Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 36208 articles
Browse latest View live

Maalim Seif afutari pamoja na Masheikh nyumbani kwake

$
0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika futari ya pamoja na Masheikh mbali mbali wa Zanzibar nyumbani kwake Mbweni.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na baadhi ya Masheikh na viongozi wa dini ya kiislamum waliofika katika futari ya pamoja

Picha na Salmin Said OMKR

Magazeti Bongo Tz.

Rais wa Zanzibar Dkt Shein, Ajumuika na Wananchi katika Futari Ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Pbz.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya bwawani kuhudhuria hafla ya futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ  Mhe. Abrahaman Mwinyimbegu na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ nDG Juma Amour. 
Rais wa Zanzibar akijumuika na Waumini wa Kiislam katika sala ya magharibi wakati wa kuhudhuria hafla ya futari iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya bwawani Zanzibar.

 




Wananchi naWafanyakazi wa PBZ wakijumuika katika hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani. 

Wananchi naWafanyakazi wa PBZ wakijumuika katika hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani. 



Meneja Rasilimali Watu  PBZ Ndg. Rajab Abdallah,akitowa shukrani baada ya kumalizika hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. 







Ujumbe wa Katuni Leo Zenj.

Article 0

Hilton Worldwide opens DoubleTree by Hilton Zanzibar

$
0
0
Hilton Worldwide opens DoubleTree by Hilton Zanzibar
Hilton Worldwide and DoubleTree by Hilton have announced the opening of DoubleTree by Hilton Zanzibar - Stone Town, located 64 kilometers (40 miles) off the coast of mainland Tanzania. 
Nestled in the heart of the UNESCO World Heritage Site of Stone Town, the 58-room DoubleTree by Hilton Zanzibar - Stone Town offers a perfect base from which to experience the enchanting island of Zanzibar. The hotel marks the brand’s third hotel to open in the country.
“Stone Town is a city of prominent historical and artistic importance, and we are proud to enter as the first global hotel brand in the city,” said John Greenleaf, global head, DoubleTree by Hilton. “Our newest hotel offers a perfect marriage of culture and comfort, underscored by DoubleTree by Hilton’s renowned culture of CARE, which stands for ‘Create A Rewarding Experience’.
CARE centers on the brand’s warm, welcoming guest service culture that begins with the presentation of a freshly-baked chocolate chip cookie upon arrival, and continues throughout the guest’s stay.”

The island of Zanzibar is known as ‘Spice Island’ for its long-standing association with the spice industry. Stone Town, the oldest section of Zanzibar, is made up of ancient stone houses, palaces from the Omani days, carved wooden doors and a treasure trove of bazaars and galleries.
The design of DoubleTree by Hilton Zanzibar - Stone Town reflects the rich architecture and influences of the travelers and settlers who traded with the islanders.
DoubleTree by Hilton Zanzibar - Stone Town features guestrooms and suites decorated with beautiful, traditional hand-carved furniture and featuring 40-inch TVs and ergonomic desks in every room. The hotel’s vibrant oceanfront location marks the perfect setting for everything from leisure getaways to conferences and social events for up to 200 guests.
The exotic Stone City location creates the perfect setting for the hotel’s conference center, offering eight versatile meeting rooms and breakout spaces, a complimentary business center, A/V resources and full catering services. The top floor of the conference center is a tranquil, open space, flooded with natural light and offering magnificent views over the city. Complimentary WiFi is available in guest rooms.
DoubleTree by Hilton Zanzibar – Stone Town also offers cuisine to suit every palate. At Taarab Restaurant and Lounge, the hotel’s rooftop dining venue, guests can savor a menu of contemporary Western fare as well as traditional Zanzibar flavors while taking in views of the sea and the old city.
At Chai Kahawa, a casual café located by the conference center, guests can enjoy international teas and coffees with local snacks.

Matukio ya hapa na Pale kisiwani Pemba

$
0
0
 Harakati za kutafuta mahitaji muhumu katika mji wa Chakechake Pemba kutokana na Wananchi kuwa katika harakati hizo baadhi ya mitaa inayotumika kwa mizunguko ya magari ilibidi kuchukua alama za tahadhari kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama inavyoonekana alama hii ya taadhari katika barabara ya kilimatinde chake.
Mitandao imerahisisha mambo mengi kwa watumiaji wa mitandao hiyo kwa kupata kumbukumbu mbalimbali kupitia simu zao za mikononi kuhifadhi mambo mengi. Kama inavyoonekana wananchi hawa wa kijiji cha Chumbageni Pemba wakipata kumbukumbu za picha kupitia simu zao wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akitembelea shamba la mikarafuu na kuzungumza na wakulima wa zao hilo alipokuwa katika ziara yake kisiwani Pemba.  

Bei za Nguo Zanzibar Juu.

$
0
0
Na Mwandishin Wetu. 
WANANCHI mbali mbali wameeleza kusikitishwa kwao juu ya  suala la upandaji wa bei za bidhaa zikiwemo nguo,kwa ajili ya matayarisho ya sikukuu.
Walisema bei za bidhaa aina hiyo katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku bila ya kufahamu sababu kuu za kuongezeka kwa bei hizo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa wanunuzi wa bidhaa hizo Mwanaisha Mgeni Hassan alisema wafanya biashara wengi wameonekana kuuza nguo,viatu  na bidhaa nyengine zinazohitajika katika kipindi cha sikukuu ambapo jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na serikali kuhusu suala hilo.
Alisema hali hiyo inapelekea kutokuwa na imani na serikali pamoja na wafanyabiashara kwa sababu kuna baadhi ya wananchi hawana uwezo wa kununua kiwango hicho ambacho kimezidishwa.
Alisema kuna baadhi wanakuwa na familia kubwa ya kuwahudumia lakini wanashindwa kwa kuwa kila nguo moja inauzwa shilingi 35,000 na shilingi 50,000.
Nae mfanyabiashara wa nguo za watoto wa Darajani Hassan Mussa Hassan alisema ni kweli kwamba bei za nguo zipo juu na baadhi ya wateja wengine wanashindwa kununua kwa kutoweza kumudu gharama hizo.

Aidha alisema sio kweli kama inavyodaiwa kuwa wafanyabiashara wanazidisha bei za nguo kila ifikapo katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani na kusema kuwa bei inayouzwa mwanzo ndio inayouzwa katika kipindi hicho.
Hata hivyo alisema sababu inayowafanya kuuza bei ya juu ni kutokana ununuzi wa dola inakuwa  kubwa na wakifika nje inakuwa imeshuka ndipo wanapoangalia ile thamani halisi ya bei waliyonunulia.

Pia alisema sababu nyengine ni mamlaka ya TRA upande wa Dar-es-Saalam kuwatoza ushuru kwa mizigo inapofika hapo na inapotolewa kuja Zanzibarpia inalipiwa.

Wenye ulemavu waomba wakalimani

$
0
0
Mwanrafia Kombo na Amina Masoud, MCC
JUMUIYA ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) umeiomba serikali kufanya jitihada za makusudi za kuwasomesha wakalimani kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wao.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Rashid Ali Mohamed,ofisini kwake Kikwajuni, wakati akizungumza na waandishi wa hari hizi.
Alisema kuwepo kwa wakalimani kutawasaidia watu wenye ulemavu kufuatilia matukio mbali mbali yanayotokea katika jamii.
Alisema lengo la kuanziwa jumuiya hiyo ni kuwakusanya pamoja watu wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kuwapatia fursa mbali mbali ikiwemo elimu na mikopo.
Alisema fursa nyengine ni kupatiwa misaada kutoka jumuiya ya wafanyakazi wa kujitolea (VSO) ambapo makao makuu yake yapo nchini Uingereza katika masula ya kilimo cha mboga mboga.

Pamoja na hayo pia wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo mitazamo finyu ya jamii juu ya kundi hilo na kuwapa majina mabaya ambayo hayafai kuitwa binadamu.
Aidha alisema watu wenye ulemavu hawapati haki katika vyombo vya sheria na kusababisha kesi nyingi zinazowahusu kufutwa.
Aliviomba vyombo vya shieria kubadilisha vipengele vya sheria ambazo zinawabana walemavu na kuzingatia haki zao katika sheria ya ushahidi. 

Wanaodaiwa na ZSTC wahimizwa kulipa

$
0
0
Na Masanja Mabula,Pemba
WAKULIMA wa karafuu waliokopeshwa fedha na Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC)  katika wilaya ya Wete huenda wasipate mikopo ya fedha  kwa msimu huu  iwapo watashindwa kurejesha mikopo hiyo waliyokopeshwa msimu uliopita.

