Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi akifungua Mkutano wa siku mbili wa Jumuiya ya Africa Mashariki wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa kwa Mamlaka za udhibiti wa bidhaa hizo kwa Nchi wanachama.
Mrajis Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhani Othman Simai akijibu masuali aliyoulizwa na wajumbe wa Mkutano huo, (kushoto) Mwenyekiti wa Mkutano Dkt. Jamala Adam Taib.
Afisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bi. Hidaya Juma Hamad akielezea changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa kazi za Bodi hiyo, (kusho) ni Meneja Operesheni wa Mradi wa Usajili wa chakula na Dawa wa nchi za Afrika Mashariki Apolo Muhaiwira.
Mratibu wa Mradi wa Usajili wa Chakula na Dawa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. John Patrick (aliesimama) akitoa maelezo kuhusiana na Mradi huo katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dk. Mohd Saleh Jidawi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Africa Mashariki wa tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar.