Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa wadi za Makunduchi yamefunguliwa rasmi na Mbunge wa Makunduchi, Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa mambo muhimu yaliyofanyika kwenye sherehe hiyo ni kukabidhiwa baiskeli 18 walimu wa mafunzo.
Baiskeli hizo zimetolewa kama zawadi na ndugu Mohamed Simba. Mgeni rasmi akimkabidhi baiskeli mwalimu kutoka Sweden ambaye anawakilisha wenzake.
Mafunzo ya ujasiriamali yanaendeshwa chini ya mashirikiano kati ya wadi za Makunduchi na Munisipaliti ya Kiruna. Muda wa mafunzo ni mwaka mmoja.