Akizungumza na masheha wa wilaya hiyo  ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman, alisema shirika la ZSTC linadai shilingi milioni 23 kutoka kwa wakulima wa karafuu wa wilaya hiyo fedha ambazo walikopeshwa msimu uliopita.

Alisema katika msimu uliopita shirika lilikopesha wakulima wa karafuu katika wilaya hiyo zaidi ya shilingi milioni 138 ambapo fedha ambazo hadi sasa zimerejeshwa ni shilingi milioni 115.12.

Aliwataka Masheha kuzifuatlia fedha hizo kwa wakulima waliokopeshwa na kuwahimiza kurejesha fedha hizo ili kuliwezesha shirikia kuendesha shughuli zake za kuwahudumia wakulima kwa ufanisi zaidi.


Aidha alisema serikali ya wilaya hiyo inakusudia kuwaita wadaiwa ambao wameshindwa kurejesha mikopo ambapo hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza na iwapo wataendelea kukaidi  watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine aliwataka masheha kuwa waadilifu katika kusimimia suala la ujazaji wa fomu kwa wananchi watakao hitaji kukopeshwa na shirikia katika msimu huu wa mavuno.


Nao baadhi ya masheha waliahidi kusimamia uadilifu ili kuona zoezi la ukopaji wa fedha linafanikiwa na wanaokopeshwa ni wale ambao wana uwezo wa kurejesha kwa wakati.

FUPECO walia na uharibifu mazingira

$
0
0
Na Kauthar Abdalla
JUMUIYA ya  Kuhifadhi Mazingira Ras Fumba (FUPECO),imeeleza kusikitishwa na tatizo la uharibifu wa mazingira unaofanywa katika eneo hilo.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa  Jumuiya hiyo, Maria Shoka Hassan ,alisema tatizo la uharibifu wa misitu katika maeneo ya ghuba ya Minai limekuwa kubwa na kupoteza rasilimali ya msitu.

Alisema katika visiwa vya Kwale,Nyemembe na maeneo ya karibu hali imekuwa mbaya kutokana na kuvamiwa na kukatwa miti ya asili.

Alisema waharibifu wakubwa ni watu wa vijiji vinavyozunguka ghuba hiyo pamoja na watu kutoka maeneo mengine.

Alisema licha ya jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwepo misitu na uhifadhi wake , bado kuna ongezeko la  uharibifu wa misitu ya asili.


Aliiomba serikali kupitia Idara ya misitu na mali asili zisizorejesheka kuandaa mikakati imara ya kuwadhibiti wahalifu ili kunusuru mali asili.


Kwa upande wake, Msaidizi Ofisa Misitu Idara ya Misitu na Maliasili Zisizorejesheka, Yussuf Haji Kombo, alisema kutokana na sheria eneo la msitu lolote linashughulikiwa na kijiji husika na inaposhindikana Idara inaweza kuchukua hatua.

Magazetini Leo Tz Bongo.

Maalim Seif awafariji wagonjwa Mkoa wa M/Magharibi

$
0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Magharibi Bi. Raisa Abdallah baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya hiyo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungua mkono wananchi katika eneo la Saateni wakati akiendelea na ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji kijana Hamza Omar Juma, anayesumbuliwa na matatizo ya moyo katika eneo la Mtoni Kidatu.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungua mkono wananchi, wakati akiendelea na ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika mitaa ya Muembe Makumbi kuendelea na ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Salmin Said, OMKR).
 
 Na Hassan Hamad OMKR
 
Wagonjwa wapatao 35 walioko majumbani wamepatiwa huduma na ushauri wa kiafya katika Wilaya sita za Unguja.
 
Hatua hiyo imefikiwa kufuatia ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar mjini na vijijini.
 
Katika ziara hiyo, pamoja na mambo mengine wagonjwa wamekuwa wakipatiwa baadhi ya dawa muhimu kulingana na maradhi yanayowakabili, sambamba na kupatiwa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matatizo yao.
 
Mhe. Maalim Seif amekamilisha ziara yake ya siku tatu ya kutembelea wagonjwa kwa upande wa Unguja iliyoanzia Mkoa wa Kaskazini Unguja na kumalizikia Mkoa wa Mjini Magharibi.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais anatarajiwa kufanya ziara kama hiyo katika Mikoa miwili ya Pemba kuanzia wiki ijayo.
 

