Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all 34163 articles
Browse latest View live

Rais Dk.Shein atembelea Benki ya Damu Salama

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifutana na Meneja wa  Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed (kulia) katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia Damu Salama zilizohifadhiwa katika mashine maalum akiwa na Aaza Humud katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifutana na Meneja wa  Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed (kulia) katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo. 

Mkuu wa maabara ya kuchunguza maradhi mbali mbali Msafiri L.Marijani  akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea Maabara katika Hospitali ya Mnazi mmoja leo Mjini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Damu Salama kiliopo Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo alipofanya ziara fupi
Afisa Mhamasishaji wa Kituo cha Damu Salama Omar Said Omar (kulia) akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na wafanyakazi  wa kituo hicho alipofanya ziara maalum ya kutembelea kuangalia maendeleo ya utendaji kazi Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo(Picha na Ramadhan Othman Ikulu)

Magazetini Tz Bongo Leo.

TUTASHIRIKIANA NA WAPENDA AMANI KUISAIDIADRC IWE NA AMANI-TANZANIA

$
0
0
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza wakati wa Mkutano wa  Kamati  ya Nne ya Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa iliyokuwa  ikijadili ajenda    kuhusu  tathmini ya jumla ya  Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi zinazochangia wanajeshi wake  katika    operesheni  hizo za ulinzi wa amani.
Sehumu   ya wajumbe wa Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa,  wakifuatilia majadiliano   ya ajenda   kuhusu Operesheni za  Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.



Na MwandishiMaalum, New York

Jamhuri ya Muunganowa Tanzania,imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa yakuwa itaendelea kushirikiana na wapenda amani katika kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa na amani na usalama.

Akichangia majadiliano juu ya ajenda inayohusu tathimini ya jumla ya Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa. Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania inafanya hivyo kwa kutambua wajibu wake katika medani ujenzi wa amani ya Kimataifa.


Amesema  pia  kuwa, ni kwa kutambua wajibu huo, ndiyo sababu iliyoifanya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia makubaliano na nchi wanachama wenzie katika SADC na Maziwa Mkuu (ICGLR),kujitolea kupeleka wanajeshi wake huko  DRC ili kuunga mkono juhudi za kuwasaidia wananchi wa DRC kuwa na amani , usalama na maisha yenye uhakika.



Balozi Mwinyi amesema kuwa Tanzania inajivunia kuwa wanajeshi wake  wanaohudumia kupitia FIB  ambayo ni sehemu ya MONUSCO licha ya mazingira magumu na hatari wanayokabiliana nayo wameonyesha umahiri mkubwa ikiwa ni pamoja na kujitoa muhanga maisha ya o kuwalinda raia wasiokuwa na hatia DRC  pamoja na kurejesha amani na usalama.


Kwa sababu hiyo, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, amesema ni vema na haki, kujitoa muhanga huko kwa wanajeshi wanaohudumia FIB kutambuliwa na wapenda amani wote na  vile vile FIB iendelea kupata uungwaji mkono stahili.


Aidha Balozi Mwinyi amesema, kutokana mabadiliko ya mwenendo mzima wa machafuko na vita  katika maeneo mbalimbali Barani Afrika, ikiwa ni pamoja na matishio na kutumik a kwa mbinu za kigaidi na mabomu ya kutengenezwa kienyeji kuna lazimisha kufanyika mabadiliko katika mfumo mzima wa ulinzi wa Amani.


Amesema, mabadiliko hayo yanapelekea Umoja wa Mataifa kulazimika kuidhinisha matumizi ya mamlaka nguvu katika baadhi ya misheni zake kutokana na ukweli kwamba matishio hayo siyo tunihatarisha kwa raia lakini pia   yamekuwa tishio kwa walinzi wa amani.


Kwa sababu hiyo, Tanzania imetaka kuwapoja kwa majadiliano ya kina ndani ya Umoja wa Mataifa kuhusu dhana nzima ya mabadiliko ya mwenendo wa machafukona  vita vinavyoendelea na hatarii nayo wakabili walinzi wa amani pamoja na matumizi ya nguvu kuwa sehemu ya mamlaka nguvu ya misheni nyingi.


“Tunahitaji majadiliano ya kina katika eneo hili,kwa sababu, mwenendo wa machafuko na mbinu za maadui zimebadilika kabisa.Kuna matumizi makubwa ya mbinu za kigaidi na mabomu yanayotengenezwa kienyeji, haya yote na mengine mengi yanabadilisha kabisa historia ya asili ya ulinzi wa amani, amesisiti za Balozi Mwinyi.

Vile vile amesema, majadiliano ya kina yanahitajika katika eneo la matumizi ya teknolojia za kisasa katika operesheni za kulinda amani,zikiwamo ndege za kiuchunguzi zisizoendeshwa na binadamu ( UAS).


Amesemahapanashaka,kama walivyozungu mza wajumbe wengine, matumizi ya teknolojia hizo pamoja na umuhimu wake yanahitaji majadiliano ya kina na makubaliano ya pamoja.


Aidha Balozi Mwinyi amesema,Tanzania inakaribisha nia ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kufanya mapitio ya Operesheni za Ulinzi wa Amani zaUmoja wa Mataifa ( UNPKOs)  na Misheni Maalumu za Kisiasa (SPMs). 

Na ameahidi kuwa Tanzania itashiriki kikamilifu katika mchakato huo.


Awali akizugumza mwanzoni mwa majadiliano hayo Mkuu wa Idara ya Operesheni ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO)Bw.Herve Ladsous, amezungumzia mafanikio na changamoto mbalimbali zinazokabili shughuli za ulinzi wa amani.


Amesema katika DRC,Misheni ya Kulinda Amani ( MONUSCO) ambayo ndani yake kuna FIB imeonyesha umahiri na ujasiri mkubwa wa kutokubali kurudi nyuma katika mapambano ya ke dhidi ya makundi ya waasi yenye silaha.


Akasema ushupavu na uhodari huo,licha ya kutoa ulinzi kwa raia pia umefungua fursa mpya ambapo mamlaka za kiutawala za DRC zimeweza kutawala maeneo ambayo huko nyuma yalikuwa yakishikiliwa na kukaliwa na makundi ya waasi.


Katika majadiliano hayo wazumgumzaji wengi wameelezea kusikitishwa kwao na ongezeko la vitendo vya kuvamiwa kwa walinzi wa amani na kusababisha wengi wao kupoteza maisha.


Wakasema, jambo hilo halikubaliki na halipashwi kuendelea kufumbiwa  macho na kwamba ni lazima pafanyike utafiti wa kina wa kwa nini kumekuwa na ongezeko la mashambulizi kwa walinzi wa amani. na wametaka wahusika wa huduma hizo watafutwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.


Wachangiaji wengine wameshauri na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kupitia DPKO na taasisi nyingine zinazohusika na masuala ya operesheni za ulinzi wa amani, kuangalia upya mazingira ya utendaji kazi ya walinzi hao wa amani, ikiwa ni pamoja na kuwa patia mafunzo zaidi yanayoendana na wakati, vifaa na zana za kisasa na vya uhakika, malipostahili na pia mamlaka zinazotekelezeka.


Balozi Seif Akabidhi Seti ya Komputa.

