Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mama Mwanamwema Awaandalia Futari Watoto Mayatina wa Mazizini Zanzibar.

$
0
0
Na Mwantanga Ame
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto, Asha Abdalla , amesema serikali itaendelea kuwawekea mazingira ya maisha bora kwa watoto wanaoishi katika nyumba ya kulelea watoto ya serikali    na wale ambao wanamazingira magumu waliopo katika maeneo mbali mbali ya visiwa vya Unguja na Pemba.
Katibu huyo, aliyasema hayo jana jioni , huko nyumba ya kulelea watoto ya serikali   Mazizini Mjini Unguja, baada ya watoto wa nyumba hiyo, kula chakula cha futari pamoja na Wake wa Makamu wa Pili wa Rais, Pili Juma Iddi, na Asha Suleiman Iddi, futari ambayo ilitayarishwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein.
Alisema watoto wanaoishi katika nyumba hizo  wanakabiliwa na mazingira magumu  ya maisha yao na serikali itahakikisha kuwa inaendelea kuwapatia misaada mbali mbali itayoweza kuwapa maisha bora.
Alisema Wizara yao, inafarijika kuona watoto hao wamekuwa wakipata msaada kutoka serikalini, jambo ambalo limeweza kuwaondoa katika utengano katika jamii, jambo ambalo linawafiriji kujiona wako sawa na watoto wengine.

Nae Mtoto wa anaeishi katika nyumba hiyo, Mulhat Ismail, akitoa shukrani kwa niaba ya watoto wenzake, alimpongeza Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, wake wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Suleiman Iddi, Pili Juma Iddi,  na wake wa viongozi kwa jitihada zao wanazozitoa kuzisaidia nyumba hizo, kwani zimewafanya kujisikia kuwa sawa na watoto wengine.
Hata hivyo, alieleza kwamba jambo la msingi kwa serikali kuona wanawasaidia zaidi katika suala la kupata elimu bora, ili waweze kukabiliana na maisha yao hapo baadae, huku wafadhili wengine kuona umuhimu wa kuvisaidia vituo hivyo.
Futari hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis, na baadhi ya Wake wa Wawakilishi na Wabunge.
Watoto wanaoishi katika nyumba hiyo, ni Chimbuko la Muasisi wa taifa la Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ambapo alianzisha nyumba hizo ikiwa ni hatua ya kuwasaidia watoto yatima kuwa na makaazi na huduma bora za maisha

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>