Viongozi wa meza kuu kutoka kulia Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wakulima Zanzibar Ndg Abdaalah Abass, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg, Juma Ameir Hafidh, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi,Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Abubakar Khamis Bakar. na Mwenyekiti wa ANGOZA Bi. Asha Aboud. Mzee.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg, Juma Ameir Hafidh, akitowa maelezo ya Mradi wa kusaidia Sekta Binafsi katika mradi huo unaosaidiwa na Umoja wa Ulaya, makubalianohayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar, kushoto Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis Bakar.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, akizungumza katika hafla hiyo ya makubaliano ya utilianaji wa saini na Serekali ya Mapinduzi Zanzibar na EU. katika Miradi ya Taasisi Binafsi NGOs.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Abubakar Khamis Bakar, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini na Umoja wa Ulaya katika kusaidia Taasisi Binafsi NGOs Zanzibar.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.kushoto Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, na kulia Mwenyekiti wa NGOs ya ANGOZA Bi Asha Aboud Mzee.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg.Juma Ameir Hafidh na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, wakitiliana saini ya makubaliano ya kusaidia Mradi wa Taasisi Binafsi NGOs, anayeshuhudia ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Abubakar Khamis Bakar, ambaye Taasisi hizoziko chini ya Wizara yake. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg.Juma Ameir Hafidh na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, wakibadilishana nyaraka za makubaliano baada ya kusainiwa na pande zote mbili za SMZ na EU.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wakulima Zanzibar Ndg. Abdallah Abass, akitowa shukrani kwa msaada huo wa kunufaisha Sekta Binafsi katika kuendeleza NGOs za Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ANGOZA Zanzibar Bi Asha Aboud Mzee, akitowa shukrani kwa msaada huo kwa ajili ya NGOs kuziwezesha katika miradi yake kuwaendeleza Vijana Zanzibar katika NGOs zao.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini na Umoja wa Ulaya.
Viongo wa Taasisi Binafsi Zanzibar NGOs wakifuatilia hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar na Umoja wa Ulaya (EU) katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.