Mallim Seif afungua mkutano wa kimataifa wa SOS

$
0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya SOS Zanzibar Mohd Bhaloo, wakati akiwasili Zanzibar Beach Resort kufungua mkutano wa kimataifa wa SOS.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa vijiji vya SOS, Zanzibar Beach Resort.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya SOS Zanzibar, Zanzibar Beach Resort.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tano wa Kimataifa wa vijiji vya SOS unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa Kimataifa wa  SOS unaofanyika hoteli ya Zanzibar Beach Resort. (picha na Salmin Said, OMKR)
 
Na: Hassan Hamad (OMKR).
Kiasi cha watoto milioni 153 wanaishi bila ya uangalizi wa wazazi duniani kote, huku Tanzania ikiwa na watoto wa aina hiyo wapatao kumi na moja elfu, mia mbili na kumi na sita (11,216).
 
Hayo yameelezwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa siku tano kwa nchi wanachama wa vijiji vya SOS, unaofanyika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
 
Pamoja na mambo mengine mkutano huo unajadili namna ya kukuza uelewa katika uendelezaji wa vijiji vya watoto vya SOS, pamoja na kutathmini mafanikio na changamoto zinazovikabili vijiji hivyo.
 
Maalim Seif amesema idadi ya watoto wanaokosa uangalizi wa wazazi imekuwa ikiongezeka kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo kufariki kwa wazazi, hali ya umaskini, unyanyasaji  pamoja na talaka.
Amefahamisha kuwa matokeo ya hali hiyo ni kuongezeka kwa ajira za watoto ambapo  Zanzibar pekee inakisiwa kuwa na asilimia tisa nukta mbili (9.2) ya watoto kati ya umri wa miaka mitano hadi 17 wanaojihusisha na ajira hizo.
 
Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo, juhudi za pamoja zinahitajika kati ya taasisi za umma na binafsi, kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa, sambamba na kuzisaidia familia zenye watoto yatima na zinazoishi katika mazingira magumu.
 
Amesema Serikali kwa upande wake inaridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na SOS Zanzibar na Tanzania, na kuzitaka taasisi hizo kuzidisha bidii katika kuleta ufanisi.
 
Ameelezea matumaini yake kuwa kampeni ya CARE FOR ME  iliyozinduliwa na vijiji vya SOS mwaka 2012, italeta faraja na mafanikio kwa kuwapatia watoto huduma bora zikiwemo za kielimu.
 
Ameyashukuru mashirika ya misaada ya Norway (NORAD), Austria (ADA) na Denmark kwa kuunga mkono miradi ya SOS, hatua ambayo amesema inaisaidia Serikali kukabiliana na matatizo yanayowakabili watoto.
 
Mapema akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa bodi ya vijiji vya SOS Zanzibar Bw. Mohd Bhaloo, amesema SOS Zanzibar imekuwa imewahudumia watoto wapatao mia nane (800) kwa kuwapatia elimu bora, kupitia  skuli ya msingi na sekondari ya Hermann Gmeiner iliyo chini ya kijiji hicho.
 
Amefahamisha kuwa SOS Zanzibar pia ina kituo cha afya ambacho hutoa huduma kwa watoto wa kijiji hicho pamoja na wananchi wa maeneo ya karibu ambapo zaidi ya wagonjwa elfu moja na mia nne (1,400) hupatiwa matibabu katika kituo hicho kwa mwaka.
Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine SOS Zanzibar kupitia mpango wake wa kuwajengea uwezo watoto, inazisaidia familia 180 zenye watoto elfu moja Unguja na Pemba, ili ziweze kuimarisha huduma kwa watoto hao.
Akizungumzia kuhusu historia ya vijiji vya SOS Zanzibar, Bhaloo amesema azma ya kuanzishwa kwa vijiji hivyo iliasisiwa mwaka 1984 na kuanza kuwahudumia watoto kuanzia mwaka 1991.
Ameishukuru Serikali na taasisi binafsi kwa ushirikiano wao katika kuunga mkono juhudi za vijiji vya SOS, na kwamba mafanikio makubwa yamepatikana tokea kuanzishwa kwa vijiji hivyo hapa nchini.
Mkutano huo wa siku tano unazishirikisha nchi mbali mbali zenye vijiji vya SOS zikiwemo Austria, Cameroon, Ethiopia, Malawi, Mozambique na Morocco. Nchi nyengine ni Uganda, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Tanzania na wenyeji Zanzibar.
 

