Na Miza Othaman – Maelezo
Wizara ya kilimo na Maliasili Zanzibar imesema inajukumu la kusimamia maendeleo ya uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara katika upatikanaji na usambazaji wa huduma za pembejeo na dhana za kilimo kwa wakulima, uhifadhi na ukaguzi wa mazao na kutowa mafunzo kwa wazalishaji.
Hayo yameelezwa huko Baraza la Wakilishi na kaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili Ramadhani Abdalla Shabani wakati alipokuwa akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/2014 barazani hapo.
Amesema katika kufikia azma hiyo wizara itazia uimarishaji wa mimea kwa kuitia dawa ambapo jumla ya lita 500 za dawa za asili
zimetayarishwa kwa kuulia wadudu waharibifu wa mimea.
zimetayarishwa kwa kuulia wadudu waharibifu wa mimea.
“ Tutatia dawa mimea lakini pia Tutawelimisha wakulima 1500,juu ya mbinu zakilimo bora pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi
kwamabibi/mwabwanashamba 95 juu ya mbinubora za kilimo,”alisema waziri.
kwamabibi/mwabwanashamba 95 juu ya mbinubora za kilimo,”alisema waziri.
Aidha ameeleza kua watazalisha Tani nane za mbegu ya mahindi , tani mbili za mbegu yam tama na 570 za mbegu ya mpunga ikiwemo NERICA.
Waziri huyo alizieleza kua pamoja na hayo wizara inakabiliwa na changamoto ambazo ni pamoja na ongezeko kubwa la mahitaji ya mazao ya maliasili kuliko uwezo wa udhalilishaji, matumizi mabaya ya dhana yanayopelekea uharibifu wa mazingira ikiwemo misumeno ya moto.
Alitaja nyengine ni uhaba wa uchakavu wa Matrekta, uvamizi wa maeneo ya kilimo kwaajili ya makaazi, uchimbaji wa mchanga na wizi wa mazao wa kilimo wa maliasili.
Pia alisema kuwa Wizara hiyo inakabiliwa uchache wa mabwanashamba, mabadiliko ya hali ya hewa na mvua zisizo tabirika, na ushiriki kuwa mdogo waskta binafsi katika kuwekeza maendeleo ya kilimo.
Akieleza mafanikio alisema jumla ya tani 535 za mbegu ya mpunga zimesambazwa kwa wakulima ( sawa na asilimia 94 ya lengo), kati ya mbegu hizo tani 300 zimenunuliwa kutoka T anzania Bara na tani 235 zimenunuliwa kupitia wakulima wa mikataba Zanzibar.
Wizara hiyo imepanga kutekeleza malengo yake kutimiza dira 2020 kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUZA II),malengo ya milenia MDGs na mikakati ya kisekta pamoja na mpango wa mageuzi ya sekta ya kilimo (ATI)
Aidha kuimarisha uzalishaji wa zao la karafuu, mpunga, utowaji wa huduma za matrekta, pembejeo za kilimo, kuzalisha matunda,mboga mboga, asali, utalii wa kimaumbile, pamoja na kuhamasisha ushirika wa vijana katika uzalishaji kilimo cha biashara.
Wizara hiyo iliomba kuidhinishiwa 30,320,998,000 kwa kazi za kawaida na kimaedeleo.