Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifunguza majadiliano kuhusu mazingira yanayochangia kuendenea kwa vitendo vya kigaidi. majadiliano hayo yamefanyika siku ya Jumatano yakitangulia mkutano wa nne utakafanya tathmini kuhusu Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibidi Ugaidi. Katika salamu zake, Katibu Mkuu amesema hakuna sababu iwayo yoyote ile inayoweza kuhalalisha ugaidi. Kulia kwake ni Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw, John Ashe .
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu ukiongozwa na Naibu Waziri Silima walioketi nyuma ni Bw. Abdalla Khamis Afisa katika Uwakilishi wa Kudumu na Bw. David Hiza. Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi na Mratibu Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Mapambano dhidi ya Ugaidi.
Wajumbe ukumbini
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Pereira Silima ( Mb) akichangia majadiliano hayo. Naibu Waziri anaongoza ujumbe wa Tanzania. Katika mchango wake amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa vijana hasa wale wasiokuwa na ajira hawashawishiki kujiunga na uhafidhina na kwamba kutoka na changamoto mbalimbali zikiwamo za ukubwa wa mipaka baina ya nchi na nchi, tishio la ugaidi na uhafidhina kwa nchi za Afrika Mashariki ni kubwa.