Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Mbarouk, akitowa Taarifa ya Serekali kuhusu Tukio la kumwagiwa Tindi Kali Watalii kutoka Uingereza na Watu wasiojulikana usiku wa jana katika maeneo ya shangani Mji Mkongwe wa Zanzibar, Serekali imelani kitendo hicho na kutoa Taarifa kwa Wananchi kushirikiana na Serekali kuwataja Watu waliohusika na tukio hilo.na kutoa Shilingi Milioni Kumi kwa mtu atakayetowa Taarifa hiyo kwa Serikali.
Waandishi wa habari wakuifuatilia maelezo ya Serekali kuhusiana na Tukio hilo.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Utalii Zanzibar ZATO Mr Abdulsamad Said Ahmeid, akilaani kitendo cha Watu wasiojulikana kuwamwagia Tindi Kali Watalii wakiwa katika matembezi yao katika mji mkongwe.Jumuiya hiyo imelaani kitendo hicho na kutowa kauli ya kulaani kwa hatua zote kuhusiana na kitendo hicho wakati wa kuzungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Zanzibar.