Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
: { أفضل الصلاة بعد الفريضة صلاة
الليل } [رواه مسلم].
'Sala iliyo bora baada ya sala za fardhi ni Sala inayosaliwa usiku'
Imepokewa na Muslim
Tunaingia katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhaan kumi lililo bora kabisa ambapo ndani yake tunatakiwa kukithirisha ibada kuliko tulizokuwa tukizifanya katika muda mwengine na ndani yake kuna usiku ulio bora katika dunia hii usiku wa Laylatul Qadr ambao tumetakiwa tuutafute kwa kufanya ibada kwa wingi..
Tuitumie fursa hii kwa kufanya ibada katika wakati ambao Allaah Subhaanahu Wata’ala huthibitisha imani ya mja wake anaemtii na kumuabudu kikweli ( wakati wa usiku mkubwa wakati watu wengine wamelala).
Aamiyn