Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Jamii yahamasishwa kupima TB

$
0
0
Na Zainab Anuwar
WASTANI ya watu 64,000 huugua kifua kikuu kila mwaka nchini Tanzania, sawa na wagonjwa 176 kwa kila siku.
Hayo yalielewa na Daktari Damana wa hospitali ya Kuu ya Mnazi Mmoja katika kitengo cha maradhi ya kifua kikuu na ukoma,Ali Ahmad, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mnazi Mmoja .
Alisema watu wengi wanapata maambukizo ya maradhi ya kifua kikuu na ukoma kwa sababu ya kutogundua mapema dalili zake na jinsi ya kujikinga.
Alisema hadi sasa kuna jumla ya wagonjwa 685 wanaoendelea na matibu katika hospitali za Unguja na Pemba.
Hivyo, aliwataka wananchi wanapoona wana dalili za kifua kikuu wafike hospitalini mapema kwa sababu ugonjwa huo unatibika.
Alisema watu walio kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo ni watu wanaoishi na VVU na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Kundi jengine ni la wazee walio na umri wa kuanzia miaka 65, watu wenye magonjwa wa muda mrefu kama vile kisukari, saratani pamoja na watoto wenye utapiamlo.

Daktari huyo alisema wanakabiliana na changamoto mbali mbali katika kupunguza ugonjwa huo ikiwemo jamii kuuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>