Katibu wa JBC.Bi Munira H Said, akitowa ratiba ya mkutano wa pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman na ya Zanzibar katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Grand Palace Malindi.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar Abdallah A Omar akizungumza katika mkutano huo na Wafanyabiashara wa Oman,katika ukumbi wa hateli ya Grand Palace Malindi Zanzibar na kuhudhuriwa na Wafanyabiashara wa Zanzibar na Taasisi za huduma za Kibenki na Uwekezaji Zanzibar.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Tanzania Bwa. Maembe N E, akizungumza katika mkutano huo, wa kukuza Ushirikiano wa Jumuiya ya Pamoja ya Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, ulioundwa mwaka jana.
Balozi wa Tanzania Nchini Oman Ali Ahmeid Saleh akizungumza na kutowa ufadanizi wa Kikao hicho.Katibu wa FGCCC Bwa. Abdulrahim Naqi, akizungumza katika mkutano huo wa Wafanyabiashara pande hizi mbili za Oman na Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Maofisa wa Taasisi za Serekali wakifuatilia mkutano huo uliowasilisha Mada za Taasisi za Fedha na Vitenga Uchumi kutowa malengo ya miradi mbalimbali, wakati wa mkutano huo wa kukuza Biashara kati ya Zanzibar na Oman.
Mtoa Mada ya Sekta binafsi Bi, Hafsa Mbamba kutoka Grassroot, kuhusiana na uwekezaji na vitega uchumi wakati wa mkutano huo na Wafanyabiashara wa Oman uliofanyika Ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.Baadhi ya Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman wakifuatilia mkutano huo, na Wafanyabiashara wa Zanzibar.
MKURUGENZI wa Huduma za Benki wa PBZ Mohammed Said Mohammed, akitowa mada kuhusiana na huduma za PBZ zinazotolewa kwa Wateja wake na mikakati ya baadae ya kupanua huduma hizo kwa Jamii na nje ya Nchi, wakati mkutano wa pamoja wa Wafanyabiashara wa Oman na Zanzibar uliandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiasha Zanzibar wakati wa ziara maalum ya Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman na Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bwa. Juma Amour, akitowa ufafanuzi kutokana na Mada ya PBZ iliowasilishwa katika mkutano huo, Jinsi PBZ inavyotowa huduma kwa Wateja wake wa Nje ya Zanzibar na ndani, wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
Viongozi wa Jumuiya za Wafanyabiashara wakifuatilia Mada zinazowakilishwa katika mkutano huo wa kuimarisha uhusiano wa Kibiashara kwa pande mbili za Oman na Tanzania baada ya kuundwa kwa Jumuiya ya pamoja ya Biashara
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman, Bwa. Khalil Bin Abdallah AlKhonji, akizungumza na Wafanyabiashara wa Zanzibar katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya hizo mbili uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi.
Wafanyabiashara wa Zanzibar wakifuatilia mkutano huo.Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Bwa. Khalil Bin Abdallah Al Khonji, akimkabidhi Ngao yenye picha ya Jengo jipya la Jumuiya ya Oman, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar Bwa. Abdallah A Omar, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
RAIS wa Jumuiya ya Wafanyabiasha Zanzibar Abdallah A Omar, akionesha Ngao ya Jengo Jipya la Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman , baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Bwa. Khalil Al Khonji na kulia Balozi wa Tanzania Nchini Oman Ali Ahmeid Saleh.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman Bwa. Khalil Bin Abdallah Al Khonji, akimkabidhi Ngao yenye picha ya Jengo jipya la Jumuiya ya Oman, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Tanzania Bwa. Maembe N E, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar. KATIBU wa FGCCC Bwa, Abdulrahahim Naqi,akibadilisha mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour(katikati), baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa pamoja kati ya Wafanyabiashara wa Oman na wa Zanzibar ulioandialiwana Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace malindi kulia Mkurugenzi huduma wa PBZ Said Mohammed Said.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar Bwa. Abdallah A Omar, kulia akibadilishana mawazo na Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa kukuza ushirikiano wa kibiashara kwa pande mbili hizi baada ya kuundwa kwa Jumuiya ya pamoja ya Biashara kati ya Oman na Tanzania.kushoto balozi wa Tanzinia Nchini Oman, Balozi Ali Ahmeid Saleh.