Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif akutana na Waziri wa fedha wa SMT pamoja na manaibu wake

$
0
0
 Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Saada Mkuya akielezea mikakati ya Wizara yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi mpya wa Wizara ya Fedha ya SMT uliofika Ofisini kwake kujitambulisha rasmi.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Fedha wa SMT Mh. Saada Mkuya, Kushoto ya Balozi ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Adam Malima na nyuma yake  Naibu Mwenzake Mh. Mwigulu Nchemba.

Wa kwanza kushoto waliosimama nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nd. Khamis Mussa.

Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Uongozi wa Wizara ya Fedha ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umekumbushwa kuzingatia uadilifu wakati unapotekeleza majukumu yake hasa yale masuala yanayohusu Zanzibar ikiwa ni njia moja wapo ya kuendelea kupunguza au kuondosha kabisa kero za Muungano.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Uongozi Mpya wa Wizara ya Fedha ya Serikali ya Muungano ukiongozwa na Waziri wake Mh. Saada Mkuya aliyefuatana na Manaibu wake wawili Mh.Adam Malima na Mh. Mwigulu Nchemba walipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi mara baada ya kuteuliwa kushika nyadhifa hizo.

Balozi Seif alisema licha ya juhudi na mafanikio makubwa yaliyochukuliwa na Viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali zote mbili chini ya Kamati ya pamoja ya kutatua kero za Muungano  lakini bado juhudi za ziada zinapaswa kuchukuliwa ili kuona kero zilizobakia zinapatiwa ufumbuzi na kubakia kuwa  historia tu hapa Nchini.

Alisisitiza kwamba huu ni wakati kwa Uongozi huo kuhakikisha kwamba yale mambo ambayo yanatakiwa kuchukuliwa hatua  na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  yanapaswa kufanywa kwa uadilifu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya pamoja na Manaibu wake kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo akielezea matumaini yake kwamba watafanya kazi kwa ushirikiano pamoja na upendo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe aliouongoza  Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Saada Mkuya aliahidi kufanya operesheni maalum ya kuondoa kero za Muungano  katika kipindi kifupi kijacho.

Mh. Saada alisema hilo litawezekana iwapo suala la mawasiliano litazingatiwa kuwa la msingi pamoja na kujenga nguvu za pamoja katika ushiriki wa vikao vya pande zote mbili vitakavyokuwa vikifuatilia utekelezaji wa mikakati inayowekwa na kukubalika.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>