Ile sintofahamu iliyoibuka asubuhi wakati wa mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum mjini Dodoma imekwisha na sasa Wajumbe wanaendelea kujadili kifungu kimoja baada ya kingine kwa amani, maelewano na busara.
Mwenyekiti wa muda Mhe Pandu Ameir Kificho alianza kuwatangazia wajumbe kwamba Wajumbe Mhe Christopher Ole Sendeka na Mhe
Abubakar Khamis Bakari wamemaliza tofauti zao na wote wawili wamerudi Bungeni wakiwa hawana kinyongo na kwamba mshikemshike wa asubuhi ulikuwa ni moja ya changamoto za mijadala kama hiyo.
Mhe Kificho pia aliwakaribisha wajumbe Mhe Profesa Mark Mwandosya na Mhe. James Mbatia kusema machache kabla kuanza mjadala rasmi. Nao bila ajizi na kwa utulivu na maneno ya busara waliwataka wajumbe kukubali yaliyopita si ndwele na wagagnge yajayo.
Mhe Mbatia alimnukuu mmoja wa wajumbe wa kamati kama hiyo ya Ufaransa kwa kusema kuwa maridhiano na busara ndivyo viliwezesha nchi hiyo kujadili na hatimaye kuapata katiba yake.
Mhe Profesa Mwandosya alionesha imani kwa wajumbe wote kuwa na uwezo wa kuhitimisha kazi waliyotumwa na wananchi kwa maridhiano na kwa muda uliowekwa na kuokoa gharama.
"Niwahakikishie wananchi wa Tanzania kwamba hii kazi mliyotutuma tutaifanya na kuikamilisha kama ilivyokusudiwa", alkisema huku akishangiliwa.
Hivyo basi, hivi sasa mjadala unaendelea na wajumbe wamekubaliana mjadala huo wa kupitia Rasimu ya Kanuni zitakazotumika katika Bunge Maalum la Katiba unaendelea bila kelele wala mikwaruzo.
Baadhi wa wajumbe maalum wa katiba wakibadilishana Mawazo Nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Semina ya ya uundwaji wa kanuni zitakazoongoza bunge maalum la katiba kuahirishwa leo mjini Dodoma.