Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee akizungumza na Waandishi wa habari Muelekeo wa Bajeti ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mwaka wa Fedha 2013 - 2014, iliokadiriwa kutumika ni Bilioni 705.1, mkutano huo na waandishi umefanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha Vuga..na kupewa Vipaumbeli Sekta za Miundombinu, Afya, Elimu na Miundombinu ya Maji Safi na Salama na kuongezeka kwa kipato kwa kila Mwanchi kwa mwaka huu wa Fedha.
Waziri wa Fedha Mhe Omarb Yussuf Mzee akisisitiza jambo wakati akitowa na kusoma Muelekeo wa Bajeti kwa Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar.
Mambo Safi kwa Mwaka huu wa Fedha
Sekta ya Uchumi imeongeza katika Kilimo na Utalii kwa Mwaka huu wa Fedha Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yussuf Mzee akiwaambia waandishi wa habari wakati akitowa Muelekeo wa Bajeti ya Serekali ya Mapinduzi Zanzinzibar inayotarajiwa kusomwa mwazo wa mwezi huu katika Mkutano wa Bajeti katika Ukumbi wa Barazala Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Watendaji Wakuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Fedha akisoma Muelekeo wa Bajeti ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, leo asubuhi Ofisini Kwake Vuga.
Maofisa wa Wizara ya Fedha wakifuatilia hutuba ya Muelekeo wa Bajeti ikitolewa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee. kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.
Waandishi wakiwa makini kuchukua figa za hesabu zikitolewa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee Ofisini kwake Vuga.ili kuwajuvya Wananchi Bajeti yao kwa mwaka wa Fedha 2013 / 2014