Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilaya ya Arusha, kimeanzisha kampeni ya kufuatilia kazi na miradi inayotekelezwa na madiwani wake, lakini pia kutafuta madiwani vivuli, kwenye kata ambazo
zina madiwani wa CCM.
Hayo yalielezwa mapema jana na Katibu wa wilaya wa Chadema,Martini Sarungi, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusiana na miradi inayoendelea kutekelezwa chini madiwani wa chama hicho kwa wilaya ya Arusha.
Alisema lengo la kuwafuatilia madiwani hao ni kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizitoa wakati wa kampeni, ili kuziondoa.
Alisema mbali na kutekeleza ahadi hizo, pia watawajulisha wananchi kinachoendelea kwenye kata na miradi ambayo imetekelezwa na madiwani wa Chadema.
Alisema kwenye kila mtaa kutakuwa na madiwani hata kama kata inaongozwa na CCM au TLP ambapo kwa sasa kwenye kata za
viongozi hao zote, kutakuwa na walezi ambao wanalenga kuwasaidia wananchi.