Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mke wa Rais wa Zanzibar Adhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea Watoto na Wanawake na Kutoa Msaada wa Mabati kwa Jengo la Wanawake la Kupumzikia.

$
0
0
Jengo la kupumzikia Wanawake wakati wakiwasubiri Wazazi wanaowaleta hospitalini hapo kujifungua katika Hospitali ya Kivenge Wilaya ya Kaskazini Unguja lililojengwa na Mwakilishi wa Mkwajuni Mhe. Mbarouk Mtando na nguvu za Wananchi wa Mkwajuni.hadi kufikia hatua hiyo na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, Mama Asha Balozi na Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM kuchangia mabati kwa ajili ya kuezeka jengo hilo, lilioko katika viwanja vya hospitali ya Kivunge. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi mabati Katibu wa CCM tawi la mkwajuni Juma Machano,wakishuhudia Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif na Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Wu Yan.ikiwa ni kusadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani.   
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimia Watoto mapacha wenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitano Najma Khamis na Mudat Khamis, wakiwa wamelazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Kivunge Mkoa waKaskazini Unguja , alipotembelea hospitali hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani,huadhimishwa kila ifikapo 8, March.  

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwasalimia Watoto mapacha wenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitano Najma Khamis na Mudat Khamis, wakiwa wamelazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Kivunge Mkoa waKaskazini Unguja , alipotembelea hospitali hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani,huadhimishwa kila ifikapo 8, March.  
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwa na mtoto aliyelazwa katika waodi ya watoto katika hospitali ya Kivunge, Mtoto Walid akiwa na mama yake Sikudhani Mustafa.

Mke waRais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitembelea Wodi ya Watoto na Wanawake katika hospitali ya Kivunge ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Jidawi akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Ujumbe wake wa Wake wa Viongozi wa CCM, walipofika katika hospitali ya Kivunge kutowa msaada wao kwa Jengo la Kupumzikia Wanawake wanaofika katika hospitali hiyo kuwaleta Wazazi kujifungua. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akihutubia Wanawake wa Mkwajuni wakati alipofika katika hospitali ya Kivunge kukabidhi mabati na kutembelea wodi ya Watoto na Wanawake ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali ya kivunge Wilaya ya Kaskazini Unguja.
Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Wanawake wa Mkwajuni Wilaya ya Kaskazuni Unguja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Jidawi akizungumza katika hafla hiyo. 
Mwananchi wa Mkwajuni Mwalim Faida akisoma risala ya Wananchi wa Mkwajuni wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya hospitali ya Kivunge.
Wanawake wa Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini Unguja wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia katika viwanja vya hospitali ya kivunge baada ya kukabidhi mabati kwa ajili ya jengo la Wanawake la kupumzikia na kuadhimisha Siku ya Wanaake Duniani.
Daktari Mkuu wa Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini Unguja Dkt. Khamis Hamad, akitowa shukrani wakati wa hafla hiyo. 




Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles