Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba meja mstaafu Juma Kassim Tindwa, akizungumza katika hafla ya kukabidhi ujenzi wa jengo la kisasa la huduma kwa wateja la TTCL Pemba, ambapo mjenzi ni kampuni ya Ms Quality building Ltd, katikati ni afisa kutoka TTCL na wa mwisho ni mkuu wa wilaya ya Chakechake, Mwanajuma Majid Abdalla.
Afisa tawala wilaya ya Mkoani, Abdalla Salim akizungumza na masheha wa wilaya hiyo, hawapo pichani, wakati akifungua mafunzo ya kuwatambulisha wasaidizi wa sheria wa majimbo, kulia ni mwanasheri wa afisi ya mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, Matar Zahoro na katikati ni Mratibu wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar , tawi la Pemba Fatma Hemed Khamis, ambao ndio waandaji wa mafunzo hayo yaliofanyika skuli ya sekondari Uweleni.
Wanakikundi cha ususi wa mikoba, makawa, vipochi vya ukindu na upandaji miti, kilichopo shehia ya Changaweni wilaya ya Mkoani Pemba, ambao wengi wao ni walemavu, wakiwa katika kazi yao hiyo, ambapo mkoba mmoja wa kisasa wenye zipu huuzwa kati ya shilingi 15,000 hadi shilingi 12,000.
Sheha wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chake chake Pemba nd: Salim Ayuob akizungumza na wanajumuia ya ‘Matumaini mapya’ ya wanawake wenye ulemavu, waliopo Vumba shehiani humo, akifungua mafunzo ya siku kumi juu ya ufugaji bora, uwekaji kumbu kumbu na utunzaji fedha, mafunzo yaliofanyika skuli ya Vitongoji.
Mratibu wa mradi wa Usafi wa Mazingira kupitia Jumuia ya uhamasishaji juu ya utunzaji wa mazingira, kupiga vita madawa ya kulevya na maabukizi mapya ya Ukimwi ya Jimbo la Kojani, KOYMOCC, Nd:Hamad Hassan, akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu, yakiofanyika Kojani, katikati ni Afisatawala wa Wilaya ndogo ya Kojani Nd: Makame Khamis Makame , akifuatiwa na Mwenyekiti wa KOYMOCC Ali Hamad Mussa
Afisa tawala Wilaya ya Chakechake Rashid Hadidi Rashid, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo, wajumbe wa kamati tendaji wa jumuiya ya ‘TUMAINI JIPYA’ kisiwani Pemba, mafunzo yaliyofanyika Gombani Chakechake, kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo Nd:Ali Suleiman Khamis na kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya Nd: Tatu Abdalla Mselem.
Afisa mdhamini wa shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Pemba, Abdulmalik Mohamed Bakar, akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Jimbo la Chambani, unaoendeshwa na Jumuiya ya Kustawisha zao la Karafuu na viungo Pemba ‘JUKAVUPE’, kulia ni Kaimu Mweyekiti wa Jumuiya hiyo Ali Abdalla Said na kushoto ni Mratib wa mradi Omar Ali Kombo (Picha na Haji Nassor Pemba).