First Vice President Speech at SOS Workshop

$
0
0
THE SPEECH BY H.E. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, THE FIRST VICE PRESIDENT OF ZANZIBAR, AT THE OPENING OF SOS WORKSHOP AT ZANZIBAR BEACH RESORT, MONDAY 13TH JULY, 2014.
 
Honourable Representatives of Revolutionary Government of Zanzibar,
Honourable Chairperson, Board of Trustees SOS Children’s Village Zanzibar.
Members of the Board of Trustees SOS Children Zanzibar
Honourable Director, SOS children’s Villages Tanzania/Zanzibar,
Honourable Representatives of NORAD and ADA
Representatives of SOS Children’s Villages International and regional offices,
Dear Delegates from SOS Children’ Villages:-Austria, Cameroon, Ethiopia, Malawi,Mozambique, Morocco,Uganda,South Africa,Zambia, Zimbabwe, Tanzania and Zanzibar.
 
 
 
Representative of Civil Society Organizations.
Distinguished Participants, Ladies and Gentlemen, good morning!
Assalaamu Alaykum.
First and foremost I would like to take this opportunity to thank the Almighty God for availing us good health and protecting those who travelled from different countries to attend this workshop.  My deep appreciation goes to the organizers for giving me this privilege to officiate at the opening of this workshop of its kind which bring together representatives of SOS Children’s Villages Member Associations from different countries.
May I take this opportunity to welcome you to Zanzibar. For all of you who have travelled from afar I ask you to feel at home among brothers and sisters. It is my hope that you will take advantage of your stay to visit some attractive parts of Zanzibar, which is known for its great historical sites that combine with natural splendour and beauty of its beaches to make it a world wonder. KARIBUNI SANA (YOU ARE MOSTLY WELCOME TO ZANZIBAR).
I am told that the purpose of this five- day workshop is to provide a forum for SOS Member Associations funded by ADA and NORAD to share experience of advocacy work to date, develop knowledge and skills in SOS’s approach to advocacy, and make plans for developing advocacy work and capacity. You are meeting to present and discuss successes and challenges experienced by Member Associations in the following areas;
(1)Planning and implementing advocacy work, (2) In mainstreaming advocacy in programmes, (3) Work together to develop knowledge and skills for planning and implementing advocacy, (4) Communications strategies, (5) Mobilising resources for advocacy projects, and (6). Monitoring and evaluating advocacy work.
Distinguished Participants,
Before I say few words on the Workshop,I would like to extend my gratitude to Norwegian Agency for Development Cooperation (NORAD, Austria Development Aid (ADA), SOS-Norway and SOS-Denmark for the great work they are doing to raise funds to support Programmes/Projects implemented by SOS Children’s Villages  in Tanzania and Zanzibar. Through such support SOS Children’s Villages Tanzania and Zanzibar are able to implement programmes which are impacting in a positive way on the children who are orphans and those living in most vulnerable families. Such programmes include;
(1)Family Based Care, which takes care of children who are orphans and those abandoned by their parents, (2) Family Strengthening programme which empower the poor and destitute families, and communities to respond to the needs of children who are at the risk of losing parental care, (3) Advocacy projects which are contributing to raise awareness about the rights of children in alternative care, and (4) Promoting children protection.
Both governments, i.e The Government of the United Republic of Tanzania and The Revolutionary Government of Zanzibar, recognize and appreciate value added through such interventions, which indeed are a great assistance to both governments.
Our Governments are proud of the good work done by SOS Children’s Villages Tanzania and Zanzibar. SOS Children’s Village in Zanzibar is known for its great work which include among other things, (1) Supporting individual care givers and their families to build their capacity so as to provide quality care to children, and (2) supporting communities and local authorities by strengthening systems and structures to better respond in sustainable manner to the needs of children, especially those at risk of losing parental care.
Distinguished Participants,
