STATE HOUSE ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuonesha kitu Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino baada ya mazungumzo yao alipotembelea Ikulu Mjini Zanzibar leo na Mkewe Princess Akishino,[Picha na Ramadhan Othman)
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 04 Julai, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema visiwa vya Zanzibar vimeendelea kuvutia wageni wengi kutokana na utajiri mkubwa wa historia yake na uthiri wa utamaduni wa watu wake pamoja na mazingira mazuri ya kuvutia.
Akizungumza na Mwanamfalme wa Japan Akishino pamoja mkewe Ikulu leo, Dk. Shein amesema pamoja na visiwa vya Zanzibar kubahatika kuwa na fukwe maridadi zinazovutia watalii wengi lakini nafasi yake katika historia iliyopelekea kutembelewa na watu kutoka nchi mbali mbali ulimwenguni kwa karne nyingi imevifanya visiwa hivyo kuwa maarufu hivyo kuendelea kuvutia wageni wengi.
Alimwambia mwanamfalme huyo ambaye yuko nchini kwa ziara maalum kuwa historia ya Zanzibar imeunganika na mataifa mengine ulimwenguni hivyo ni vigumu kuandika au kuzungumzia historia ya watu wake bila kugusia mataifa mengine.
Alitolea mfano mji mkongwe kuwa moja ya urithi wa uthibitisho wa makutano ya tamaduni kutoka nchi mbalimbali hadi sehemu hiyo ya mji wa Zanzibar kuwa uthiri wa dunia chini ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni ya Umoja wa matyaifa-UNESCO.
Katika mazungumzo hayo Dk. Shein ameishukuru pia Serikali na wananchi wa Japan kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiipatia Zanzibar na ametolea mfano sekta ya huduma za jamii na miundombinu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amempongeza Mwanamfalme Akishino na mkewe kwa kuitembea Zanzibar na amemueleza kuwa milango iko wazi kwa Mwanamfalme huyo kutembelea Zanzibar wakati wowote.
Dk. Shein alieleza matumaini yake kuwa ziara hiyo ya Mwanamfalme huyo itafungua njia kwa watalii wengi kutoka Japan kutembelea Zanzibar .
Kwa upande wake Mwanamfalme Akishino amemueleza Mhe Rais kuwa ni mara yake ya kwanza kutembelea Zanzibar na anatarajia kujifunza mengi kuhusu Zanzibar kwa kutembelea sehemu mbalimbali.
Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim,Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Bi Hindu Hamad Khamis na Balozi wa Tanzania nchini Japan Balozi Salome Sijaona.
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino alipowasili Ikulu mjini Zanzibar leo akifuatana na Mkewe Princess Akishino na baadae kufanya mazungumzo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akifuatana na Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino mara walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leoRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuonesha kitu Mwana Mfalmewa Japani Prince Akishino baada ya mazungumzo yao alipotembelea Ikulu Mjini Zanzibar leo na Mkewe Princess Akishino,[Picha na Ramadhan Othman)