Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Meya adai kuna miungu watu CHADEMA

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad,Mwanza
MEYA wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Nd. Henry Matata, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekiponda vikali chama hicho akidai  kimekuwa kikijiendesha kwa kutumia mabavu,ukabila na uchu wa madaraka na kwamba kuna viongozi hawaguswi.
Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake kuhusiana na mgogoro wa umeya katika manispaa hiyo baada ya kuwafukuza madiwani wenzake watatu wa Chadema kwa kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Alisema mfumo wa chama hicho ni batili kwa kuwa umekuwa ukiendesha mambo yake kimabavu kwa kuangalia sura za watu na kudai kuna watu ndani ya chama hicho hata wakifanya makosa hawaguswi.

Alisema uendeshaji wa mambo ndani ya chama hicho ni batili kwa kuwa katiba ya chama hicho inaminywa maksudi bila demokrasia kuchukua mkondo wake.
“Mfumo wa Chadema ni batili unakwenda kinyume na sheria za nchi,chama kinaendeshwa kimabavu na ukabila, kuna watu wakifanya makosa hawaguswi,” alisema.
Akizungumzia ugomvi baina yake na Mbunge wa jimbo la Ilemela, Highness Kiwia, alisema Mbunge huyo hajitambui na wala hatambui nafasi yake huku akisisitiza kuwa vurugu anazofanya ni kutokana na hofu kwamba huenda yeye akagombea katika uchaguzi ujao kwa kuwa anakubalika na watu.
Kuhusu hatma yake ndani ya Chadema alisema katika uchaguzi mkuu ujao ataangalia chama kinachomfaa lakini kwa sasa amebaini kwamba chama kilicho na demokrasia ni CCM pekee kwa kuwa hakiendeshwi kibabe.
“Nitaangalia chama ambacho kitanifaa lakini kwa sasa nawaona CCM afadhali kwani hakina ugomvi, ubabe, kufukuzana, uhasama tofauti kabisa na Chadema,”alisisitiza.
Kuhusu hatma ya madiwani wa Chadema aliowafukuza, alisema  suluhisho ni serikali kutangaza uchaguzi mdogo kwa nafasi hizo vyenginevyo ni sawa na “kutwanga maji kwenye kinu.” 
Alisema yeye kama meya wa Chadema ataendelea kuchapa kazi za kuwatumikia wananchi bila wasiwasi na endapo kama kuna diwani atakiuka sheria ya kushiriki vikao vya baraza la madiwani mara tatu mfulululizo atachukuliwa hatua bila kujali chama anachotoka.

Aidha alisema kamwe madiwani hao hawana haki ya kukata rufaa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zaidi ya kwenda mahakamani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>