Na Himid Choko BLW.
DAR ES SALAAM July 14, 2014
Kamati ya mashauriano ya bunge Maalum la Katiba inatarajiwa kukutana kutathmini kazi zilizofikiwa za utungaji wa katiba mpya ya Tanzania.
Kamati hiyo inatarajiwa kukutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 24 mwezi huu katika ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Daresalaam.
Taarifa iliyotolewa na katibu wa bunge maalum la katiba Yahya Khamis Hamad imeeleza kuwa kamati hiyo inawajumuisha wajumbe thelathini walioteliwa na Mwenyekti wa bunge hilo Mh Samwel Sita kwa kushirikiana na Makamu wake Mh Samia Suluhu Hassan.
Uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo ya mashauriano ya bunge hilo ni kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 54(4) na (5) ya kanuni za Bunge Maalum za mwaka 2014.
Taarifa hiyo imewaomba wajumbe walioteuliwa kuhuduhria kikao hicho kwa lengo la kufanikisha kazi waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Watanzania.