Mwakilishi Mkaazi wa Shirika linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) Mariam Khan akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya DK. Mohd Saleh Jidawi vifaa mbali mbali vya mama wajawazito na watoto vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400 za Kitanzania. Hafla hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya waliohudhuri hafla ya kukabidhiwa vifaa vya Afya vilivyotolewa na Shirika linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA)