Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

ZIRPP yaandaa Semina kuhusu Rasimu ya Katiba

$
0
0



SEMINA KUHUSU RASIMU YA KATIBA

Kwa heshima na taadhima kubwa, nina furaha kukuarifuni kuwa, kwa niaba ya uongozi wa ZIRPP, mnaalikwa kuhudhuria na kushiriki katika Semina Mahsusi kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayowasilishwa katika Bunge Maalum la Katiba mnamo siku chache zijazo.

Kuhudhuria na kushiriki kwenu katika mjadala huu muhimu sana katika historia na mustakbali wa taifa letu, kutasaidia sana katika jitihada zetu za pamoja za kuchangia fikra na mawazo yatakayowasaidia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kufanya maamuzi ya busara kwa madhumuni ya kupata Katiba itakayozingatia na kuwakilisha maslahi ya wananchi wote bila ya kujali kabila, rangi, jinsia au itikadi zao za kisiasa.

Semina hiyo itafanyika katika Ukumbi wa SUZA uliopo ndani ya Jengo la Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni, Vuga, siku ya Jumapili tarehe 09 Februari 2014, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana; na itakuwa chini ya Uenyekiti wa Bibi Mariam Mohammed Hamdani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya ZIRPP na Mwanahabari mzoefu.

Mchango wenu adhimu katika mjadala huo utathaminiwa sana.


Muhammad Yussuf
MKURUGENZI MTENDAJI
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: 0777 707820 Cellular;
Tel: 0242 223 8474 Office;
Fax: 0242 223 8475;
Website: www.zirpp.org

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>