Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa ya Walipa Kodi Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhin Shaban, akiongoza Mkutanonwa Rufaa ya Kodi kwa Kijiji cha SOS Zanzibar, wakipinga makadirio waliotakiwa kulipa ikiwav kama Kodi ya TRA kwa kuingiza Vifaa mbalimbali kwa vipindi tofauti kodi ya karibi shilingi milioni mia tisa, mkutano huo wa Rufaa umefanyika katika Ofisi za Bodi hiyo Wizara ya Fedha Zanzibar.kulia Mjumbe wa Bodi hiyo Kamal S Kombo..
Mjumbe wa Bodi ya Rufaa ya Walipo Kodi Zanzibar Kamal Kombo akizungumza katika mkutano huo wa Rufaa uliofanyika katika Ofizi za Bodi hiyo Wizara ya Fedha Zanzibar.
Wawakilishi wa TRA wakiwa na Wakili wao wakifuatilia mawasilisho ya Malalamikaji kupitia Wakili wake akiwakilisha katika kikoa hicho cha kwanza cha Rufaa tangu kuazishwa kwa Bodi hiyo Zanzibar Bodi hiyo ni ya Pili baada ya kwanza kumaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa ya Walipa Kodi Zanzibar Mhe. Khamis Shaban Ramadhan,na Wajumbe wa Bodi hiyo kulia Bwa.Kamal .S. Kombo na kusho Bwa Ahmeid Maulid Simai , wakimsikiliza Wakali wa mlalamikayi wa Kijiji cha SOS,Suleiman Salum, akiwakilisha.
Wakili walalamikaji wa SOS Zanzibar Suleiman Salum, akizungumza katika mkutano huo wa kwanza kuwasilishwa kwa madai ya kupinga makadirio ya Kodi, uliofanyika katika Ofisi za Bodi hiyo Wizara ya Fedha Zanzibar
Wakili wa Wadai TRA akiwasilisha madai ya Mteja wake katika mkutano huo wa Rufaa ya Bodi ya Walipa Kodi Zanzibar, uliofanyika katika Ofisi yake iliko Wizara ya Fedha Zanzibar.
Waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano wa Kwanza wa Bodi ya Rufaa ya Walipakodi Zanzibar,uliofanyika kwa kuwasilishwa Madai ya Mlalamikaji Kijiji cha SOS Zanzibar.