Jeshi la Polisi kisiwani Zanzibar, hatimaye limemfikisha mahkamani Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa mwakilishi wa Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mansour Yusuf Himid
Wakati akisomewa mashitaka hayo mwendesha mashtaka kutoka ofisis ya Mkurugenzi wa mashitaka( DPP) Maulid Ali amesema mtuhumiwa huyo mnamo Agosti 2, mwaka huu majira ya saa 7.18 huko nyumbani kwake Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar alikutwa na silaha aina ya pistol (Director) yenye namba F76172 W.
Kitendo hicho cha kumiliki silaha kimedaiwa mahkamani hapo kuwa ni kwenda kinyume na kifungu cha sheria no 6(3) na 34 (1) (2) cha sheria ya silaha na risasi No 2 ya mwaka 1991 sura ya 223 sheria ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania.
Kosa la pili linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kupatikana na risasi za moto 295 za pistol jambo ambalo pia ni ni kosa kisheria.
Aidha Kosa la tatu ni kupatikana na marisau 112 ya bunduki aina ya short gurn( gobore) baada ya marisau 50 aliyotakiwa kuwa nayo kisheria.
Kwa upande wake mtuhumiwa Mansour aliyakana makosa yote hayo matatu aliyosomewa Mahakamani hapo.
Kosa la pili linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kupatikana na risasi za moto 295 za pistol jambo ambalo pia ni ni kosa kisheria.
Aidha Kosa la tatu ni kupatikana na marisau 112 ya bunduki aina ya short gurn( gobore) baada ya marisau 50 aliyotakiwa kuwa nayo kisheria.
Kwa upande wake mtuhumiwa Mansour aliyakana makosa yote hayo matatu aliyosomewa Mahakamani hapo.
Kwa kuwa mahkama hiyo ya mkoa haina uwezo wa kutoa dhamana kwa kosa la aina ya kwanza isipokuwa makosa mengine mawili, mshtakiwa hakupata dhamana na kesi yake iliahirishwa hadi tarehe 18 mwezi huu atakapopelekwa tena mahkamani.
Kwa mujibu wa wanasheria wake, sasa wanajiandaa kuomba dhamana kupitia Mahkama Kuu.
Wanasheria hao wakiongozwa na wakili mzalendo Omar Said Shaaban akishirikiana na wakili Gasper Nyika ambaye ni mshirika wa wakili Fatma Karume; leo asubuhi waliwasilisha ombi mahkama kuu la “Habeas Corpus” kuhusiana na mteja wao Mhe. Mansour Yusuf Himid na lilisikilizwa na Jaji Abraham Mwampashe, ambapo aliamuru mshtakiwa apelekwe mahkamani. Baadae “court order” ilichapwa na kupelekwa polisi kwa utekelezaji.
Hata hivyo Hakimu Khamis ameiakhirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 mwaka huu kwa kutajwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande hadi tarehe hio wakati kesi yake itakapotajwa tena.
Chanzo: Zanzibari yetu