Mjengo ukiwa katika maandalizi, utakuwa na Gorofa 10, gorofa mbili ni sehemu ya maegesho ya Magari,kutakuwa na sehemu ya Benk.
Mjengo huu utakuwa na Ofisi za Mkuu wa Mkoa na sehemu nyegine kwa ajili ya Biashara na gorofa mbili sehemu ya maegesho ya magari.Litakuwa na gorofa 10.
AFISA Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg, Ayuob Mohammed na Mwakilishi wa Kampuni ya Ex Investments Switzerland Ndg. Razvan Pintilie, wakisaini makubaliano ya awali ya Ujenzi wa Jengo la Kisasa la Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika eneo la Amaan Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Jumba la Wananchi Forodhani
Afisa Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg. Ayuob Mohammed, akikamilisha taratibu za utiaji wa saini ya makubaliano ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kutakuwa na sehemu nyegini kwa ajili ya kukodisha na biashara.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Zanzibar Joseph Meza, akizungumza katika hafla hiyo ya Utilianaji wa saini ya makubaliano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kampuni ya Ex Investments Switzerland, itakayojenga jengo hilo.
Afisa Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg. Ayoub Mohammed, akitowa maelezo ya Jengo hilo kuelezea, baada ya utilianaji wa saini hiyo uliofanyika katika ukumbi wa jengo laWananchi Forodhani Zanzibar.
Afisa Tawala akizungumza na kutowa ufafanuzi wa ujenzi huo unaotarajiwa kuaza baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria baina ya pande zote mbili.
Chief Operations Officer wa kampuni ya Ex Investments. Ndg. Razvan Pintilie, akizungumza baada ya kukamilisha utiaji wa saini hiyo ya kujenga jengo la kisasa la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika eneo la Amaan
Viongozi wa Osifi ya Mkuu wa Mkoa wakifuatilia utiaji wa saini hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya utilianaji wa saini ya ujenzi wa Jengo la Kisasa la Gorofa 10 kwa ajili ya Ofisi yaMkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.