$
0
0
Balozi Seif akiwasisitiza wanafunzi wa Unique Learning School kujitahidi katika masomo yao ili kujijengea hatma njema ya maisha yao ya baadaye kielimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiof Ali Iddi akikabidhi Seti ya Kompyuta na Printa yake kwa Uongozi wa Unique Learning School iliyopo Upenja Wilaya ya Kaskazini “ B”.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi na Wanafunzi wa Unique Learning School mara baada ya kuwakabidhi Kompyuta kutekeleza ahadi aliyoupa uongozi wa skuli hiyo.(Picha na Hassan Issa OMPR)

Pinda azungumza na waTanzania wanaoishi Oman

$
0
0

Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh.
Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. 
Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014.
Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

Msimamo wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar

$
0
0
                MSIMAMO GRAND MALT PREMIER LEAGUE

ZANZIBAR 2014/2015

POS

TIMU

P

W

D

L

GF

GA

GD

PTS

Y/C

R/C

1

ZIMAMOTO

7

5

1

1

13

7

6

16

7

2

2

MAFUNZO

7

4

1

2

9

5

4

13

8


 3

JKU

7

2

4

1

6

3

3

10

4


4

KIPANGA

7

2

4

1

7

5

2

10

14


5

HARDROCK

7

3

1

3

7

10

-3

10

8


6

CHUONI

7

2

4

2

8

8

-

10

11

1

7

POLISI

7

   1

5

1

6

5

1

8

6


8

KMKM

7

2

3

3

6

8

-2

9

9

2

9

MTENDE

7

1

4

2

6

7

-1

7

10


10

MIEMBENI

7

1

4

2

9

12

-3

7

14

1

11

MALINDI

7

2

1

4

9

13

-4

7

16

1

12

SHABA

7

-

4

3

8

11

-3

4

7



114

7

Jumla ya mabao 94 yameshafungwa kupitia michezo 42


Wafungaji:

Ali Juma Hassan              -5 Mafunzo                           Iddi Kambi                - 2 KMKM

Nyange Othman               -3 Zimamoto                         Amour Bakar            -1 Chuoni

Ibrahim Hamad Hilika     -3  Zimamoto                        Ali  Rajab                  -1 Mtende

Mkadam Ali                     -2 Miembeni                         Ibrahim  Khamis       -1 KMKM

Suleiman A. Nuhu           -2 Shaba                                Hassan Seif               -2 Miembeni

Juma Moh’d Philipo        -2 Chuoni                              Yussuf  Seif              -1 Malindi

Khatib Said                      -2  Zimamoto                        Imran Abdul Rai       -1 Kipanga

Devid Julius                    -2 JKU                                                                                                        Juma Ali Ramadhan      -1  Zimamoto                           

Yahya Said Tumbo         -2 Mtende                              Aboubakar Ayoub     -1 Kipanga

Hakim Khamis                -2 Zimamoto                         Mussa Suleiman         -1 Kipanga 

Jackson Dickson             -2 Shaba                                Mudrik Muhibu          -1  KMKM 

BurhanRashid             -3Hardrock                       OthmanOmarTamim   -1Miembeni                                                  
Sadik Habibu                 -2 Mafunzo  
 Fasihi Hija                     -2 Malindi                             
Jumanne Seif               -2 Mtende                      
Maulid Ibrahim            -1  KMKM                           
 Omar Juma Haji          -1 Hardrock                    
Haji Wahaji                  -1  Malindi                            
 Mbarouk  Chande       -1 JKU                              
Mussa Haji                   -1 Hardrock                                                                                                     
 Is-haka Othman       -1 JKU                                   
 EmmanuelMartin  -1 Hardrock                                                                                                                                                                            
    Mwita Mohammed      -1 Polisi    
    Mwinyi Haji                -1 KMKM                     
    Haule Innocent            -1 Polisi                                
    Suleiman Ali Haji        -1 Miembeni                  
     Ibrahim   Rajab            -3 Chuoni                           
    Saleh Hamad                 -1 Chuoni                          
     Mohammed Nyasa      -1 Shaba                               
    Khamis Abrahman        -1 Polisi                            
    Adam Abdalla             -1 Kipanga                          
  George Thomas            -1 Chuoni                          

 Abdulhamid Ali         -1 Zimamoto                          
Yunus Bernard              -3 Kipanga                        
Makame Hamad        -1 Zimamoto                    Amour Omar Janja        -1 JKU                                       

Rashid  Abdalla             -1 Mafunzo                       Mansour Marzouk        -1 Miembeni

Salum Masoud              -1 Malindi                         Juma Mwalim Juma    -1 Shaba                                

Amour  Sleiman            -2  Malindi                        Moh’d Salim               -1 Shaba 

Bakar Manyeto              -1 Shaba                           Salum Seif                 -1 Miembeni                                   


KADI ZA ADHABU



JINA LA KLABU/TIMU

KADI YA NJANO

KADI  NYEKUNDU





KIPANGA

ABOUBAKAR  AYOUB  - 2

HASSAN  SALEH

MUNIR  IDDI             -2

SELEMANI HAMAD

MASOUD ABDALLA

MASOUD MOH’D

ADAM  ABDALLA

HAJI  IDRISSA

ABDALLA RAMADHAN

AMOUR SLEIMAN

MUSSA  SULEIMAN

IMRAN ABDUL





CHUONI

JUMA MOH’D JUMA

MOH’D JUMA

MOH’D ABASS    - 2

OMAR MUSSA

MUSSA  JUMA

AMOUR  BAKAR

ABRAHMAN SAID

HAFIDH MOH’D

NASSOR ABDALLA

ADAM  HAMAD


AHMED MOHAMMED

ZIMAMOTO

IBRAHIM  HAMAD   - 2

HAKIM KHAMIS

HASSAN JUMA AME

HASSAN SAID             - 2

RAMADHAN  ABDALLA

ALI SALUM BAKAR  - 2



MIEMBENI

MAJID  SLEIMAN  - 3

AZIZI SHAWEJI     - 2

IBRAHIM ABASS

RAJAB KHAMIS    - 2

MKADAM ALI

OTHMAN OMAR    - 2

ISSA OTHMAN

ABDULKADIR MWINYI

SULEIMAN ALI

SULEIMAN ALI HAJI

HARDROCK

GEORGE JOHN

MOH’D ALI RASHID

EMMANUEL  G. MALALE

SALUM ABD. JUMA

SALEH JUMA SHIJA   -2

EMMANUEL MARTIN

BARAKA  KHAMIS


POLISI

MOH’D OTHMAN  - 3

HAULE INNOCENT

SULEIMAN MOH’D

KHAMIS ABRAHMAN








MALINDI

HAJI  WAHAJI

YUSSUF  SALEH

SAID  MUHAMADI

ALI  THABIT

ABDULSAMAD  OTHMAN

SAID  KHALID

FASIHI  HIJA   - 2

SALUM  MASOUD

NDAKA  MAIKO       - 3

DAUD  SLEIMAN

SAID  OMAR

ABDALLA  SAID

AMOUR SLEIMAN




KMKM

MWINYI  HAJI    -2

KASSIM ABDULHALIM

MUDRICK MUHIBU

FAKI HAMAD ALI

MUDATHIR  KHAMIS

IDDI MGENI

KASSIM ABDULKADIR

IBRAHIM KHAMIS

KHAMIS ALI KHAMIS


MAULID IBRAHIM

SHABA

MOHAMMED  SALUM

HASSAN SHAABAN

SHEHA KHAMIS

JUMA MWALIM

MOH’D SALUM

MOH’D NYASA

BAKAR HASSAN



JKU

ISMAIL  KHAMIS

KHAMIS ABDALLA ALI

HILALI  REHANI




MTENDE

SLEIMAN  SAID    - 3

SELEMANI  JUMA

ALI   RAJAB

YAHYA  SAID TUMBO

MUSSA SAID  -2

AMOUR HAJI HASSAN

ALI MOH’D




MAFUNZO

SADIK  HABIBU

ALI OTHMAN MMANGA

KHEIR SALUM

SAID YUSSUF

HAJI RAMADHAN

SAID MUSSA

KHALID RAMADHAN

MOH’D ABDULRAHMAN


Ligi Kuu ya Zanzibar KMKM na Chuoni. Amaan

$
0
0
Beki wa timu ya KMKM Mwinyi Haji akiokoa mpira golini kwake huku mchezaji wa timu ya Chuoni akijiandaa kumnyanganya mpira.
           Mchezaji wa timu ya CHuoni Juma Mohammed, akimpita beki wa timu ya KMKM.

Golikipa wa timu ya KMKM Salum Amour akidaka mpiora huku mshambuliaji wa timu ya Chuoni Amour Bakari akiwa  jirani akisubiri mpira huo wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya grand malt. 

