Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt Yamalizika na Timu ya KMKM Yatowa Ubingwa huo kwa mwaka 2014/2015.

$
0
0
Meneja Masoko wa Grand Malt Ndg Fimbo Butallah kushoto na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar BMZ Khamis Said, wakiwa katika maongezi  katika hafla ya tafrija ya kutowa zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt, iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar. 
Makamu Mwenyekiti wa BMZ Khamis Said, kushoto akimkabidhi Cheki Mwenyekiti wa timu ya KMKM Dng. Khatib Khamis Mwadin, ilioweza kutetea Ubingwa wao kwa kuifunga timu ya Chipukizi katika mchezo wa mwisho uliofanyika katika uwanja wa Gombani Pemba.imeshinda 3-2.
Makamu Mwenyekiti wa BMZ Khamis Said, kushoto akimkabidhi Cheki ya shilingi milioni Tano, Kiongozi wa timu ya Polisi   baada ya kushika nafasi ya Pili ya Ligi ya Zanzibar Grand Malt,baada ya kuwekewa ngumu na timu ya Jamuhuri katika mchezo wake wa mwisho uliofanyika uwanja wa Amaan kwa kufungwa bao 1--0. 
Makamu Mwenyekiti wa BMZ Khamis Said, kushoto akimkabidhi Cheki ya shilingi milioni moja Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Grand Malt, Ali Bushiri wa Timu ya KMKM. 
Refalii Bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt akipokea zawadi yake Cheki ya shilingi milioni moja.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Maichezo Zanzibar (BMZ) Khamis Said, kushoto akizungumza katika tafrija hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt, iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar.mkabidhi Cheki 
Meneja Masoko wa Grand Malt Ndg. Fimbo Butallah akizungumza katika hafla hiyo na kutowa kwa pongezi kwa Uongozi wa ZAF kwa uishirikiano wao na kuendesha Ligi bila ya mizozo hadi kufikia kwa tamati hiyo iliozikutanisha timu nne kumalizia Ligi hiyo na mbili kuwania Ubingwa nazo ni timu ya Polisi na KMKM .


Makamu Mwenyekiti wa ZFA akizungumza katika haflahiyo ya tafrija ya kuwazawadia zawadi washindi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt na kuitaka Kampuni ya Grand Malt kuongeza Ufadhili wa ligi hiyo kwa ligi ya mwakani na kuitaka kuifadhili timu ya Taifa ya Zanzibar inaposhiriki michuano ya Kimataifa.
Viongozi wa Timu washiriki wa Ligi Kuu ya Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi.
Wachezaji na Viongozi wa timu wakiwa katika tafrija hiyo ya kukabidhi zaadi kwa Washindi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt.
Wapata msosi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

Mamaku Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar BZM Ndg. Khamis Said akimkabidhi Kombe la Ubingwa Kiongozi wa timu ya KMKM baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa Ligi hiyo kwa kuifunga timu ya Chipukizi 3-2 mchezo uliofanyika uwanja wa gombani Pemba.
Meneja Masoko wa Grand Malt Ndg Fimbo Butallah akimkabidhi  Cheki ya mfano ya shilingi milioni kumi ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt
Viongozi wa Timu ya KMKM wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Grand Malt na ZFA wakiwa na kombe laola Ubingwa , baada ya kukabidhiwa kwa kulitowa Kombe hilo kwa kuifunga timu ya Chipukizi wakiwa Pemba katika uwanja wa Gombani.
Rais wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA Ndg Ravia Idarus akimkabidhi mfano wa cheki ya shilingi milioni tano nahodha wa timu ya Polisi Ndg Adam Azingwa
Kiongozi wa Timu ya Polisi akipeana mikono na Viongozi wa ZFAna wa Grand Malt baada ya kukabidhiwa medeli zao za mshindi wa Pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt.

Mabingwa wa Pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt timu ya Polisi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa ZFA na Grand Malt wakiwa ma mfano wa cheki ya shilingi Milioni Tano.
Wachezaji wa timu ya Jamuhuri wakisalimiana na Viongozi wa ZFA na waGrand Malt baada ya mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Jamuhuri kilichotoa kipigo kwa timu ya Polisi kwa kuwanyima Ubingwa kwa kuwafunga Bao moja katika mchezo wao wa mwisho na kushuka daraja Ligi Kuu ya Zanzibar katika mchezo huo timu ya Jamuhuri ilionyesha mchezo wa hali ya juu dhidi ya timu ya Polisi na kuibuka na ushindi huo.

Maafande wakiwa hawaamini macho yao kutokana na matokeo ya mchezo huo kwao nin kama Fainal wakishindi wangekuwa mabingwa kwa mwaka huo lakini bahati haikuwa kwao na hatimai kukubali kipigo cha bao 1--0.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>