Na Miza Othman-Maelezo Zanzibar 27/ 3 /2014
Wizara ya Kilimo na Uvuvi Zanzibar Imeishukuru Serikali ya Japan kwa kuamuwa kuwajengea Soko la kisasa kwa lengo la kuimarisha na kuleta maendeleo hapa Zanzibar
Mkataba huo umetiwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya KilImo na Uvuvi Dr. Kassim Gharib pamoja na Meneja wa Fisheries Engineers Company Of Japan, Tadashi Ogawa huko Afisini kwake Maruhubi Mjini Zanzibar ikiwa ni njia moja ya kuleta ushirikiano.
Amesema huu ni wakati muwafaka kwa kujitokeza Meneja huyo kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika ambalo litakaloweza kuhifadhi samaki wengi wanaovuliwa hapa Zanzibar.
Aidha Dr. Kassim amesema hii ni njia ya kuiimarisha Serikali na kuwaletea maendeleo Wavuvi katika ufanyaji wakazi zao hasa kwa kipindi kigumu walichonacho.
Hata hivyo amesema kuwa faraja hiyo haitowanufaisha wavuvi tu bali na Wananchi kwa ujumla hasa wakati wanapohitaji kitoweo cha haraka katika Mji wao wa Zanzibar.
Vilevile amesema hadi hivi sasa bado hajapatikana Mkandarasi atakaeweza kusimamia soko hilo lakini endapo ikiwa tayari itatangazwa tenda na kuweza kupatikana kwa haraka.
Amewashauri wananchi wanaolitumia soko hilo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na kwa lengo la kuwaletea faraja soko hilo.
Dr. Kassim Gharib amesema katika ujenzi wa Soko hilo litagharimu Sh. Bilion 14 hadi kumaliza kwake.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR