Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wananchi Ulanga wakumbushia ahadi za JK

$
0
0
Na Mariam Kamgisha, Ulanga
WANANCHI wa jimbo la Ulanga Magharibi, wilayani Ulanga mkoani Morogoro, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete, kutimiza ahadi yake  aliyowapa wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 za kuwapatia wilaya mpya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji na makao makuu ya tarafa nne za wilaya hiyo za Lupiro, Mtimbira, Malinyi na Ngoheranga, baadhi ya wananchi hao,walidai wanashangazwa na ugumu unaojitokeza katika upatikanaji wa wilaya mpya, wakati Rais Kikwete aliwaahidi wakati wa kampeni.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao walibainisha umuhimu wa wilaya mpya ili kusogeza huduma za kijamii na za kiuchumi kwa karibu, huku wale wa Minepa, wakimtuhumu diwani wao Athumani Kapati kuwashawishi wananchi kukubali Lupiro iende Ulanga mashariki, huku diwani huyo akikanusha madai hayo.


Wananchi hao walidai wana hofu kuwa mchakato huo umeanza kuingiliwa na mmoja wa viongozi wa juu serikalini, ambaye anatoka Ulanga Mashariki, (Celina Kombani, Mbunge wa Ulanga Mashariki na Waziri wa nchi ofisi ya Raisi, Utumishi) ambaye anafanya kampeni za kukwamisha mchakato huo.

Aidha aliwasema Waziri huyo anawashawishi wataalamu wa wilaya na mkoa wakubali tarafa ya Lupiro ihamishiwe Ulanga mashariki kwa maslahi yake binafsi.

Walidai kiongozi huyo huwaeleza watu wa Malinyi kuwa iwapo Lupiro itaaondoka katika jimbo hilo, makao makuu yatakuwa Malinyi na vivyo hivyo akiwaeleza wananchi wa Mtimbira kuwa wakifikia maamuzi hayo, basi makao makuu ya wilaya yatakuwa katika eneo hilo, mambo ambayo yanalenga kuwachanganya wananchi.


Akizungumza na wananchi hao,Mbunge wa jimbo la Ulanga Magharibi, Dk. Haji Mponda, aliwataka kuwa na subira wakati serikali ikiendelea na mchakato wa kupata wilaya mpya, na kukiri iwapo Lupiro itaondolewa Ulanga magharibi, kuna hatari ya jimbo hilo kukosa wilaya, kwani jimbo hilo lina tarafa nne tu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>