Kutoka kwa ‘Abdullah Ibn ‘Abbass, Allah awawie radhi yeye na baba yake, amesema:-
" فرض رسول الله صلى الله عليه وسلم زكاة الفطر طهرة للصائم من اللغو والرفث وطعمة
للمساكين من أداها قبل الصلاة فهي زكاة مقبولة ومن أداها بعد الصلاة فهي صدقة
من الصدقات
“Mtume Swalla Allahu ‘alayhi wasallam amefaradhisha Zakaatul Fitr kwa wale waliofunga ili iwatoharishe na yale mambo ya kipumbavu na maneno machafu (waliokuwa wakifanya na kuongea wakati wa kufunga) na pia kwa wale maskini wapate kulishwa. Yeyote mwenye kuitoa kabla ya sala basi hiyo ni Zakaah iliokubalika , na mwenye kuitoa baada ya sala itahesabika kama ni sadaqa miongoni mwa sadaqa”
Imepokewa na Abu Daaud, Ibnu Majah na Ad daaru Qutniy
Imepokewa na Imaam Annawawiy kwamba Wakii bin Al Jaraah amesema:
زَكَاةُ الْفِطْرِ لِشَهْرِ رَمَضَانَ كَسَجْدَتِي السَّهْوِ لِلصَّلاةِ تَجْبُرُ نُقْصَانَ الصَّوْمِ كَمَا يَجْبُرُ السُّجُودُ نُقْصَانَ الصَّلاةِ .،
Mfano wa Zakaatul Fitr kwa Ramadhaan ni sawa na mfano wa Sijdatu Ssahw kwa Sala. Zakaatul fitr huikamilisha funga kama Sijdatus Sahw inavyoikamilisha Sala kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.