Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Amour, akielezea huduma zinazopatika kupitia kwa Benki ya PBZ Islamic,wakati wa mkutano huo na kueleza huduma hizozinazopatika kupitia Islamic Benk ni pamoja na mikopo ya Nyumba, Magari, Mashine za Viwandani, Ukodishwaji wa Nyumba na mikopo mengine kupitia njia hiyo, Benki hulipa pesa kwa muhusika na kuchukua Fedha hizo kwa mteja wake kidogokidogo kila mwezi, amewataka Wananchi kujiunga na kufungua Akantu katika pbz Islamic ili kunafaika na huduma hiyo inayotolewa kupitia Islamic Benki.
Mjumbe wa Bodi ya PBZ Dkt Hafidh, akiongoza mkutano huo wa kutowa Elimu ya huduma zinazotolewa na Benk ya Kiislam, na faifda zake kwa Wateja wa Benk hiyo.
Prof Dkt. Monzer Kahf akizungumza katika mkutano huo na Wafanyabiashara na Mashekh, katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
Shekh Ahmeid Jabir, akitafsiri na kutowa maelezo ya ufafanuzi wa Benki ya Kiislam wakati wa Mkutano huo wa Prof. Dkt Monzer Kahf, uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar mkutano huo umeandaliwa na PBZ Islamic.
Mashekh na Wafanyabiashara Zanzibar wakimsikiliza Prof Dkt Monzer Kahf, akizungumzia Benki ya Kiislam inavoendeshwa kwa wateja wake na hutowa huduma ya Mikopo kwa kuchukuwa Bidhaa, kwa wateja wake na sio kukopeshwa Fedha taslim, na kutowa faida za Benki hiyo kwa Wateja wake jinsi wanavyofaidika kwao na kuongeza mapatokwao kupitia Benki ya Kiislam.