Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hadithi ya leo (17)

$
0
0

Imepokewa na ‘Abdullah Ibn  ‘Umar, Allaah awawie radhi (yeye na baba yake), kwamba  Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema :
" فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ
عَلَى الْعَبْدِ وَالْحُرِّ وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى وَالصَّغِيرِ وَالْكَبِيرِ مِنْ الْمُسْلِمِينَ وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ
النَّاسِ إِلَى الصَّلاةِ

Amefaradhisha Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam Zakaatul Fitri katika Ramadhaan kwa kila mtu miongoni mwa waislamu huru na mtumwa, mwanamke na mwanamme, mdogo na mkubwa kutoa  pishi moja ya tende au pishi moja ya uwele, Na akaamrisha kutolewa kabla ya watu kutoka kwenda kusali (Eid)

                                                 Imepokewa na Bukhaari

Kwa mujibu wa hadithi hii, Zakaatul Fitr itabidi itolewe kwa Waislamu wa aina zote bila ya kujali hali, jinsi na mazingira ya Muislamu husika pindi uwezo ukiruhusu na Muislamu kuushuhudia mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
Uwezo unaokusudiwa ni kwa Muislamu kuweza kuwa na vya kujitosheleza katika siku ya eid na kisha kuwa na cha ziada.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>