Benchi la Ufundi la timu ya Chuoni wakiwa na majonzi baada timu yao kulkazimishwa sare na timu ya KMKM katika mchezo wa ligi kuu ya grand malt mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.

Mchezaji wa timu ya Chuoni Hamad Mshamata akiwapita mabeki wa timu ya KMKM katika mchezo wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Chuoni Amour Bakari akiruka kiunzi cha bneki wa timu ya KMKM Mwinyi Haji, wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan. 
Mchezajhi wa timu ya Chuoni Goerg Thomas, akimpita beki wa timu ya KMKM Khamis Ali,wakati wa mchezo wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan, timu hizo zimetoka sare ya      1--1. 
Golikipa wa timu ya KMKM Salum Amour, akidaka mpira huku mchezaji wa Chuoni Amour Bakar, akijaribu kupiga kichwa mpira huo, huku beki wa timu ya KMKM Iddi Mgeni,akiwa tayari kutoa msaada kwa kipa wake.
Mchezaji wa timu ya KMKM Iddi Mgeni,akizuiya mpira huku mchezaji wa timu ya Chuoni Amour Bakar, akirusha daluga katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan.timu hizo zimetoka sare,
Kocha Mkuu wa timu ya KMKM Shaban Ramashan kushoto na Kocha wa timu ya Chuoni Ali Bakar wakipongezana baada ya mchezo wao wa ligi kuu ya grand malt kumalizika kwa sare ya bao 1--1 mchezo uliofanyika uwanja wa amaan.

Katuni na Ujumbe wake Huooooo................


Mjue Bui Kinanda

$
0
0
Mjuwe Bui kinanda ni mmoja wa mabui wengi katika Zanzibar, akiwa katika mawindo yake akijitafutia mlo kwa kubaka wadudu warukao karibu yake ndio huwa mlo wake bui kinanda. 




Magazetini Tz Bongo leo

Kutoka Baraza la Wawakilishi leo

$
0
0
        Wajumbe wakiupitia mswadwa wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa baraza la wawakilishi
Mjumbe wa Jimbo la Wawi Pemba Mhe Saleh Nassor Juma akichangia wakati wa mkutano wa baraza la wawakilishi kuchsangia miswada iliowakilishwa katika kikao hicho.
Wajumbe wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza wakati wa kuchangia miswada hiyo leo asubuhi.
             Mwakilishi wa jimbo la kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akichangia
MWAKILISHI wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar Mhe Mbarouk Wadi Mussa  Mtando, akisisitiza jambo na Wawakilishi wa katikati Mwakilishi wa (Tumbe) Mhe. Rufai Said Rufai na Mhe Salim Abdallah Hamad (Mtambwe)wakiwa nje ya ukumbi wa  mkutano baada ya kuchangia mswaada uliowakilishwa katika kikao hicho 

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, akibadilishana mawazo na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Abubakar Khamis Bakary, wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi kwa mapumziko mafupi. 
Mwakilishi wa jimbo la Mpendae Mhe Mohammed Said Dimwa akisisitiza jambio na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi kwa mapumziko mafupi.
Mwakilishi wa Jimbo la Muembemakumbi Mhe, Machano Othman, akizungumza na na kubadilishana mawazo na Mwakilishi wa Bububu Mhe HGusein Makungu Bhaa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa Mhe. Joseph Meza wakimsikiliza Mhe Machona wakiwa nje ya ukumbi wa Baraza baada ya kupitisha Mswaada wa Wizara hiyo. 

Katuni wa leo na Ujumbe wake huoooooooooo

Hotuba ya Ufungaji Mkutano wa Baraza la Wawakilishi

$
0
0

  
HOTUBA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI KATIKA UFUNGAJI WA MKUTANO WA KUMI NA SABA WA BARAZA LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR.
TAREHE 31 OKTOBA, 2014


UTANGULIZI:

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutukutanisha hapa tukiwa katika hali ya uzima na afya njema na kufanikiwa vizuri kushiriki katika Mkutano huu wa Kumi na Saba wa Baraza la Wawakilishi. 


Aidha, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Said Hassan Said kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.  Kuteuliwa kwa Mhe. Said kunaonyesha imani kubwa ambayo Mheshimiwa Rais anayo juu yake, hasa kutokana na uzoefu wake na uwezo wake mkubwa wa kuchapa kazi.  Tunamtakia kila la kheri na mafanikio mema katika kazi yake hiyo mpya.  Tunakuhakikishia ushirikiano wetu kila wakati.


Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa, niruhusu nitoe shukurani zangu za dhati kwako wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti na wasaidizi wako wote kwa kuendelea kuliendesha Baraza hili Tukufu kwa busara na umakini mkubwa. Pia nawashukuru Waheshimiwa Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati mbali mbali wa Baraza hili kwa busara zao katika kutekeleza majukumu yao.


Mheshimiwa Spika, pongezi maalum nazitoa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuendelea kuiongoza nchi yetu kwa hekima, busara na uadilifu mkubwa. Aidha, nachukua fursa hii kumpongeza Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuendelea kumsaidia vyema Mheshimiwa Rais katika utekelezaji wa majukumu yake.


Mheshimiwa Spika, nawapongeza Waheshimiwa Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi, Mawaziri, Naibu Mawaziri kwa umahiri wao mkubwa katika kuchangia mijadala mbali mbali ndani ya Baraza hili. Aidha, nawashukuru Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Watendaji wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi.


Mheshimiwa Spika, pia navipongeza vyombo vyahabari vya hapa Zanzibar, hususan Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC)  kwa kuwapasha habari  mbali mbali wananchi wetu kwa kupitia redio, TV na magazeti. Hali ambayo ilipelekea urahisi kwa wananchi kufuatilia kwa makini matukio yote yaliyojiri Barazani. Vile vile, nawapongeza wakalimani wetu wa lugha ya alama kwa kazi nzuri walioifanya ya kutafsiri mawasilisho na mijadala katika kipindi chote cha kikao hikina kuwawezesha wananchi wenzetu wenye ulemavu wa kusikia kufuatilia shughuli za Baraza kwa ukamilifu.  


Mheshimiwa Spika, mwisho navipongeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango wao mkubwa katika kudumisha amani, usalama na utulivu uliopo hapa nchini.



MASUALA MUHIMU YALIYOJIRI NCHINI


Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba nchi yetu inaendelea na mchakato wa kupata Katiba mpya  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kwa sasa katiba inayopendekezwa tayari imekabidhiwa kwa  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein. Makabidhiano hayo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri huko Dodoma, tarehe 8 Oktoba, 2014.


Mheshimiwa Spika, kutokana na tukio hili kubwa la kihistoria katika nchi yetu, hatuna budi kuwapongeza viongozi wetu hawa kwa kuanzisha na kufanikisha kupata Katiba Inayopendekezwa kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nawanasihi wananchi wote kupata muda wa kuisoma kwa kina katiba hiyo inayopendekezwa ili kuielewa na hatimaye kutumia haki yao ya kidemokrasia kushiriki katika zoezi la upigaji kura ya maoni wakati muda utakapofika.


Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nachukua fursa hii kuwapongeza kwa dhati kabisa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mheshimiwa Samuel John Sitta na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna walivyoliendesha Bunge hilo Maalum kwa ufanisi na mafanikio makubwa. Pia, nawapongeza wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba walioshiriki katika kuandaa Katiba Inayopendekezwa kwa wananchi.


Mheshimiwa Spika, nchi yetu inajivunia hazina kubwa aliyotujaalia Mwenyezi Mungu ya amani na utulivu tulionao ambao ni nyenzo kubwa kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu. Hivyo, hatuna budi sote kwa pamoja kuilinda na kuidumisha hazina hiyo kwani amani ikivurugika hakuna hata mmoja miongoni mwetu atakaebaki salama. Serikali itaendelea kwa juhudi zake zote kusimamia amani na utulivu tulionao na ni vyema viongozi na wananchi tukatoa ushirikiano katika kufanikisha azma hii.



