Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji ya askari wa polisi na mgambo mmoja ambao waliuwawa kwenye tukio la uvamizi wa kituo cha polisi cha Kimanzimchana walaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani Juni 11 mwaka huu.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Kusini Pemba ACP Juma Yussuf Msige amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Hamis Othman Mzee maarufu kwa jina la Hamis Mabunduki na makachero walifanikiwa baada ya kufuatilia nyendo zake na kumkamata wakati wa mchana akiwa mafichoni katika kijiji cha Matale Chake Chake Pemba na hivi sasa wanawasilaina nawenzao wa Pwani kwa ajili ya upelelezi zaidi