Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kikombe cha babu kiliua watu wengi, asema Waziri

$
0
0
Na Fatina Mathias, Dodoma
DAWA ya asili ya Mchungaji Ambilikile Mwasapila  wa Loliondo mkoani Arusha maarufu kama 'kikombe cha babu ' kilichoaminika kutibu ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa mengine sugu,hakikutibu na badala yake kiliua watu wengi zaidi waliokuwa  wameathirika na magonjwa mbali mbali ukiwemo Ukimwi,bunge limeelezwa.

Akiuliza wali la nyongeza jana bungeni mjini hapa,Mbunge wa Nzega, Khamis Kigwangala ( CCM) aliitaka serikali kueleza kama hatua zozote zilichukuliwa baada ya dawa hiyo kutoonesha matunda yaliyokusudiwa na badala yake kuua zaidi.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Afya, Dk.Stephen Kebwe, alisema hakuna ushahidi wowote ulioonesha wagonjwa waliokunywa kikombe cha babu walikufa kwa ajili hiyo.

Alisema kufuatia utafiti uliofanywa na kituo cha Utafiti cha Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ulionesha dawa hiyo haikuwa na madhara kwa
matumizi ya binadamu na kusema waliokufa,ilikuwa ni kutokana na magonjwa yaliyokuwa yakiwakabili.


Awali katika swali lake la msingi,Kigwangala aliitaka serikali kuruhusu hospitali zote kutibu wagonjwa hao ili kila mmoja atibiwe na daktari anayemtaka huku akisema kwa sasa  wananchi wana uelewa kuhusiana
na ugonjwa huo na madaktari wengi wanauelewa pia.

Pia alitaka kujua kwa nini dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARVs) hazipo kwenye hospitali zote hasa kwenye maduka ya dawa.

Akijibu hilo, Dk. Kebwe alisema, hadi kufikia Disemba 2013 ,hospitali zote na vituo vya afya na baadhi ya zahanati nchini zilikuwa zinatoa huduma ya

matunzo na tiba ikijumuisha dawa za kupunguza makali ya Virus vya Ukimwi kwa watu wanaosihi na VVU.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles