Mwanasheria wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar akitowa maelezo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Jengo la Shirika la Magari Malindi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya PBZ Islamic Bank Mpirani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Rashid Ali na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Mhe. Juma Amour, wakitiliana saini ya makubaliano ya makabidhiano ya Majengo ya pande mbili Wizara ya Biashara imeikabidhi PBZ jengo la Shirika la Magari malindi na PBZ imeikabidhi Wizara ya Biashara jengo lake la PBZ lilioko Darajani.PBZ itatumia eneo hilo kujenga Jengo la Kisasa la Makao Makuu ya PBZ.
Kaimu Meneja wa Shirika la Magari Zanzibar Ndg. Thabit Mwinyi, akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Ali, hati ya Umiliki wa jengo hilo, katika hafla ya makabidhiano majengo hayo iliofanyika katika Ofisi za MakaoMakuu ya PBZ Islamic Bank Mpirani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Mhe. Rashid Ali, akionesha Hati ya Umiliki wa Jengo la Shirika la Biashara la Magari, kwa Uongozi wa PBZ na Wizara ya Biashra kabla ya kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour.katikati Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Mhe. Abdurahaman Mwinyi.makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya PBZ Islamic Bank Mpirani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Zanzibar Mhe. Rashid Ali, akimkabidhi Hati ya kumiliki Jengo hilo baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria, kuhamisha miliki ya jengo hilo kwenda Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ, katikati Mwenyekitin wa Bodi ya PBZ Mhe. Abdurahaman Mwinyi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Mhe. Abdurahaman Mwinyi, akizungumza na kutowa maelezo kwa Waandishi wa habari waliouliza maswali wakati wa makabidhiano ya majengo hayo, hafla iliofanyika katika Ofisi za PBZ Islamic Bank. Mpirani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Mhe. Juma Amour, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kutokana na ujenzi wa Jengo la Kisasa lenye hadhari ya Kibenki , katika eneo hilo linalotarajiwa kuaza ujenzi wake hivi karibuni baada ya kukamilisha kwa taratibu wa ujenzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Rashid Ali akizungumza katika hafla hiyo.
Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Majengo ya pande hizo mbili wakati wa makabidhiano wa Nyaraka za hati miliki.
Viongozi wa Wizara ya Biashara wakifuatilia hafla hiyo.Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ, Abdulrahama Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Mhe. Rashid Ali na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour, wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa PBZ na wa Wizara ya Biashara Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Mhe.Abdulrahaman Mwinyi na Mkurugenzi wa PBZ Mhe. Juma Amour, wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar, nje ya Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya PBZ Islamic Benk, lilioko katika maeneo ya Mpirani Zanzibar.