Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dkt. Shein Asisitiza Vipaumbele katika Kupanga Bajeti za Wizara na Idara za Serekali.

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                             30-4- 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza umuhimu kwa wizara kutambua vipaumbele katika kupanga bajeti ili kupata matokeo mazuri.
Alibainisha kuwa umuhimu huo wa wizara kutambua vipaumbele usaidie Wizara hizo kuainisha na kuteua miradi michache muhimu katika Mpangokazi wa mwaka wa fedha ili iweze kutekelezwa kwa mujibu wa bajeti iliyopangwa.
Dk. Shein alisema hayo jana wakati akifunga mjadala wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais katika mfululizo wa vikao vinavyoendelea vya kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi za Serikali kwa kipindi cha Julai 2013 na Machi 2014.
Alifafanua kuwa malengo ya wizara ndio yanayopanga bajeti na kukumbusha kuwa mipango mizuri ni ile inayozingatia vipaumbele pamoja na matumizi mazuri ya rasilimali hivyo suala la kupangaji vyema wa malengo halina budi kuzingatiwa wakati wote wizara na Idara za Serikali zinapopanga bajeti zao.
Mhe Rais aliipongeza Ofisi ya Makamu wa Pili kwa Rais kwa kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio katika kipindi kilichopita ambapo Ofisi hiyo iliweza kufikia malengo yake.
Hata hivyo, alitoa wito kwa Ofisi hiyo kutoa elimu zaidi kuhusu Mradi wa TASAF Awamu ya Tatu ili wananchi waweze kuufahamu vyema.
Mapema akitoa maelezo ya utangulizi katika kikao hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alisema katika kipindi husika Ofisi hiyo imeweza kutekeleza majukumu yake kwa wastani wa asilimia 79.

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa kushirikiana na Tume ya Mipango na Tume Sayansi na Tekinolojia Tanzania (COSTESH) ilishiriki katika kuandaa vipaumbele vya utafiti.
Halikadhalika alieleza Ofisi hiyo imetoa elimu ya kukabiliana na maafa na kuandaa Mpango wa Wilaya wa Kukabiliana na Maafa pamoja na kuandaa Mazoezi ya Majaribio(simulation excercises) juu ya namna ya kukabiliana  na maafa ikiwemo mafuriko na ajali za baharini kwa kushirikiana na Shirika la  Chakula Ulimwenguni. 
Wakati huo huo Serikali imesema jumla shilingi milioni 466.2 zimelipwa kwa kaya masikini Unguja na Pemba katika kipindi cha Januari na Aprili mwaka huu chini ya Mradi wa TASAF Awamu ya Tatu.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Katibu Mkuu Dk. Khalid Salum Mohamed alieleza kuwa kati ya fedha hizo shilingi milioni 138.2 zimelipwa kwa kaya masikini ya 4054 kisiwani Pemba kati ya mwezi Januari na Februari na shilingi milioni 155.1 zililipwa kwa kaya masikini 4084 kisiwani humo kati ya mwezi Machi na Aprili 2014.
Katika taarifa hiyo, Dk. Khalid alisema kwa upande wa Unguja jumla ya Kaya 2,674 zimepokea msaada kama huo kwa awamu mbili ambapo jumla shilingi milioni 172.8 zilitolewa.
Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa Mpango huo wa Kunusuru Kaya Masikini ambao lengo lake ni kuzisaidia kaya hizo kumudu gharama za elimu, afya na kuongeza kipato umeonesha mafanikio makubwa ambapo kumekuwepo na ongezeko la watoto wanaohudhuria masomo kutoka kaya zinazopatiwa msaada huo.
Dk. Khalid aliongeza kuwa kumekuwa pia na ongezeko la mahudhurio katika kiliniki kwa mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5.
Kuhusu utambuzi na uteuzi wa kaya masikini alieleza kuwa hufanywa kwa kushirikisha wananchi wa jamii husika na kumekuwepo na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na maafisa wa mfuko huo.
Chini ya Mpango huo kaya zinazopata msaada huo ambao zina watoto wenye umri wa kwenda skuli wanapaswa kuwasimamia kuhudhuria masomo na kwa kaya zenye wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wanapaswa kwenda kliniki kupata matibabu na ushauri wa daktari kama mwongozo wa afya ya mama na mtoto unavyoelekeza. 
Msaada unaotolewa kwa kaya hizo ni shilingi 34,000 kila baada ya miezi miwili kwa kaya zenye watoto na wajawazito na shilingi 17,000 kwa kaya nyingine.  

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>