The protection of children and the promotion of their well-being are closely linked to the development and well-being of their societies. On the basis of the vital importance of human rights, equitable development and the centrality of human security, it is important for all stakeholders to join hands to promote the agenda of child protection, in order to ensure that all children live a life free from all forms of violence, are protected in conflicts and disasters and thrive in a safe family environment. Being key partners of the Government, I should request you to focus your investment in supporting the government in the following fields;
(1) To build and strengthen local and national child protection systems, (2) To address the scourge of child abuse, neglect and exploitation which remain major problems threatening the well-being of children.
Child protection needs are immense and diverse in any country. In Tanzania, they are further augmented by widespread poverty and the impact of HIV and AIDS. A total of 282 children’s homes exist and are spread all over the 21 regions of mainland Tanzania. There are 11,216 children in the 282 children’s homes out of whom 6,089 are boys and 5,127 are girls.
69.6 percent of the children are aged between six and seventeen years. 21.6 percent of the children are under five. 9.8 percent are eighteen and above. 79 percent of the children homes are owned by CBOs, NGOs and FBOs.13 percent are owned by individuals, 4 percent by affiliated homes, 0.4 percent by government and 4 percent by families. The main factors causing children to end up in the homes include; increase of orphans, provision of shelter for street children, and sympathy of the children home’s owners.
Distinguished Participants,
Other reasons are family poverty, child harassment, verbal and physical abuse, thrashing, parental drunkenness, family conflicts, social irresponsibility, divorces and early pregnancy.
In both Zanzibar and the mainland the true extent of child abuse and violence does exist and increasingly it is catching headlines in the media   suggesting that violence against children, sexual exploitation and abuse is a significant problem occurring at the level of home, communities and in schools. Other problems affecting children, which call for partner’s support, include children without appropriate care, which include children living and working in the streets, orphans and the neglected and child labour.  In Zanzibar, it is estimated that 9.2 per cent of the children aged between 5-17 years are likely to be  involved in child labour.
This situation demands combined efforts of the government, civil society organizations and private sector to promote a culture where children, especially orphans and most vulnerable are taken care of in loving and caring family environment.
Distinguished Participants,
I would like to take this opportunity to commend the contribution and significant role played by SOS Children's Villages International in helping children who are orphaned, abandoned or the neglected. SOS Children’s Villages work enable such children to grow within an alternative family setting environment. I am pleased that all countries represented in this workshop carry flags of good and noble work undertaken by SOS Children’s Villages.
Besides, SOS Children’s Villages   launched CARE FOR ME! In December 2012 as a research and advocacy campaign to help realise every child’s right to quality alternative care. Statistics show that about 153 million children Worldwide are living without parental care.
For many of these children they receive care is inadequate or even dangerous. SOS Children’s Villages through CARE FOR ME! Campaign seek to foster research and advocacy at national and international levels to ensure that fundamental rights of children in alternative care are observed and respected by all stakeholders involved.
I believe through CARE FOR ME campaign, SOS Children’s Villages, in collaboration with partners and stakeholders will be able to reach more children with quality care.
Distinguished Participants, Ladies and Gentlemen,
I would like to conclude my remarks by stressing on the importance of institutional engagement towards better quality, better environment and better services for children. CARE FOR ME  Campaign which represents efforts of SOS Children Villages International to promote the UN Guidelines for the Alternative Care of Children, to improve child care systems and ensure a child’s right to quality care are observed by all stakeholders is a great initiative which is part and parcel of CARE FOR ME Campaign.
 
