Bi Mwanaidi Saleh amewasili jana akitokea Nchini India baada ya kupata matibabu ya majeraha yake ya kuungua kwa moto miezi Sita iliopipita.
Kwa mujibu wa Daktari alieongozana nae Nchini India amesema kwa kiasi kikubwa matibabu yake yamefanikiwa na anaendelea vizuri.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ndege ya Shirika la Ndege la Oman Air, mnamo saa kumi na moja jioni, Bi Mwanaid amepelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kuendelea na matibabu yake akiwa katika hali nzuri ya kiafya.
Kwa kipindi hiki atakuwa katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu na kuendelea, akiwa katika wodi ya Wanawake ghorofa ya tatu.
ZanziNews inatowa shukrani za dhati zinazotoka moyoni kwa Wananchi wote waliojitokeza katika kufanikisha safari yake Nchini India kwa matibabu kwa kutowa michango yao kumsaidia Bi Mwanaid Saleh kuweza kumsafirisha. Pia wale ambao hawakubahatika kuchangia lakini walimwombea du'aa pia tunawashukuru kwa duaa zao.
Hakuna mwengine wa kuwalipa isipokuwa Allaah Subhaanahu Wata'ala na InshaAllah aijaalie michango yenu iwe katika mizani ya amali zenu njema siku ya siku.