Hichi ndicho kikosi cha Kundemba FC ambacho kimefanikiwa kupanda Daraja la pili kikiongozwa na Kocha Ahmada ( Bwan noma) aliyesimama kushoto.
.
Kundemba FC ya miaka ya tisini iliyokuwa chini ya Kocha Seif Mbuzi (aliyesimama kushoto)ambayo iliweza kuzitikisa timu kubwa enzi hizo.
Kundemba FC ya miaka themanini
Kundemba FC ni timu kongwe inayoendeshwa na nguvu za wanakundemba wenyewe ambayo kwa sasa iko chini ya kocha Ahmada (Bwan nnoma) imefanikiwa kupanda daraja la pili baada ya matokeo ya jana kati ya Union Rangers na Small Villa ambapo Union Rangers iliilaza Small Villa 3-2.
Kundemba FC imefanikiwa kupanda daraja baada ya kujikusanyia pointi 10 katika michezo mine iliyocheza mbapo imeshinda mitatu na kutoka sare mmoja.
katika kundi la Kundemba FC , matokeo ya mechi ya mwisho kati ya Kwa Alinato na ZMCL hayatowaathiri chochote kutoka na uwiano wa pointi ilizozipata.
Mechi za raundi ya tano na ya mwisho zitachezwa leo Jumamosi wakati mmoja katika viwanja tofauti vya Amani, Mao na Bomani ili kuepuka kupangwa matokeo.
Kundemba Fc sasa inajiandaa na kutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu baada ya kuingia nne bora ambazo inajumuika na timu za Magomeni na Sayari zilizofanikiwa kuingia katika kundi la pili katika ligi fupi ya timu nne.