Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Serikali yaombwa kusimamia haki za watoto

$
0
0
Na Husna Mohammed
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeombwa kusimamia ipasavyo jukumu la kulinda haki za watoto kwa kudhibiti matukio ya udhalilishaji ikiwemo ubakaji.
Akiwasilisha ripoti ya utafiti kuhusu ukatili kwa wanawake na watoto katika wilaya sita za Unguja na Pemba huko ofisi za TAMWA Zanzibar Mombasa, Ofisa wa Jumuya hiyo, Asha Abdi, alisema iwapo serikali itasimamia ipasavyo haki hizo kwa kiasi kikubwa itatoa nafasi kwa watoto wa kike kutumia umri wao katika suala zima la kupata elimu.
Sambamba na hilo, alisema haki hizo pia zitawawezesha kuwapatia fursa zinazostahiki wanawake ili waweze kupunguza wimbi la utegemezi.
Akizungumzia kuhusu kukabiliana na kesi za udhalilishaji alisema, serikali haina budi kuwapatia motisha na malipo ya kutosha watendahji wa sekta za sheria ili kupunguza tatizo la rushwa.
“Ni lazima hatua kali zichukuliwe kwa atakaepatikana ama kutoa au kupokea rushwa kwani kufanya hivi kwa kiasi kikubwa kutasukuma mbele kesi za udhalilishaji ambazo zinaonekana kukwama hasa vituo vya polisi,” alisema.

Alisema utafiti huo umebaini kukosekana ushirikiano wa kutosha baina ya polisi, mahakama, ustawi wa jamii, wanasheria na wanaharakati wa kupinga udhalilishaji jambo ambalo TAMWA imependekeza kuandaliwe mtandao madhubuti utakaosimamia kwa pamoja matukio hayo.
Akioa takwimu za matukio ya udhalilishaji kwa kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka 2013 kwa wilaya hizo,alisema makosa yalioripotiwa ni 996 yakiwemo ya ubakaji, mimba za umri mdogo, ndoa za mapema, kutelekeza wanawake na watoto na kubakwa.
“Matukio ya kupigwa ni mengi kuliko yote kwani yamefikia 388, yakifuatiwa na ubakaji 242 na 228 ni mimba za umri mdogo, utelekezaji wa wanawake na watoto 96 na ndoa za umri mdogo ni 42,”alisema.
Alizitaja wilaya ambazo zimefanya utafiti wa matukio hayo kuwa ni pamoja na kaskazini ‘B’ , wilaya ya kati, wilaya ya kkazini ‘A’, wilaya ya kusini na qilaya ya mjini kwa Unguja ambapo Pemba ni wilaya moja tu ya Chake Chake.
Mara baada ya kuwasilisha ripoti hiyo, wanahabari walipendekeza kuwa ni lazima kuwe na ajenda ya pamoja itakayosaidia kuzisukuma kesi zinazohusu udhalilishaji kwa vyombo vya habari.
Walisema kuripoti wingi wa takwimu za kesi hizo hazitasaidia kitu bali ni lazima vyombo husika vya sheria vitiwe msukumo wa kutosha katika kusughulikia kesi hizo.

Utafiti huo ulihusisha vyombo mbalimbali vya habari na ulisimamiwa na Chama vha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) na kufadhiliwa na UNFPA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>