Mfanyakazi wa Jumuiya ya ZAYEDESA akitowa ushauri nasaha kwa Vijana hao waliofika kuangalia Afya zao, katika viwanja vya mpira lumumba. Jumla ya Vijana 143 wamejitokeza kupima afya zao.
Vijana wakiwa katika foleni ya kusubiri kucheki afya zao katika zoezi la Jumuiya ya ZAYADESA kuhamasisha Vijana kuacha Matumizi ya Dawa za Kulevya na Maambukizo ya VVU kwa Vijana.
Vijana wakiitikia mwito kwa kujali Afya zao na kujitokeza katika zoezi la kupima afya kwa Vijana lililotolewa na Jumuiya ya ZAYEDESA katika viwanja vya lumumba wakati wa mchezo wa mpira wa Vijana wa Maskani ya Rangers, wa Timu mbili za Vijana walioowa na Wasioowa, Jumla ya Vijana 143 wamejitokeza kupima afya zao.katika zoezi hilo.