MRATIBU wa Idara ya Makumbusho na mambo ya kale Pemba Khamis Ali Juma akiwaelezea wanafunzi wa skuli za sekondari za mkoa wa kusini Pemba, historia ya msikiti aliokuwa akitumia mtawala Haroun eneo la Chwaka Tumbe, zaidi ya miaka 200 iliopita wakati wanafunzi hao walipokuwa na ziara maalumu ilioandaliwa na Kamisheni ya Utalii, ili kueneza sera ya utalii kwa wote, (picha na Haji Nassor, Pemba)
MWALIMU kutoka skuli ya sekondari ya Uweleni Mkoani, Khamis Mohamed Ussi, akichangia jambo kwenye mkutano uliohusishwa wanafunzi na walimu uliofanyika hoteli ya Misali sun seat beach, ambao ulikuwa na lengo la kuwaelezea umuhimu wa utalii kwa wote (picha na Haji Nassor, Pemba)