WAANDISHI wa habari kutoka Nchi za Afrika wakiwasili katika Jengo la Gazeti la China Daily mjini Beijing, kuona utendaji wa Kazi za Uandishi wa magazeti wa China Daily wakiwa katika ziara ya Kimafunzo Nchini China, Jumla ya Waandishi na Maofisa habari wa Nchi 11 za Afrika wameshiriki mafunzo hayo.kwa Nchi za Afrika zinazizungumza Kingereza.(Picha na Othman Maulid Beijing China)
AOFISA Habari na Waandishi kutoka Nchi za Afrika wakiwa katika chumba cha mikutano katika Ofisi za Magazeti ya China Daily Mjini Beijing wakifuatilia historia ya kuazishwa kwa Magazeti ya Lugha ya Kingereza na kusambazwa Nchi mbalimbali Duniani(Picha na Othma Maulid Beijing China)
MAOFISA Habari na Waandishi wa habari kutoka Nchini Afrika wakimsikiliza Deputy Editor -in-Chief Ndg. Gao Anming, akitowa historia ya uazishaji wa Magazeti ya China Daily wakati wa ziara yao kutembelea Ofisi hizo mjini Beijing leo (Picha na Othman Maulid Beijing China)
WAHARIRI wa China Dailry wa kwanza Deputy Editor -in-Chief Ndg. Ji Tao, Deputy Editor -in-Chief Ndg. Gao Anming na Deputy Editor -in-Cheif Bi. Han Lei, wakisikiliza michango na maswali walioulizwa na Maafisa habari kutokana na uendeshaji wa magazeti ya China Daily wakati wa ziara yaokutembela Ofisi za magazeti hayo Mjini Beijing China leo,24-7-2014.(Picha na Othman Maulid Beijing China)
DEPUTY Editor -in-Chief wa China Daily Ndg Ji Tao, akitowa maelezo ya Gazeti la China Daily husambazwa katika Nchi za Kenya, South Africa, Nigeria, Ethiopia na Tanzania, huandika habari mchanganyika kutoka Afrika na China, gazeti hiloimezinduliwa mwaka 2012 Nchini Kenya.(Picha na Othman Maulid Beijing China)