Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
(إن الله وملائكته يصلّون على المتسحّرين) رواه ابن حبّان
Hakika Allaah na Malaika wake wanawasalia wanaokula daku
Imepokewa na Ibn Hibaan
Kula daku ni mojawapo katika mambo yaliyotiliwa mkazo na Mtume Swalla Allaahu ‘alayh wasallam
Kwani ndani yake kuna baraka na kheri nyingi , pia ni kujipamba na tabia za Mtume wetu kwani jambo ambalo alikuwa akilifanya kila Ramadhaan. Tunapoamka kula daku ni fursa ambayo Allaah Subhaanahu Wata’ala hushuka mpaka mbingu ya dunia na kusubiri na kuwasikiliza wenye kuomba na wenye shida zao awakubalie.
Tuitumie fursa ya kula daku si kwa kula au kunywa pekee bali pia kwa kuomba maghfira kwa Mola wetu na kwa lengo la kufuata Sunna ya Mtume wetu Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam.