Ramani ya Mradi wa ujenzi wa barabara mpya kisiwani Pemba zilizozinduliwa leo na Rais wa Zanzibar Dkt. Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Maofisa wa Ubalozi wa marekani baada ya kuwasili Mtambwe kwa ufunguzi wa barabara tano zilizojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Virginia Blaser, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Barabara mpya tano kisiwani Pemba zenye urefu wa KM 35. uzinduzi huo umefanyika katika moja ya barabara hizo ya Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Virginia Blaser, wakiondoa kipazia kuashiria uzinduzi huo.wa Barabara mpya tano kisiwani Pemba zenye urefu wa KM 35. uzinduzi huo umefanyika katika moja ya barabara hizo ya Mtambwe Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akipanda mti wa historia wakati wa uzinduzi wa barabara ya Mtambwe Pemba.
Kaimu Balozi wa Marekani Nchinin Tanzania akipanda mti wa historia wakati wa uzinduzi wa barabara ya Mtambwe Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, na Kaimu Balozi wa Marekani Bi.Virginia Blaser, wakibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa huo.wa Barabara mpya tano kisiwani Pemba zenye urefu wa KM 35. uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa gombani Pemba.
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bi. Virginia Blaser, akihutubia wakati wa uzinduzi huo wa barabara katika uwanja wa gombani Pemba.
Waziri wa Wizara ya Mawasilianona Miundombinu Mhe. Rashid Seif, akizungumza wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika uwanja wa Gombani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MCAT, Ndg. Bernad Mchomvu,akitowa risala ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara tano kisiwani Pemba, wakati wauzinduzi wa barabara hiyo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu Dkt. Juma Malik Akili , akitowa maelezo ya ujenzi wa barabara hizo zenye urefu wa Kilomita 35.
Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika uwanja wa Gombani.Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati wa uzinduzi wa barabara hizo.
Wanafunzi wakisoma Utenzi wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Barabara Tano Kisiwani Pemba Wilaya ya Kusini Pemba.uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa Gombani Wilaya ya ChakeChake.