Mheshimiwa Spika, Sekta ya Kilimo  bado inaendelea kuwa ni muhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar ambapo inatoa mchango wa moja kwa moja katika kujikimu kimaisha, kuwa na uhakika wa chakula, lishe na afya za wananchi walio wengi vijijini na mijini. Takriban zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wanategemea sekta hii kwa kuendeleza maisha yao.  Kwa mwaka wa fedha 2012/2013  sekta hii ilichangia wastani wa asilimia 30 ya Pato la Taifa.


 Mheshimiwa Spika, kwa Msimu wa Kilimo cha Mpunga cha Masika 2013/2014,  jumla ya ekari 30,444 (Unguja 12,548 na Pemba 17,896) zililimwa katika maeneo ya juu, sawa na  asilimia 87  na ekari 1,736 zililimwa katika maeneo ya umwagiliaji maji (Unguja ekari 1,143.61 na Pemba ekari 592.8) sawa na asilimia 88 ya lengo lililowekwa.


Mheshimiwa Spika,  katika msimu huo, jumla ya tani 21,895 za mpunga zimevunwa katika maeneo ya juu (tani 14,354 Pemba na Tani 7,541 Unguja) na tani 2,070 za mpunga katika maeneo ya umwagiliaji maji (Unguja tani 1,302 na Pemba tani 768) zilivunwa. 

Kupungua kwa uzalishaji wa mpunga katika msimu ulioainishwa umetokana na uvamizi wa viwavi jeshi hasa katika mkoa wa Kaskazini Unguja na kupungua kwa maeneo ya ukulima wa mpunga ekari 3,400 (Upenja ekari 700 na Mahonda ekari 2,700) kwa maeneo ambayo yanamilikiwa na Kiwanda cha Sukari cha Mahonda ambapo tayari mashamba hayo yamepandwa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa Sukari.


Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kuliendeleza eneo la hekta 2,410 Unguja na Pemba kwa ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji maji kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea Kusini na Serikali ya Marekani. Utekelezaji wa mradi huu mkubwa utasaidia sana katika kuendeleza  kilimo cha mpunga kwa uhakika na kuongeza uzalishaji na hivyo kuwaongezea kipato wakulima wetu na kuchangia katika kupunguza umasikini.

Mheshimiwa Spika, matayarisho ya uzalishaji wa zao la mpunga kwa kipindi cha 2014/2015 yamefikia hatua ifuatayo:

·  
 Serikali imeweza kununua matrekta 20 kutoka SUMA JKT pamoja na kuyafanyia matengenezo matrekta 24 makongwe ambayo tayari yameanza kazi ya ukulima katika kwa msimu wa kilimo cha mpunga 2014/2015. Lengo ni kuweza kulima eneo la ukubwa wa ekari 32,100 (Unguja 12,901 na Pemba 19,199).


·         Kwa upande wa pembejeo Serikali imefanya zabuni ya ununuzi wa mbolea tani 750 (Urea tani 600 na TSP tani 150), dawa ya kuulia magugu lita 15,000 pamoja na mbegu ya mpunga tani 150.


Mheshimiwa Spika, katika juhudi za uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali zetu, Serikali imekamilisha mapitio ya Sera na Sheria ya Misitu pamoja na Mpango wa muda mrefu wa matumizi ya maliasili. Aidha, juhudi za kuendeleza zao la karafuu nchini zinaendelea kwa matayarisho ya uzalishaji wa miche ya mikarafuu 650,000 katika vitalu vya Serikali na watu binafsi na hatimae kuisambaza kwa wakulima katika msimu ujao wa masika 2014/2015.


Mheshimiwa Spika, katika kuiendeleza Sekta ya Mifugo, Serikali imeendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu ufugaji bora. Katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2014, jumla ya wafugaji 5,432 wamepatiwa elimu hiyo kupitia vikundi vya wafugaji, mashamba darasa ya mifugo na mfugaji mmoja mmoja.


Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka tani 8,118,519 hadi tani 8,397,540 na uzalishaji wa mayai umeongezeka kutoka mayai  40,924,594 hadi mayai 49,900,389  kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2014. Aidha, huduma za upandishaji ng’ombe kwa sindano zinaendelea kuimarika na upatikanaji wa mbegu za kupandishia ng’ombe si tatizo tena kwa wafugaji.


Mheshimiwa Spika, kuhusu migogoro ya ardhi bado Serikali inaendelea kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo. Hali halisi inaonesha kwamba migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na wananchi wenyewe. Kesi nyingi zilizopo zinatokana na migogoro ya mipaka, uvamizi wa ardhi na mauziano yasiyo rasmi. Baadhi ya migogoro inasababishwa na muingiliano wa majukumu miongoni mwa taasisi na mamlaka zinazosimamia masuala ya ardhi katika utoaji wa vibali usiozingatia masharti na miongozo ya matumizi ya ardhi inayotolewa katika ngazi mbali mbali zikiwemo Halmashauri za Wilaya, Madiwani pamoja na Masheha. Aidha, kuna baadhi ya migogoro inasababishwa na watendaji wasio waaminifu ambao humilikisha na hata kushiriki katika mauziano ya ardhi yasiyo rasmi hali ambayo inapelekea wananchi kuuziana zaidi ya mara moja.


Mheshimiwa Spika, idadi ya kesi zinazowasilishwa katika Mahakama ya Ardhi zimekuwa zikiongezeka  siku hadi siku  na hili linatokana na hali halisi ya ufinyu wa ardhi katika visiwa hivi vya Zanzibar ukilinganisha na ongezeko kubwa la watu ambalo linaenda sambamba na ongezeko la harakati za kiuchumi na kijamii. Pamoja na kwamba idadi ya kesi zimekuwa zikiongezeka mwaka hadi mwaka lakini kasi ya usikilizaji na utolewaji wa maamuzi nayo kwa kiasi kikubwa imeongezeka.  Kwa mfano mwaka wa fedha 2011/12 jumla ya kesi 188 zilifunguliwa kwa Unguja na Pemba na kwa mwaka 2013/14 kesi zilizofunguliwa ni 210.


Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudiakukabiliana na hali hii kwa kuhakikisha kwamba migogoro ya ardhi inapungua au kumalizika kabisa. Ili kuhakikisha hilo linafanikiwa Serikali inajipanga katika kutekeleza mikakati ifuatayo:

  1. Kutoa elimu kwa wananchi kufuata taratibu na miongozo ya ardhi hasa katika umiliki na ujenzi wa nyumba.

  2. Kukamilisha maandalizi ya Sera ya Ardhi ambayo hivi sasa ipo katika hatua za mwisho.

  3. Kuimarisha zoezi la utambuzi na Usajili wa Ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi.

  4. Kuandaa Mpango Mkuu wa Taifa wa matumizi ya ardhi ambao utawezesha wananchi kutumia ardhi kwa kuzingatia miongozo imara.

  5. Kuzipitia tena na kuzifanyia marekebisho Sheria za Ardhi ikiwemo Sheria ya Mipango Miji ya mwaka 1959.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imeongeza idadi ya Mahakimu wa Mahakama ya Ardhi kutoka watatu hadi watano na kuongeza idadi ya wakadiriaji (assessors) kutoka 11 hadi 26. Hali hiyo imepelekea kuimarika kwa Mahakama hiyo kiutendaji. Vile vile, juhudi zinazoendelea hivi sasa za kupatikana majengo kwa ajili ya Mahakama za Ardhi katika ngazi za Mikoa zitaimarisha zaidi utendaji wa Mahakama.


Mheshimiwa Spika, dira ya Serikali kuhusu Sekta ya Mifugo na Uvuvi ni kuibadililisha Sekta ya Mifugo na Uvuvi kutoka katika mfumo wa uzalishaji wa kujikimu hadi kufikia kilimo cha biashara ifikapo mwaka 2020.  Azma hiyo, itafikiwa kwa mkakati wa kuimarisha hali ya uchumi na kijamii kwa jamii za wafugaji na wavuvi kwa kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji, kutoa huduma za ugani, kuongeza thamani na upatikanaji wa taarifa za masoko ili kuongeza uzalishaji na kipato.


Mheshimiwa Spika, hali ya sekta ya mifugo na uvuvi nchini inaendelea kuimarika siku hadi siku kutokana na kukua kwa soko la ndani, linachangiwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya soko la utalii nchini ambalo ni mtumiaji mkubwa wa bidhaa za mifugo na samaki, sambamba na ongezeko la watu mijini.  Hali hii imesababisha wananchi kuendelea kujiajiri katika sekta hizi hasa vijana kutokana na tija zake.


Mheshimiwa Spika, kutokana na mnasaba huo, mwelekeo wa Serikali hivi sasa ni kutatua changamoto muhimu zilizopo ili kuweza kutoa matokeo makubwa sasa (Big Results Now).  Hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:


1.            Kuendeleza utafiti na utoaji wa huduma za ugani kwa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi, ili wafugaji wetu waweze kupata faida kubwa, jambo ambalo litawafanya wananchi wengine hasa vijana kuendelea kujiajiri katika sekta ya ufugaji na uvuvi.  Suala la utafiti ni kikwazo kwa sekta zetu hizi, kuanzishwa kwa idara ambayo pia inasimamia suala la utafiti haitoshi, bali kuwepo kwa taasisi zinazojitegemea kushughulikia utafiti kisekta pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa utafiti, Serikali tayari imo katika mpango wa kufanikisha suala zima la vituo vya utafiti kwa kuanzia na sekta ya uvuvi na Serikali ya China na KOICA.


2.            Kuongeza uwezo wa kitaaluma kwa wafanyakazi na kuajiri wataalamu zaidi ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma mbali mbali kwa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi ikiwemo huduma za ugani, ujasiriamali katika shughuli za ufugaji na uvuvi.  Aidha, Serikali imo katika kuandaa mpango wa kuanzisha Chuo cha Uvuvi hapa Zanzibar.


3.            Kuongeza ajira kwa vijana kupitia shughuli za uzalishaji mifugo na uvuvi; ingawaje kila siku sekta hizi zimekuwa muajiri mkubwa wa vijana, lakini kwa makusudi Wizara itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya kuweza kujiajiri na kufanya kazi zao kwa faida.  Kwa hivyo, Serikali imekuwa ikiandaa programu tofauti zitakazowasaidia pamoja na kuwaunganisha na taasisi na mashirika ili kupata misaada na mikopo isiyo na masharti magumu.


4.            Kuendelea kuhamasisha wananchi kupandisha ng’ombe wa maziwa na nyama kwa kufuga kibiashara na kuondokana na mazoea.  Kwani hivi sasa ni kiasi cha asilimia 5 tu ndio ng’ombe wa kisasa wanaozalisha maziwa, bado fursa ipo kwa watu kubadilisha ng’ombe wa asili.


5.            Kuimarisha miundombinu ya kuendeleza uzalishaji wa mifugo ikiwemo vituo vya uzalishaji na utabibu wa mifugo (animal health and production centres) karantini na majosho.


6.            Kuimarisha shughuli za mazao ya baharini kwa kujenga kituo cha uzalishaji vifaranga vya samaki hapo Beit el Ras kwa mashirikiano na Shirika la FAO na KOICA.


Mheshimiwa Spika, Serikali pia itaendelea kuandaa mazingira mazuri ya kisera, sheria, kanuni na miongozo mbali mbali ili kuifanya sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kuendeleza sekta endelevu, ufugaji wa ng’ombe pamoja na uwekezaji wa viwanda vya usarifu wa samaki na mifugo bila kuathiri mazingira yetu.


Mheshimiwa Spika, Serikali pia imo katika kuandaa Mkakati Maalum wa Kuendeleza Sekta ya Uvuvi hapa Zanzibar, pamoja na Mkakati wa Kusimamia Utawala wa Baharini.  Aidha, Wizara inakusudia kutoa taaluma kwa wadau wote wa sekta ya uvuvi ikiwemo wavuvi pamoja na kushirikisha jamii katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kufanya tathmini ya shughuli za uvuvi; na pia kushirikiana na wanajamii na vyombo vya sheria kuendeleza doria katika maeneo ya hifadhi na shughuli nyengine za baharini.



MAMBO MUHIMU YALIOJITOKEZA BARAZANI


Mheshimiwa Spika, katika mkutano huu wa 17, Baraza lako Tukufu lilikamilisha mambo makuu manne yafuatayo:


                         i.    Kujibu maswali yaliyoulizwa na Waheshimiwa Wajumbe.

                        ii.    Uwasilishwaji wa miswada minne (4) ya Sheria ambayo ina umuhimu mkubwa kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu.


                       iii.    Kiapo cha uaminifu kwa Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

                       iv.    Hoja ya Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuliomba Baraza la Wawakilshi kutoa maazimio kuhusu uimarishaji wa huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi wa Zanzibar.


Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu Wajumbe waliuliza na kujibiwa maswali ya msingi na maswali ya nyongeza. Jumla ya maswali ya msingi 48 na maswali ya nyongeza 100 yaliulizwa na kujibiwa na Waheshimiwa Mawaziri wa Sekta husika. Nawapongeza Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliouliza maswali ya msingi ambayo yalikuwa na lengo la kudadisi utekelezaji na ufanisi wa shughuli za Serikali.  Aidha, nawapongeza na kuwashukuru Waheshimiwa Mawaziri kwa kutoa majibu sahihi ambayo yamewejengea uelewa Waheshimiwa Wawakilishi pamoja na wananchi kwa jumla.


Mheshimiwa Spika, Mswada wa mwanzo uliowasilishwa ni Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Wauguzi na Wakunga (uanzishwaji wa Baraza la Usajili wa Wauguzi na Wakunga) Nam. 9 ya mwaka 1986 na kuanzisha badala yake Sheria mpya ya Wauguzi na Wakunga na Mambo Yanayohusiana na Hayo.


Mheshimiwa Spika, Mswada huu una madhumuni ya kukabiliana na hali halisi ya mabadiliko yaliyopo hivi sasa ulimwenguni katika sekta ya Uuguzi na Ukunga ambapo Sheria Nam. 9 ya 1986 inaonekana kutokidhi haja kwa matumizi ya wakati huu.


Mheshimiwa Spika, Waheshimwa Wajumbe wa Baraza lako Tukufu walipata fursa ya kuchangia Mswada huu kwa kina ambapo wengi wao waliiomba Serikali kuwa makini katika kusimamia utekelezaji wake ili kuleta ufanisi uliokusudiwa. Pia wameiomba Serikali kuyaangalia upya maslahi ya wauguzi na wakunga ili kuwapa motisha katika kutekeleza majukumu yao.  Serikali imekisikia kilio hicho.


Mheshimiwa Spika, Mswada wa Pili uliowasilishwa ulikuwa ni Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Shirika la Nyumba la Zanzibar. Madhumuni ya Mswada huo ni kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba la Zanzibar kwa mujibu wa sheria ili kuweza kuziendeleza nyumba ziliopo nchini, kusimamia kodi, kujenga nyumba mpya na kutoa huduma nyengine zinazohusiana na masuala ya nyumba.


Mheshimiwa Spika, katika michango ya Waheshimiwa Wajumbe wameiomba Serikali kuwa makini na kuangalia madhumni ya kuanzishwa nyumba za maendeleo zilizopo nchini ambazo zimeanzishwa na Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na dhamira ya uanzishwaji wa sheria hii. Aidha, Waheshimiwa Wajumbe walionesha kuwepo kwa tatizo la umiliki na ukodishwaji wa nyumba kwa wananchi ambao wanaishi katika nyumba hizo.


Mheshimiwa Spika, Mswada wa Tatu uliowasilishwa ulikuwa unahusu kufuta Sheria ya Baraza la Manispaa Nam. 3 ya mwaka 1995 na Halmashauri za Wilaya na Mabaraza ya Miji Nam. 4 ya mwaka 1995 na kuanzishwa upya Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2014 kwa madhumuni ya kuanzisha Serikali za Mitaa, uwezo wake, kazi na wajibu, muundo, mpangilio, fedha na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo.


Mheshimiwa Spika, kuhusu Mswada huo Wajumbe wameishauri Serikali kuwa na tahadhari kubwa na kuangalia kwa makini suala la kijiografia juu ya mipaka ya Serikali za Mitaa. Aidha, waliishauri Serikali kumfanya Naibu Meya kuwa mfanyakazi wa kudumu na pia wameiomba Serikali kuboresha maslahi ya Madiwani kwa kuwapatia mishahara na sio kuwapa posho tu.


Mheshimiwa Spika, Mswada wa Nne uliowasilishwa unahusu kufuta Sheria Nam. 1 ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 1998 na kuanzisha Sheria mpya ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 2014 na Mambo Mengine Yanayohusiana na Hayo. Mswada huu unalenga kuweka mfumo wa Kiutawala wa Serikali Kuu kuanzia ngazi ya Shehia hadi Mkoa kwa kuzingatia mageuzi ya Serikali za Mitaa na kuondoa kasoro zilizojitokeza katika sheria ya sasa ya Tawala za Mikoa na kuweka mtiririko ulio bora zaidi kwa mujibu wa mahitaji ya sasa. Aidha, madhumuni ya mswada huu ni kupata Sheria itakayoonesha wajibu, muundo, kazi na uwajibikaji kwa kila ngazi ya Serikali Kuu kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya na Shehia na kukuza uhusiano baina ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.


Mheshimiwa Spika, Serikali imesikia na kuzipokea hoja za Waheshimiwa Wajumbe kuhusiana na miswada yote minne iliyowasilishwa na itazizingatia na kuzifanyia kazi hoja hizo kadri hali itakavyoruhusu.


HITIMISHO:


Mhesimiwa Spika, kwa mara nyengine tena naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe binafsi kwa umahiri wako na umakini mkubwa katika kuliendesha Baraza letu. Vile vile, narudia kuwapongeza na kuwashukuru Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, kwa kazi zao nzuri katika kusimamia utendaji wa Serikali na kwa michango yao yenye tija katika kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika Serikali.


Mheshimiwa Spika, nawashukuru Waheshimiwa Mawaziri wote waliosaidia kutoa ufafanuzi wa hoja mbali mbali zilizotolewa na Waheshimiwa Wajumbe. Pia nawashukuru waandishi wa habari na wakalimani wa lugha ya alama kwa kazi yao nzuri ya kuwapatia taarifa wananchi kuhusu majadiliano ya Baraza katika mkutano huu wa kumi na saba.


Mheshimiwa Spika, naomba tena kuwahakikishia Waheshimiwa Wajumbe kwamba Serikali yao chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein itajitahidi kuhakikisha kwamba inaimarisha utendaji na uwajibikaji katika Serikali na kuendelea kudumisha amani na utulivu.


Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo,sasa naomba kutoa hoja ya kuliakhirisha Baraza lako Tukufu hadi siku ya Jumatano, tarehe 21 Januari, 2015 saa 3.00 asubuhi panapo majaaliwa.



Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.


DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 4 WA KITAIFA KUHUSU UBORESHAJI VIWANGO VYA HUDUMA YA AFYA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano huo ulifanyika leo Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi tunzo za waliofanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya kwa Mkurugenzi wa huduma za uuguzi Hospitali ya Bugando jijini Mwanza Sister Viola Mumishi

Katika Mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano  huo ulifanyika leo Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini                    Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Afisa ustawi wa Jamii Damel Masunzu alipotembelea banda la Wizara ya Afya kwenye maonesho uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya. Katika Mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano  huo ulifanyika leo Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini                    Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasikiliza wahudumu wa mfuko wa bima ya Afya NHIF alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye  mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano huo ulifanyika leo Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja wa washiriki wa  

Mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano  huo ulifanyika leo Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini                    Dar es salaam. (Picha na OMR)

Un yaokoa maisha ya watoto 3000 Zanzibar

$
0
0
DSC_0152

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Zaidi ya watoto 3000 waliokuwa wakikabiliwa na utapiamlo nchini Zanzibar sasa wapo katika hali nzuri baada ya Umoja wa Mataifa (UN)kwa kushirikiana na wadau wengine kufanikisha programu ya kusaidia kukabili utapiamlo mkali kwa watoto hao.
kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni ambapo UN ilielezea mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja huo ukiadhimisha miaka 69 ya uwepo wake imefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana katika maeneo ambayo ilikuwa imejikita kusaidia kukabili umaskini,kuhakikisha utawala bora na kusaidia jamii.
Alisema pamoja na kuendeleza na juhudi za kukabiliana na utapiamlo katika visiwa vya Pemba pia Umoja huo umefurahishwa na hatua zilizofikia katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto na kusema ni wajibu kuhakikisha watoto hawana matatizo ya utapiamlo kwani wao ndio msingi wa taifa la sasa na lijalo.
Alisema hata hivyo upo umuhimu wa kuendelea na washirika wengine wa maendeleo kuona kwamba tatizo la utapiamlo la visiwa vya Pemba kwa watoto linamalizwa.
DSC_0177

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea kufurahishwa kwake na Serikali Tanzania kwa kupigia hatua katika kutoa ajira nyingi kwa walimu kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa unaendelea na ujenzi wa uwezo kwa baraza la wawakilishi ili kuhakikisha kwamba baraza hilo linawezesha kuwepo kwa sheria nzuri na bora na zinazotekelezeka ambazo hazikwazi kukua kwa demokrasia na ustawi wa jamii.
Aidha alisema kwa kuzingatia kwamba mwaka huu mwishoni kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na pia uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kura ya maoni ya katiba, Umoja huo unaendelea kufanyakazi na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuiwezesha kitaalamu kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa wananchi.
Aidha katika masuala ya utawala bora Umoja wa Mataifa unashirikiana na taasisi za sheria kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika mfumo wa sheria za watoto ili kuwepo na usalama mkubwa kwa watoto hasa kutokana na utamaduni uliopo visiwani kwa sasa.
Aidha alisema kwamba yamepatikana mafanikio makubwa katika sekta ya tiba na kuzuia maambukizi ya Ukimwi na kuondokana na unyanyapaa.
DSC_0121

Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar, Talib Ussi akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Aliwahimiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelezea mafanikio na pia changamoto zinazotokana na program za Umoja wa mataifa zilizolenga kusaidia maendeleo ya wananchi wa Zanzibar.


Alisema matokeo ya program ya kusaidia maendeleo ya Tanzania (UNDAP) ndiyo yatakayotumika kutengeneza UNDAP 2 ambayo inatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2016.
Katika mkutano huo ambapo waandishi walipata nafasi kubwa ya kuuliza masuala yanayohusu shughuli za Umoja wa Mataifa Zanzibar, Bara na duniani kwa ujumla Alvaro alizungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika.
Alisema pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, baada ya vita kuu ya dunia ya pili mwaka 1945 ya usalama na kujenga uchumi baada ya kuharibiwa na vita yapo palepale, mabadiliko katika utendaji kwa lengo hilo hilo la usalama na maendeleo ni dhahiri.
Alisema mathalani malengo ya millennia (MDGs) ambayo yalisanifiwa kwa lengo la kuleta maendeleo duniani katika demokrasia, utawala bora na ustawi wa jamii, bado yanatakiwa kuimarishwa kupitia mpango mpya wa maendeleo SDGs wenye lengo la kutokomeza umaskini uliotopea duniani ifikapo mwaka 2030.
DSC_0060

Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
Alisema ni matumaini yake kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na UN katika kuhakikisha kwamba mafanikio katika MDGs yanaendelezwa na pia kukamilisha yale ambayo hayakufikiwa kwa lengo la kutokomeza umaskini uliotopea ifikapo mwaka 2030.
Alisema mafanikio ya UNDAP kwenye utawala bora, ustawi wa jamii na uondoaji umaskini na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, ni matokeo ya ushirikiano kati yake ya mamlaka mbalimbali nchini Tanzania na kwamba UN itaendelea kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha maendeleo ya kuwezesha amani na usalama na ukuaji wa uchumi yanapatikana.
Naye Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema lengo la kukutana na waandishi wa habari wa Zanzibar lilikuwa kuangalia mafanikio na namna ambavyo program za Umoja wa Mataifa katika visiwa vya Zanzibar zinafanyakazi.
Alisema kwamba shughuli za Umoja wa Mataifa visiwani humo zinaweza tu kujulikana kwa wananchi kwa kupitia waandishi wa habari ambao wanakuwa wanajua Umoja huo unafanya nini na wapi.
DSC_0063

Mkutano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa Zanzibar ukiendelea.
DSC_0131

Mwandishi wa habari wa TBC, Kulthum Ally, akiuliza swali kuhusiana namna Umoja wa Mataifa unavyoweza kuwasaidia Wanawake wa Zanzibar kupata nafasi za uongozi sawa na wanaume.
DSC_0192

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (waliokaa katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) pamoja na Meneja wa Baraza la Habari Zanzibar, Suleiman Omar (kushoto) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Zanzibar.

Zeco kuna cha kujifunza hapa

$
0
0
 A solar farm in Tunisia could soon provide energy to around 2.5 million homes in the UK. It is said to be 20 per cent cheaper than other sources
Photo: www.nurenergie.com
Photo: www.nurenergie.com
A Tunisian solar power project could soon provide homes in the UK with energy. If approved by the British government, the project could see up to 2.5 million UK homes benefit from solar energy by the year 2018.
TuNur is a partnership between British renewables investor Low Carbon, developer Nur Energie, and Tunisian investors.
Kevin Sara, chief executive of TuNur had this to say of the project, “This is a serious project. Yes, it is risky like any big energy project is risky.”
TuNur says that they will provide energy that is 20 per cent cheaper than other sources.
Source: Daily Mail

Mihadarati yaongeza uhalifu Zanzibar

$
0
0
Na Mwinyi Sadallah
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekiri kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu katika mji mdogo wa Mochuari kisiwani Pemba kutokana na kushamiri kwa matumizi ya dawa za kulevya - mihadarati
                              
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachofanyika Chukwani mjini hapa.
Alisema kutokana na tatizo hilo, polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba wameamua kuanzisha operesheni ya kila mara ya kuwasaka watumiaji wa dawa za kulevya pamoja na wauzaji na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Waziri Aboud alisema eneo la Mochuari ni sugu kwa vitendo vya uhalifu.
Alisema tayari operesheni saba zimefanyika katika eneo hilo na watu watatu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kukutwa na pombe za kienyeji na dawa za kulevya.
“Mheshimiwa Spika, polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, wataendelea kufanya oparesheni endelevu hadi kero za uhalifu zitakapokoma katika eneo la Moshuari,” alisema Waziri aboud. Awali, mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Juma alitaka kujua ni lini SMZ itachukua hatua ya kukabiliana na vitendo hivyo.
 
Chanzo : Mwananchi

Sherehe za Kuipongeza Timu za Michezo za KMKM viwanja vya Maisara

$
0
0
Mbio za kilomita 10 zikiaza katika eneo la Kibweni Ikulu lililowashirikisha wakimbiaji zaidi ya 330 wa Kimataifa wa Zanzibar na Wanamichezo wa vikundi vya mazoezi vya Kitambi noma wakiaza mbio hizo kuelekea katika viwanja vya maisara KMKM.
Wakimbiaji wa mbio za kilimita 10 wakiaza mbio hizo katika maeneo ya Kibweni Ikulu barabara ya bububu kuelekea viwanja vya maisara.
     Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mchezo wa mbio za kilimita 10 zilivyoaza kwa ushindani mkubwa.
Wakimbiaji kutoka Ndijani wanawakev wakishiriki mbio hizo za kilomita 10 wakionesha uvundi wao.
Wakimbiaji kutoka vikosi vya Ulinzi na Usalama wakishiriki mbio hizo wakioneshana ufundi.wakipita katika maeneo ya maruhubi wakiwa katika nafasi ya tatu na nne katika michuano hiyo ikielekea katika viwanja vya maisara.
Mshindi wa kwanza wa mbio hizo za kilimita 10 Filipo Jacob kutoka Mafunzo Zanzibar akiongoza mbio hizo akifuatiwa na mkimbiaji kutoka JWTZ Elia John, wakipita katika maeneo ya muembemakumbi kuelekea maisara kumalizia mbio hizo.
Mshindi wa mbio za kilimita 10 kutoka Kikosi cha Mafunzi Filipo Jacob, akimaliza mbio hizo kwa kuwa mshindi wa kwanza wa mbiuo hizo za kusherehekea Ubingwa wa Timu za Vikosi vya KMKM Zanzibar kwa kuchukua ushindi kwa miaka miwili mfululizo  
Mkimbiaji kutoka JWTZ Elia John, akisaidiwa kumaliza mbuio hizo baada ya kubana na misuli akiwa karibu kumaliza mbiop hizo katika viwanja vya maisara alikuwa akichuana na mshindi wa mbio hizo Filipo Jacob. 
Mkimbiaji wa Kike kutoka KMKM Aldina Edward akimaliza mbio hizo kwa kuwa mshindi wa kwanza kwa wanawake walioshiriki mbio hizo.
Katika mbio hizo pia zimawashirikisha Wanamichezo wwenye ulemavu kama anavyooneka mwanamchezo Hadaa Khatib akimaliza mbio hizo katika viwanja vya maisara.
Mkimbiaji kutioka Japan Seiki Shinizy  akishiriki mbio hizo na kutchukua nafasi ya 45katika mbio hizo 
         Viongozi wa meza kuu wakifuatilia sherehe hizo katika viwanja vya KMKM Maisara
Maofisa Wastaaf wa KMKM wakivuta kamba na Maofisa wa KMKM katika sherehe hizo wakiongozwa na Kocha wao Mzee Haidar wakiongoza jinsi ya kufuta kamba na kushinda mara mbili na kujinyakulia fedha zilizotolewa na Mfanyabiashara Muhamadi Pande kwa mshindi wa mchezo huo na kujinyakulia shilingi laki tano zilizotolewa kwa mshindi wa mchezo huo.
Maofisa wa KMKM wakishindana kufuta kamba na Maofisa wastaaf wa KMKM hatimai kushindwa na Maofisa Wastaaf mara mbili ya mchezo huo. 
Maofisa waastaf wa KMKM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwashinda Maofisa wa KMKM katika mchezo wa kuvuta kamba na kujinyakulia shilingi laki tano zilizotolewa na Mfanyabiashara maaruf Zanzibar Muhamadi Pande kwa mshindi wa mchezo huo.

Mkim,biaji kutoka Kikundi cha mazorzi cha ZAFISA akimaliza mbio hizo katika viwanja vya maisara akishindikizwa na msimamizi wa mbio hizo 
Mkuu wa Kikosi Cha KMKM Komodoo Hassan Mussa, akizungumza katika uzinduzi wa kusherehekea Ubingwea na Timu za KMKM kwa miaka miwili iliochukuwa katika michezo. uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya KMKM maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanamichezo wa KMKM kwa kuwa mabingwa wa mchezo wa Mpira wa miguu za Ligi Kuu Grand Malt Zanzibar  kwa miaka 2012/2013 na 2013/2014. sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya mpira maisara Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za kilimita 10 kwa wanawake kutoka KMKM Aldina Edward.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi yake mshindi wa kweanza wa mbio za kilimita 10 Wanaume Filipo Jacob
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi mshindi wa Pili wa mbio hizo kwa Watu wenyev Ulemavu Amina Daud.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Ofisa Mstaaf wa KMKM Ndg Fetei kwa ushindi wa kufuta kamba walikabidhiwa shilingi laki tatu zilizotolewa na Mfanya Biashara wa Zanzibar Ndg Muhamad Pande. kwa kuvutiwa na Maofisa hao wastaaf kwa kuwa na stamia ya kuhimili mikiki ya Vijana Maofisa wa KMKm katika mchezo huo.



