50 KVA kwa Dongongwe, ujenzi wa njia ndogo zenye urefu wa kilomita 2.5 pamoja na malipo ya fidia ya vipato shilingi milioni 18,614,7000.00 huku akiwataka wananchi wa kijiji cha Mkuku kujiandaa kupata huduma hiyo hivi karibuni.


Katika risala yao wananchi wa Dongongwe walisema kuwa wanakamilisha safari ndefu ya kusaka umeme na wanakuwa kijiji cha mwisho katika jimbo la Uzini kupata umeme na kutoa shukurani kwa Serikali, Shirika la Umeme, pamoja na viongozi wao wa Jimbo akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Mohamed Seif Khatib.


Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Gombani

$
0
0

Buldoza la Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba , likichawanya Kifusi katika barabara ya kukimbilia kwa ajili ya kuweka TATAN.

PICHA NA BAKAR MUSSA-PEMBA
Viewing all 34162 articles
Browse latest View live




Latest Images