Mtunda ambao ulipandwa Kundemba mnamo mwaka 1982-1983 na kubatizwa jina la Mkundemba Leo hii umetuaga rasmi kwa kukatwa kutokana na chini kuwa umeshaoza sana na kuhatarisha usalama na amani kwa wakaazi wa hapo.
Mtunda huu ndipo lilipokuwa duka maarufu la Alwatan wa Kundemba Ali Kibanda.
Kwa wakaazi wa Kundemba walio ughaibuni ambao wanaufahamu vizuri sana mtunda huu ambao ulipandwa na Marehemu Hassan Wigi wakija kutembea kwa leo wataona tofauti imetokea mtaani kwao