                       Maofisa Wastaaf wa KMKM wakifuatilia michuano hiyo ya sherehe
                                Mambo ya mbwa kachoka hayoooooooooo

Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania Latoa Tamko kwa Baadhi ya Viongozi kuitumia TAHLISO

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                                                                                                               01 Nov 2014

Ndugu waandishi wa habari ,

Kwanza napenda kumshukuru M/Mungu kwa mapenzi yake ya kutukutanisha hapa leo tukiwa wazima wa afya , pili napenda kuchukua fursa hii kukushukuruni nyie waandishi wa habari kwa kupoteza muda wenu na kuja kushirikiana na sisi , kwa hili tunawashukuru sana.


Ndugu waandishi wa habari,

Tuliopombele yenu ni viongozi halali wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) ambao tumechaguliwa kihalali tarehe 14/12/2014 kufuatia uchaguzi mkuu wa TAHLISO uliofanyika chuo cha Afya Bugando Mwanza, ambapo uchaguzi huo ulimchagua ndugu Mussa Mdede (Mwenyekiti), ndugu Abdi Mahamoud Abdi (Makamo mwenyekiti), ndugu Halima Bakari Nyange (katibu mkuu), ndugu Rajab Ali Rajab (Naibu katibu mkuu), ndugu Mollel Hillary (Mhazini) na ndugu Khamis Hamza Khamis (Mhazini Msaidizi).


Ndugu waandishi wa habari

Kwa mujibu wa katiba ya shirikisho la vyuo vikuu Tanzania (TAHLISO) ibara ya 5 (2) NI MARUFUKU kwa kiongozi yeyote haswa wa ngazi ya juu katika TAHLISO kushiriki katika shuhuli zozote za kisiasa haswa kupanda juu ya majukwaa ya kisiasa kwani kufanya hivyo nikuiwakilisha taasisi katika siasa wakati TAHLISO ni taasisi ya kijamii, lakini Mh. Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) ndugu Mussa Mdede alishiriki katika vugu vugu la siasa za vyama vingi kwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kalenga kufuatia kifo cha aliekua Mbunge wa jimbo hilo Mh. Marehemu Mgimwa



Ndugu waandishi wa habari,

Kwa kua katiba ya TAHLISO hairuhusu viongozi kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa tarehe 3 April 2014 katika chuo cha kodi jijini Dar es salaam.TAHLISO tulikutana katika  kikao cha senate na kikao kiliamua kumuondoa madarakani ndugu Mussa Mdede kutokana na kuenda kinyume na katiba hiyo pia kikao kiliamua nafasi yake ikaimiwe na makamo mwenyekiti Ndudu ABDI MAHAMOUD ABDI mpaka pale Shirikisho litakapofanya uchaguzi mwengine au ikionekana kuna haja ya kufanya uchaguzi mdogo kabla ya uchaguzi wa December mwaka huu. Kwa kushangaza mara tu baada ya miezi sita kupita na kubadilika kwa viongozi katika serikali za wanafunzi katika vyuo mbali mbali Ndugu Mussa Mdede aliitisha kikao na kuwadanganya viongozi wapya wachache waliofika katika kikao hicho na kuendelea kujitangaza kwamba yeye ni mwenyekiti wa TAHLISO katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo tv na magazeti pamoja kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu kuandamana na kufanya migomo kwa ajili ya kuikomoa serikali.


Ndugu waandishi wa habari,

Hapa ndo tunataka mtutegee masikio yenu, vipaza sauti vyenu pamoja na kamera zenu kua Shirikisho la vyuo vikuu Tanzania TAHLISO na Shirikisho la vyuo vikuu Zanzibar ZAHILFE tunakemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa siasa nchini kuanzisha tabia mbaya ya kuwaita wanafunzi wa vyuo vikuu kisiri siri katika majumba yao, mahoteli mbalimbali na kupanga nao vikao vya siri, kualika viongozi wengi wa serikali za wanafunzi kutoka Tanzania bara kuja kushiriki mikutano mikubwa katika hoteli zilizopo Zanzibar  ili kuweza kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kuwaunga mkono katika maadhimio yao. Shirikisho la vyuo vikuu nchini tunawaomba wanasiasa kuwacha tabia hiyo mara moja kwani tabia hiyo ndio iliyopelekea machafuko katika nchi mbali mbali duniani kama vile Libya, Bakhrein, Misri,Uturuki na nchi nyengine nyingi kuwataka wanafunzi kuandamana na kuwaahidi mambo mengi makubwa ambayo kiuhalisia hayatekelezeki na kuingiza nchi katika vita visivyo koma kama tunavyoona katika nchi kama vile LIBYA na MISRI katika kipindi hiki


Vile vile tunaziomba serikali zote mbili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo husika pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kulifuatilia suala hili na kulikataza mara moja kutokana na sababu kwamba amani ya nchi ikiondoka ni vigumu sana kuirudisha vile vile mambo haya yanaweza kuligharimu taifa kwa kupoteza wananchi wengi wasiokua na hatia.


Ndugu waandishi wa habari

MWISHO tunanapenda kuchukua fursa hii kuwaomba wanafunzi wote wa Tanzania kuitafuta katiba pendekezwa kuipitia na kuisoma katiba pendekezwa ya bunge maalum sura kwa sura ibara kwa ibara na neno kwa neno, ili kuifahamu na kuielewa na kuwacha kuwasikiliza wanasiasa ambao wanamalengo yao binafsi na ikifika april mwakani kuja kuipigia kura katiba hii kwa kua tulishirikishwa tokea mwanzo kwenye kutoa maoni ya mtu mmoja mmoja, vikundi, mabaraza na mwisho kushirikishwa katika hatua  muhimu ya bunge maalum la katiba ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia taasisi zetu hizi ya ZAHILFE na TAHLISO tulitoa wawakilishi na kufaanikiwa kuingiza maoni yetu katika katiba na kueka historia ya taifa na kushiriki kuandaa misingi mizuri ya nchi yetu hususan katika vipengele vyote vinavyo ashiria kuufanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kua imara zaidi kwa kuziondoa kero zote za muungano huu uliodumu kwa muda wa miaka 50 sasa.     

Imetolewa na:

Abdi Mahamoud Abdi

Makamo mwenyekiti TAHLISO


                                  

Kaimu Mwenyekiti wa TAHLISO Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar

$
0
0
Kaimu Mwenyekiti wa TAHALISO Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, akizungumza na waandishi wa habari kulaani vitendo vya Baadhi ya Viongozi wa TAHLISO kutumia vyeo vyao katika majukwaa ya kisiasa kwa kutumiwa na Viongozi wa siasa kwa shirikisho hilo wanakwenda kinyume na Katiba ya Tahliso.Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mdogo wa bwawani hoteli.  . 
Katibu Mkuu wa TAHLISO Ndg Rajab Ali Rajab, akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari kuhusiana na baadhi ya Viongozi swa TAHLISO  wanajishughulisha nac kutumiwa na Wanasiasa kwa kupitia TAHLISO kuwatumia Vijana wa Vyuo Vikuu walioko katika Uongozi wa Shirikisho hilo.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Uongozi wa Kitaifa wa TAHLISO kulaani vitendo vya baasdhi ya Viongozi wa TAHLISO kutumia shirikisho hilo katika majukwaa ya kisiasa 
Viongozi wa TAHLISO wakiwa katika ukumbi wa mkutano na waandishi wa habari Zanzibar
Waandishi wakifuatilia mkutano huo kwa kuchukuwa point katika mkutano huo na viongozi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Tanzania uliofanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya bwawani.


Viewing all 34163 articles
Browse latest View live




Latest Images