Na Abdi Suleiman, Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, amesema mikoa ya Pemba ni sehemu ya mikoa ya Tanzania, iliyofanya vizuri katika mradi wa TASAF awamu ya pili na kubahatiaka kuendelea na miradi mengine inayofadhiliwa na TASAF.
Aliyaeleza hayo wakati akifungua mafunzo ya siku 10 kwa wawezeshaji kuhusiana na kaya masikini kisiwani Pemba katika ukumbi wa Tassaf Chake Chake.
Aliwataka wawezeshaji hao kuendelea kuipatia sifa kubwa Pemba katika kutoa kwao taaluma na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema wananchi wana matumaini kwamba TASAF awamu ya tatu itatoa matunda bora zaidi yatakayosaidia kupunguza kasi ya umaskini.
Alisema mpango huo wa kunusuru kaya masikini zipatazo milioni 1.2 zilizo katika mazingira magumu na hatarishi kwenye vijiji, shehia na mitaa, unalenga kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake, Meneja Msajili ya Walengwa, Phillipien Mmari, alisema awamu ya tatu ya amradi huo utakamilika mwaka 2012.