Wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiimba wimbo Maalum wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha { AICC }.
Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha { AICC }.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyeta wa Kenya akihutubia Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha.Wa mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta.
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini baadhi ya hati za makubaliano ya Jumuiya hiyo.
Majaji wapya walioapishwa kushika nyadhifa mbali mbali kwenye Mkutano wa 12 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.Kutoka Kushoto ni Jaji Edward Mtakangwa, Dr. Anon Regerwa na Jaji Fakih Jundu.
Wakuu waJumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha Tanzania.Kutoka Kushoto waliokaa vitini ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza Majaji wapya wa Mahkama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki waliokula kiapo kwenye Mkutano wa 12 wa kuitumikia Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.(Picha na Hassan Issa OMPR)