 
I therefore urge you to use this unique opportunity presented over the next five days to reflect and learn from each other and plan together about ways to reach more children with quality care through advocacy.
I wish you fruitful deliberations and sharing experiences over the next five days. Also do find some time to enjoy our beautiful Island and experience the Zanzibar hospitality.
It is now my pleasure to declare this workshop officially open.
Thank you for your attention.

Maalim Seif afutarisha watendaji wake

$
0
0


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akifutarisha watendaji wa Ofisi yake nyumbani kwake Mbweni Zanzibar. Miongoni mwao ni Watu Wenye Ulemavu wa aina mbali mbali. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Rais Kikwete afutarisha wananchi wa Mbeya

$
0
0
 Mbunge wa Mbeya Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu" akipata futari na wananchi wenzie wa Mbeya katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.
 Meza Kuu katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.
 Wananchi wa Mbeya waliohudhuria futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini MbeyaJumapili Julai 13, 2014.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishurkuru wananchi wa Mbeya kwa kujitokeza kwa wingi katika futari aliyoiandaa katika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.

  Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika futari aliyoandaa  katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.
 Rais Jakaya Kikwete akiungana na wananchi wa Mbeya katika swala ya Magharibi katika  futari aliyoandaa  katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.
Waziri wa Nchi Katika Ofisi ys Rais (Kazi Maalumu) Profesa Mark Mwandosya, na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu" wakiungana na wananchi katika futari iliyoandaliwa na Rais Jakaya mrisho Kikwete katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya Jumapili Julai 13, 2014.
  .
 
PICHA NA IKULU

Nungwi wahamazishwa kulinda mazingira

$
0
0
Na Kauthar Abdalla
VIONGOZI na watendaji wa serikali wametakiwa kuongeza nguvu katika kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya safisha Zanzibarili kuhakikisha inafikia lengo.

Wakizungumza katika kampeni hiyo wakaazi wa kijiji cha Nungwi, walisema kufanya hivyo kutaongeza ari ya utendaji kwa washirika wa maendeleo ambao wameanzisha mpango huo ili kukuza utalii wa kimazingira.

Mmoja ya wanakijiji hao, Kazija Silima, alisema endapo hali ya mazingira itakuwa ya kuridhisha idadi ya watalii wanaotembela kijiji hicho itaongezeka.

Alisema mpango huo unaoendeshwa na jumuiya ya ZANREC umeanzishwa baada ya Zanzibarkutangazwa kuwa katika kiwango kisichoridhisha cha usafi ambapo imesababisha kupokea watalii wa daraja la chini hali inayotishia kuathiri uchumi wa Zanzibar kwa kuwa sekta ya utalii ndio inayotegemewa.


Alisema kijiji cha Nungwi kimekuwa kikipokea wageni wengi lakini wanakijiji wanapata  hofu ya kupungua kiwango wageni hao kutokana mazingira yake kutokuwa safi.


Nae Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya la  Labayka Development Fund, Haji Khamis Haji, alisema katika kudumisha dhana ya mtu na mazingira ni vyema kuzingatia madhara ya uchafu ambayo athari yake ni kubwa.

Zaidi ya Shilingi Milioni 300 Zatumika kuangamiza Kunguru

$
0
0
Na Laylat Khalfan
ZAIDI ya shilingi milioni 300 zimetumika kwa ajili ya mradi wa kuangamiza kunguru weusi kuanzia 2012-2013.
Hayo yalielezwa na Msaidizi Mratibu wa huo, Salim Ali Khamis, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Maruhubi.

Alisema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za  wafadhili kutoka serikali ya Finland.

Alisema lengo la mradi huo ni kupunguza idadi ya kunguru weusi ambao wanasababisha kero na adha kwa wananchi na maisha ya ndege wengine muhimu.

Alisema kwa kiasi kikubwa mradi huo umefanikiwa  ambapo kiasi cha kunguru 168,000 wameangamizwa kwa Unguja na Pemba32,000.


Hata hivyo, alisema mradi huo unakabiliwa na  changamoto mbalimbali ikiwemo kuibiwa kunguru hao wanapoingia katika mtego.

Aidha alisema kuna baadhi ya watalii huwa wanawanasua kunguru waliongia kwenye mitego kwa madai kwamba wanateswa.


Baadhi ya wananchi wa maeneo ya mjini waliupongeza mradi huo wakisema umesaidia kupunguza idadi ya kunguru ambao walikuwa kero kwa mifugo yaoikiwemo kuku.

Kwamtipura wahimizwa kushirikiana

$
0
0
Na Mwanajuma Mmanga
MWENYEKITI wa CCM jimbo la Kwamtipura, Kombo Said Ally,  amasema maendeleo ya jimbo hilo yatafikiwa endapo kutakuwa na mashirikiano baina ya viongozi wao.
Alisema  yeye yuko tayari kushirikiana na wananchi katika kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma  maendeleo ya jimbo hilo.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wazee wa jimbo hiloMkele wilaya ya mjini Unguja.

Alisema endapo watashirikiana na kuunganisha nuvu zao watafikia malengo waliyojiwekea na kukipatia chama ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.

Aliwasisitiza wazee hao kuzidisha mashirikiano na kusimamia maendeo ndani ya jimbo lao bila kujali itikadi za kisiasa.


Nae Sheha wa shehia ya Mkele, Khamis Khamis Mkadamu, alisema maendeleo ya jimbo hilo yatafikiwa endapo kutakuwa na mashirikiano mazuri baina ya viongozi  na wananchi.
Viewing all 36208 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>