Afisa wa Tamwa Zanzibar Bi. Shekha Dau akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uzini wakati wa kuhamasisha Watoto waliotoroka Skuli kurudi skuli na kuendelea na masomo yao, ili kuachana na Ajira za Utotoni za Ajira.
Kiongozi wa Wazazi wa watoto ambao wametoroka skuli kwa kipindi kirefu na kushughulika na Ajira, wengi wao wamejitokeza kurudi skuli baada ya kupata elimu kupitia Mradi huu, wa Save tha Children. ulinaosimamiwa na TAMWA.
Mwandishi wa habari wa Redio Zenj FM Grace Kihondo, akimuhoji mmoja wa Mwanafunzi aliyerudi Skulikuendelea na masomo Hussein Yussuf (15) wa skuli ya Uzini ambae alirejeshwa skuli baada ya kutoroka na mradi wa kupambana na ajira za watoto Save the Children unaosimamiwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) akizungumza na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari baada ya kufanya ziara katika skuli hiyo kuangalia maendeleo ya watoto hao.
Mwandishi wa habari akiwahuji Wazee wa Watoto wa Kijiji cha Uzini ambao watoto wao tayari wamesharudi Skuli kuendelea na masomoyao baada ya kutoroka skuli kwa muda mrefu.