Ujumbe wa Manisipaliti ya Kiruna nchini Sweden umewasili Makunduchi kufuatilia maendeleo ya mradi wa pamoja kati ya Wadi za Makunduchi na Manisipaliti ya Kiruna. Ujumbe huo utakuwa nchini kwa siku nne. Miradi mingine ya maendeleo inayofikiriwa kufanywa baina ya pande hizi mbili ni mradi wa maji, kumbusho na mradi wa kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake hasa ubakaji. Katika picha kutoka kushoto walioketi ni ndugu P.G, Ove, Maria na afisa tawala mstaafu ndugu Abdallah Ali Kombo. Waliosimama kutoka kushoto ni ndugu Mohamed Simba na ndugu Keneth. Habari na picha kutoka ndugu Mohamed Muombwa ambaye ni mratibu wa ushirikiano baina ya Kiruna na Makunduchi
↧